sisi wafuasi wa Magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Samia baada ya kutoka Ulaya, tunauliuza watu hawa walikuwa chama kimoja kweli? Achilia mbali kuwa kwenye ticket moja ya kupigiwa kura.
Tunauliza where is our pride? Maneno haya ni kinyume kabisa na kujiamini alipotupa Magufuli na Kabudi...na wana CCM wengi walivyo wanafiki wanampigia makofi kama walivyopiga kwa Magufuli, ndiyo maana kuna wakati najiuliza CCM ni chama cha siasa au ni genge tu la watu wanaolindwa na mabunduki kujipa madaraka na kula kodi zetu?
Ni chama gani cha siasa kisichokuwa na itikadi? Ukiwaambia hii haifai wataitikia na kushangilia, kesho mwingine anakuambia inafaa wanashangilia tena, hiki ni chama kweli? Tunapata wapi confidence ya kuwakejeli vyama vingine kama chama chetu kipo hivi?
View attachment 2125025