Sisi wafuasi wa Hayati Magufuli tumeumizwa sana na maneno haya ya Rais Samia

Magufuli hakukataza wawekezaji, ila akiweka masharti tu Tanzania pia ifaidi

Wawekezaji hutakiwi kuwawekea masharti magumu,,,acha wafanye biashara zao kama wazawa, muhimu wanalipa kodi za serikali kama mzawa anavyolipa,, Sasa ukimuwekea masharti unadhani atakukalia!!!! Kuna manchi kibao hawana masharti na zinasonga mbele kimaendeleo mfano uganda, kenya n.k. kenya wananufaika mno na mapato ya wawekezaji. Tembea uone kaka
 
Huu ndio ufala alioukataa JPM, kupigia magoti hao wanyonyaji wanaoitwa wawekezaji...na tulinchagua kwa kishindo, Samia asitake kuharibu, sisi tulimchagua JPM kwa ajili hiyo
 
Stop compromising people and let our beloved one rest ease in the eternity!!!.

Yes he is dead....but the visions and the legacy left behind by Magufuli will last for generations.
 
Unataka kusema Kenya hawana masharti ya wawekezaji? Alafu unafikiri sisi watanzania kipimo chetu ni Kenya.
Hovyo kabisa.
 
Tumekuwa kama Mzee Matonya.
 
Huu ndio ufala alioukataa JPM, kupigia magoti hao wanyonyaji wanaoitwa wawekezaji...na tulinchagua kwa kishindo, Samia asitake kuharibu, sisi tulimchagua JPM kwa ajili hiyo
Mh.Samia(Rais wa JMT) atambue kwamba hatukuwahi kumpigia kura hata moja ya urais. Kila kitu amekipata through virtue and anonymity. She should play safe....sio kuigawa nchi. Hawezi kuwa anatoa kauli za kuiponda awamu ya tano utafikiri hakuwa sehemu ya uozo huo.
 
Mkiumia sana mkichoka jinyongeni wenzenu wengi tuu wanajiua pindi hii!! Hasa Geita ndovifo vyaajabu nje-nje... nakamba jero tuu
 
''Lakini pia tumeweza kukwamua miradi iliyokuwa imekwama, kama mnavyojua katikati hapa tulichokozana kidogo na umoja wa Ulaya uhusiano ukatetereka miradi ikakwama, Lakini tumeshakwamua fedha mradi mmoja umeshatiliwa na mwingine utatiwa hivi punde, kazi zitaendelea.''
 
Unataka kusema Kenya hawana masharti ya wawekezaji? Alafu unafikiri sisi watanzania kipimo chetu ni Kenya.
Hovyo kabisa.

Hata kama yapo lakini hayafanani na yakwetu. Wenzetu wanajali na kuthamini wawekezaji,,,sasa wakati wa magufuli na nyerere hawakuonyesha haya.


Huyu mama namwaminia sana, tangu aingie nchi imeanza kupendeza, wawekezaji wanamiminika, vijana wanapata ajira. Huyu ndiye rais wawanyonge.
 
Huu ndio ufala alioukataa JPM, kupigia magoti hao wanyonyaji wanaoitwa wawekezaji...na tulinchagua kwa kishindo, Samia asitake kuharibu, sisi tulimchagua JPM kwa ajili hiyo

Ulimchagua kwa ajili hiyo wakati wananchi hawana hela,,,tajiri/mwekezaji akiumia masikini haponi na hata serikali inakoswa kodi, Tangu migodi aifunge wananchi wangapi wamerudi manyumbani!!! Maelfu ya wananchi hawana makazi.


Mama samia tunakuombea afya njema na umri mrefu wewe na familia yako,,umekuja kulikomboa taifa. Hakika wewe ndiye rais wa wanyonge.
 
SSH ni mkweli embe analiita embe haliiti tunda la mwishoni mwa mwaka. Ni mkweli kwa maana hawapi watu anaowaongoza matumaini ya utajiri wa bandia.

Anaitazama sasa yenye uhalisia sio ile baadae ya matumaini ambayo kuifikia ni mpaka tutoke jasho jingi na tuumize sana vichwa vyetu.

Sisi ni tajiri wa rasilimali lakini hatuna bado ujanja wa kuzigeuka rasilimali hizo leo hii zikawa fedha, ni mpaka watu wetu wasomeshwe na wawe na mitazamo ya wanaotafuta kweli utajiri.

Ni kumvimbia mzungu ni kupoteza muda tu, lazima mmoja ajishushe kwa kutumia hekima ili watu wake wafaidike na kinachoweza kupatikana.
 
Juzi nilikuwa nasikiliza wimbo alotunga Mbaraka Mwinshehe Mwaruka unohusu kamati kuu ya /TANUCCM kupitisha uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma.

Serikali ilipaswa kuhakikisha suala hilo ni la kitaifa na wananchi wanaelewa.

Ila JPM alijitahidi kuhakikisha serikali yahamia huko Dodoma lakini hadi leo watu washinda Dar-es-Salaaam na viongozi wengi wanapinga suala hilo.

Raisi Samia ametuangusha sana watanzania tunoamini katika kujitegemea khasa kwenye suala la mikopo ya nje na kutotaka kujitafutia pato la ndani na kubuni vyanzo mbalimbali vya fedha vya ndani.

Januray Makamba nae bungeni hajibu masuali ya msingi kuhusu uhakika wa umeme nchini, hii serikali ina lengo lipi khasa?

Tuhakikishe bwawa la Nyerere linakamilika ili kuondoa tatizo la umeme ambao ukiwepo wa kutosha viwanda vingi9 vitajengwa, ajira zitapatikana, bidhaa za ndani zitazalishwa na pato la taifa GDP litakua.

Serikali ibuni njia mbadala za kupata fedha za ndani tusiwe wavivu na tupunguze kukopa nje.

Twangojea kuona uchaguzi wa 2025 fedha zitatoka wapi, na je leo hii fedha za ndani zote zaenda wapi?
 
Hakusema miradi yote tunajenga kwa fedha za ndani, na ambayo tulikuwa tunakopa alisema
Tanzania kwani haikuwa uhusiano na mataifa mengine kipindi cha Magufuli? Kuna ubalozi ulifungwa Tanzania kisa Magufuli?
Roeland van Geer alikuwa Balozi wa EU hadi November 2018, alirudishwa kwa sababu ya kuzorota mahusiano kati ya Tz na Jumuiya ya Ulaya. Soma zaidi hapo chini

 
Huu ndio ufala alioukataa JPM, kupigia magoti hao wanyonyaji wanaoitwa wawekezaji...na tulinchagua kwa kishindo, Samia asitake kuharibu, sisi tulimchagua JPM kwa ajili hiyo
Johnny Sack wewe ndiye fala, unamdanganya nani kuwa tulimchagua JPM?

Magufuli aliiba kura kibwege!! Hamna namna kwa Tanzania ya leo mgombea anaweza kupata zaidi ya 62%. Eti yeye anadai 80% kwa kura za nani? Ndiyo maana limekufa mapema na likatembezwa mzoga mikoa 5 kudhalilishwa
 
Alikopa wapi na kiasi gani?
Credit Suisse, AfDB, EADB, Standard Chartered Bank, CRDB (Ikiwakilisha mabenki mengi), Exim Bank of China.

Amekopa Tsh 29 Trillion kati ya 2016-21 alipokufa
 
Mabalozi kurudishwa nyumbani kama wasipofuata protocol za kibalozi ni sawa..ila ubalozi wa EU haukufungwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…