sisi na Tanzania

sisi na Tanzania

Mbunge wa CCM

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2009
Posts
475
Reaction score
25
hi waungwana.
leo nimejiunga rasmi uwanjani hapa JF. ni matarajio yangu kuwa tutaendelea kuwasiliana na ndugu wote na kubadilishana mawazo na michango mbalimbali kwa maendeleo yetu kama binadamu na nchi/taifa letu kama mahali ambapo Mungu alipenda tuishi sisi na vizazi vyetu.

kama lilivyo jina langu, ndivyo ilivyo dhamira yangu pia. niko katika matayarisho ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao. sina shaka kuwa wana JF watanisaidia kwa namna moja au nyingine ktk kufikia azma yangu hii kupitia mchango yao ya mawazo, ushauri nk.

nimekuwa nikitoa mawazo yangu siku za nyuma kupitia tovuti ya gazeti la Tanzania Daima, lakini cha kushangaza wahusika wameamua kufunga fursa ile bila hata kuwashirikisha wadau. nadhani yoyote mwenye kujua faida za kupashana habari hawezi kamwe kufikiri kupunguza fursa za habari na majadiliano.

nashukuru sana na natangaza rasmi kuwa sasa nimeingia JF

Mungu ibariki Tanzania
 
hi waungwana.
leo nimejiunga rasmi uwanjani hapa JF.
karibu sana mzee usisahau kujitambulisha kule mahali pake!
kama lilivyo jina langu, ndivyo ilivyo dhamira yangu pia. niko katika matayarisho ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao
Chama gani?.
lakini cha kushangaza wahusika wameamua kufunga fursa ile bila hata kuwashirikisha wadau
.
walivyofungua walikushirikisha?
 
ni kweli kimey walivyofungua hawakunisirikisha, na hata tulipoanza kuutumia hatukuwashirikisha! hata hivyo ujumbe mkuu hapo ni kuwa ilikuwa fursa muhimu na imeondolewa.

kuhusu chama gani, nafikiri nitasema baadaye, labda atika hali private kidogo.

naomba nisaidie huko kwingine kwa kujisajili ni wapi tena, si unajua tena mie mgeni kwenye JF?
nashukuru
 
Nadhani alitaka kusema kwenye Ukumbi wa Utambulisho na sii hapa kwenye ukumbi wa siasa..Ielewe tu kwamba ukumbi huu unajadili SIASA, sii vizuri kuanza kukujadili wewe kwa sababu tu ni Mwanasiasa..Hivyo utaona kwamba kichwa cha mada yako kimetupelekea kufikiria vitu tofauti kabisa na maelezo yaliyofuatia...
 
sii vizuri kuanza kukujadili wewe kwa sababu tu ni Mwanasiasa..Hivyo utaona kwamba kichwa cha mada yako kimetupelekea kufikiria vitu tofauti kabisa na maelezo yaliyofuatia... [/QUOTE said:
si vizuri sana kujadili wanasiasa kwani kwa kufanya hivyo si tu mnapoteza muda wa ujadili masuala muhimu, bali pia mnaharakisha kuwaua kisiasa hao wanasiasa. mi si mmoja wa wanasiasa wanaopenda kujadiliwa.

kichwa cha habari kinaendana na dhamira ya ndani ya mwanasiasa yoyote wa kweli kiuhalisia. najua TZ sasa tunafahamu vizuri tofauti ya wanasiasa wasio wanasiasa na wanasiasa halisi, ndio maana sasa tunazungumza habari ya kutenganisha siasa na mambo mengine.

mimi na tanzania, sisi na tanzania... sote na tanzania, ni kauli halisi ya mzalendo halisi
 
Mkuu wangu weee Ujumbe wako ni kujitambulisha..HAIHUSU, ktk ukumbi huu.
Haya ya sisi sote ni watanzania siyaoni mahala popote ktk maelezo yako..Ebu chukua pumzi kidogo, upate kueleweshwa maanake inaonyesha wazi kutaki hufahamishwa ila yale unayoyaona wewe.
 
Back
Top Bottom