Sisi watanzania ni wachafu sana ndio maana wageni wakija tunafukuzwa mjini ,wageni 36 tu shule ,masoko zimefungwa!

Panga wewe halafu nenda, ndugu zako watakuzika bila usumbufu, shida mnaleta dharau kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, nakuhakikishia tuna vijana wana uwezo mkubwa sana hapa Tanzania wewe jichanganye
Vijana wenu hao hawahusiki na kuwalinda wananchi wa Tanzania? Make kuna watu wameshambuliwa sana hapa nchini kama Tundu Lisu, Prof yule wa Sheria, Dr Ally Kibao, au wao ndiyo wasiyojulikana.
 
Vijana wenu hao hawahusiki na kuwalinda wananchi wa Tanzania? Make kuna watu wameshambuliwa sana hapa nchini kama Tundu Lisu, Prof yule wa Sheria, Dr Ally Kibao, au wao ndiyo wasiyojulikana.
Vikosi vya ulinzi na usalama vina Department nyingi sana, acha kufananisha Lissu na kiongozi wa nchi , ulinzi wao ni tofauti, hata US kuna ulinzi mkali sana lakini Kenedy alipigwa risasi na Trump alipigwa risasi ya sikio, makosa yapo ila haina maana kuwa US sio bora kwenye ulinzi
 
Watanzania wengi kwa uchafu ni wachafu hasa, isipokuwa Moshi,
Viongozi nao ni wachafu kuanzia Balozi wa nyumba kumi, Mw/kiti wa mtaa ama kijiji, mkuu wa wilaya, mkoa hadi ngazi kuu.
Mfano nenda tu Unguja kisiwa kichafu utadhani hakina viongozi, au Mbagala pachafu balaa,
Kuhamasisha usafi ni hadi wakati wa uchaguzi, aibu sana, nani katuronga Watanzania?
 
Katika mkoa mchafu Tanzania ya kwanza ni Dar.
Huo mkutano bora wangepeleka Moshi au Arusha au hata Dodoma.

Dar posta tu ile ukishuka chini hapa kwenye fukwe unaweza jiuliza marambili sisi waTz tuna shida gani kila kitu chetu ni hovyo.
Dodoma au Moshi una Hotel za kuwalaza hao wageni? Hivi unajua kila Rais wa nchi anakuja na kundi la watu wapi? Bado makamu wa Rais na Mawaziri wakuu? Hapo hujataja watu mashuhuri, wafanyabiashara na viongozi wa Taasisi za kitaifa na kimataifa? Tupunguze ujuaji
 
Dar jiji lina kila harufu mbaya unayoijua huku Duniani.

Mamlaka zilitazame sana hili jambo.
Halafu Serikali mbona kuna mikoa wanaitelekeza na inaweza kuwa na potential sawa na Dar , mfano Tanga, Lindi na Mtwara.
Yaan,
Mkutano upelekwe mikoa ya kusini ambako huko msumbiji amani Hali Tete 🏃🏃🏃
 
Panga wewe halafu nenda, ndugu zako watakuzika bila usumbufu, shida mnaleta dharau kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, nakuhakikishia tuna vijana wana uwezo mkubwa sana hapa Tanzania wewe jichanganye
Kama hamzaa ilitumika nguvu kubwa ilitakiwa akamatwe akiwa HAI.

nyinyi mkamimina marisasi ovyo OVYO pale angetakiwa aambiwe ajisalimishe .

Kwa kua hakuna na akili hizo mka Angua PAPAI KWA KUTUMIA GOBOLE.
 
Wale ni polisi wa kawaida ndio maana nikasema vyombo vya ulinzi na usalama vina idara nyingi, tuna vijana wako vizuri sana
 
Barabara zenyewe za mjini ni mbaya na chafu, mitaa michafu huachi kuona uchafu ukizagaa zagaa hovyo
 
Sasa siku G5 wakijakufanya ziara Tz si wote tutaambiwa tujifungie majumbani hakuna kutoka nje labda tuchungulie madirishani.

Japo jiwe sikumkubali kiivyo lkn asingeruhusu watu wasiende kazini na watoto wasiende shule kisa kuna wageni wamekuja kufanya mkutano.
 
Panga wewe halafu nenda, ndugu zako watakuzika bila usumbufu, shida mnaleta dharau kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, nakuhakikishia tuna vijana wana uwezo mkubwa sana hapa Tanzania wewe jichanganye
Tumeambiwa kariakoo tu ndio huduma zitaendelea maana yake biashara zote
 
Sasa kama viongozi hawajali huo usafi utatokea wapi?!
Kwamba viongozi wakufanye wewe usiwe mchafu? Au mimi ndio sijakuelewa maana unakuta kubwa zima linakunywa maji ndani ya gari au daladala akimaliza anatupa chupa ya maji barabani kupitia dirishani. Hapo kiongozi anahusikaje na uendawazimu wa kubwa jinga kama huyu?
 
Wagange wapone ndugu Mganguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…