Sisi ndio nchi pekee yenye amani EAC " - Kenani Kihongosi

Sisi ndio nchi pekee yenye amani EAC " - Kenani Kihongosi

KIJICHO PEVU

Member
Joined
May 4, 2024
Posts
69
Reaction score
49
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Laban Kihongosi, amewataka wamiliki na wafanyakazi wa saluni jijini Arusha kufanya kazi kwa bidii, kutunza kipato chao, na kuendelea kuishi kwa mshikamano na amani, hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Akizungumza na wamiliki na wafanyakazi hao wanaojumuisha vinyozi, wasusi, na watengeneza kucha siku ya jana Julai 22, Kihongosi amesema kuwa utulivu wa nchi ni msingi wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, hivyo akawataka kuhakikisha wanahifadhi hali hiyo kwa vitendo.

Aidha, Kihongosi alisisitiza kuwa Tanzania imeendelea kuwa kisiwa cha amani ukanda wa Afrika Mashariki, na hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kulinda hali hiyo na kuikataa mitazamo inayoweza kuvuruga umoja wa kitaifa.

“Afrika Mashariki nchi pekee yenye utulivu ni sisi (Tanzania) peke yake, sisi hatujagombana, wanatamani wageni watuchochee, tuvurugane, tugombane, ili waje wafanye mambo yasiyofaa ndani ya nchi yetu, tukiharibu hii hatuna nyingine”, ameongeza.

 
Back
Top Bottom