Sisi wafuasi wa Hayati Magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Rais Samia

Yaani kama wewe ni mfuasi wa maiti/mfu/alieoza/msukule hapa tayari ni tatizo.

Utakuwaje mfuasi wa mfu kama wewe sio mfu kichwani!?

Walio hai hawana ushirika na waliokufa labda km ww ni mchawi.
Namaanisha fikra na falsafa zake, viongozi wakifa fikra zao bado zinaishi
 
First paragraph ungeandika kwa herufi kubwa.
 
sisi wafuasi wa Magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Samia baada ya kutoka Ulaya, tunauliuza watu hawa walikuwa chama kimoja kweli? Achilia mbali kuwa kwenye ticket moja ya kupigiwa kura...
[emoji1787]
 
sisi wafuasi wa Magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Samia baada ya kutoka Ulaya, tunauliuza watu hawa walikuwa chama kimoja kweli? Achilia mbali kuwa kwenye ticket moja ya kupigiwa kura...
Kwani mradi gani ulikwama?
 
Nchi gani iliyowahi kuuzwa Mzee? Acha kukalia akili ndg
China wananunua ardhi kibao Afrika na Carribean huko, nchi haiwezi kuuzwa kama embe ila inaweza kuingizwa kwenye mikataba ya ajabu na rasilimali zake zikatwaliwa, na uwezo wake wa kujiamulia ukawa umepunguzwa
 
Unampangia Rais atawale kama unavyotaka kuna wafuasi wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa,Kikwete, hawa wote muda wao umepita sasa hivi ni muda wa Rais Samia na yeyye muda wake utapita Rais hayupo kufurahisha wafuasi wa mtu.
 
Poleni sana mnaoumia wakati huu, waswahili husema kutesa kwa zamu..!!! Vumilieni na mvumilie sana maana mpaka 2035.
 
Tunachopaswa ni kushukuru Mungu na aidha kumsaidia mama au kutuliatu.
Haiwezekani kulazimisha mama kufuata njia za Magufuli,kama ilivyoshindikana kulazimisha Magufuli kufuata njia za Jakaya
Tukubaliane na mapenzi ya Mungu jamani
So hiki ni chama gani sasa ambapo kila kiongozi haiamini anachofanya mwenzake ila anamshangilia?, lazima tu confront haya maswali magumu, na tutapataje maendeleo kama tukiwa na taifa la wanafiki na waongo kiasi hiki?
 
Na itikadi ya CCM ni ipi, na JPM aliitekeleza vipi kiasi cha kuona ndo alikuwa sahihi na Samia ana-miss vipi?

Au ndo ile mkikutwa mmejiopanga barabarani mnaambiwa nchi hii ni tajiri na hatuhitaji misaada wakati uhalisa ni:-

View attachment 2125546
Hivi mkuu umemsikia Samia kuhusu mambo ya Sekta binafsi kuingizwa kwenye miradi ya Serikali?

JPM hili alilikataa kata kata, hawaaminiki hawa
Ila Samia kasema kuna wafanyabishara kutoka Ulaya ambao watakuwa wakitoa hela zao kwenye miradi ambayo hugharimikiwa na Serikali,
Yaani huoni tofauti ya Samia na Magufuli kweli? Hata la kuruhusu wanafunzi wenye mimba, chanjo, kwa shinikizo la mabeberu?
 
Ushawishi gani utawapa wazungu wakupe hela bila wao kufaidika na chochote? Ndo maana hii misaada inatolewa kwa mikataba yenye masharti lukuki, kwa kiongozi mwerevu akitafakali impact ya hayo masharti hawezi kukimbilia misaada ya hawa watu.
Ushawishi gani kwani hawajatoa criteria za kupata pesa? Unapoenda Benki Kukopa huwa unapeleka nini Ili kujenga hoja ya kupata pesa?

Unaelewa maana ya bankable business plan? Watu mliosoma history mna matatizo Sana.
 
We mdau mwenye yale maneno ya viongozi wa chadema dhidi ya lowasa kabla ya 2015 na baada ya kufika 2015 walipomkabidhi kijiti cha kuiongoza katika mbio za uraisi tafadhali tupia ili mtoa mada nae aone halafu atuambie twende wapi!!! Ahsante
Kwa hiyo tuna justify upumbavu wetu kwa kuangalia walichofanya chadema?
 
Ukosefu wa itikadi ndicho kinachowafanya ninyi kuwa wafuasi wa marehemu na bado mnajitangaza hadharani.Marehemu wenu alikuwa na itikadi gani?
CCM ni janga la Taifa na wafuasi wake ni watu wenye kuabudu wafu.
Hivi mkuu watu wanavyoenzi fikra za akina Mandela, Mao, Nyerere, Martin Luther King Jr, hawa ni wanaabudu wafu?
 
Kuendelea kufikiri kuwa CCM itakuja kuwaletea Maendeleo Watanzania ni kujipumbaza,CCM ni janga kwa Taifa letu.
 
Hakuna ubaya sisi kuwa tegemezi bila aibu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…