Sisi Watanzania tunashangaza; humsifia kila Rais, akiondoka tunaanza kulalamikia aliyotenda.

Kididimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
4,418
Reaction score
4,031
Sisi Watanzania tunayo sifa moja tofauti na wenzetu. Humsifia kila Rais anayekuwepo madarakani na kumpa majukumu ya kufikiria kila jambo kwa niaba yetu! Akiondoka madarakani tunaanza kulalama tena kichinichini kwa woga . Kuwa hili na lile hakutenda sawa.

Dr. Magufuli alinunua midege, tukamsifia sana, alipotwaliwa, hata Mh. Spika akamsema hadharani kuwa mradi wa ndege haukuwa na tija. Na ripoti kadhaa zikaonyesha namna ndege zinavyoiingizia nchi hasara.

Jana, tumeona ndege mbili zikishuka Zanzibar na kupokelewa na Rais wa Zanzibar. Katika hotuba nzima ya mapokezi sikumsikia akitaja jina la Magufuli, ila alizisifia sana na kusema bado nyingine 5 zinakuja jumla zifike 16.

Ninaamini, siku Marais hawa watakuwa hawapo,tutaongea mengi sana ambayo kwa sasa tunaogopa au kwa hulka yetu tunaona siyo wajibu wetu!

Na kwa bahati nzuri au mbaya kila Kiongozi anayeingia gia ya kwanza ni kuweka mfumo ambao utahakikisha hulka yetu ya kutokosoa jambo unaendelezwa. Siyo bungeni,siyo uraiani na kila pande.
Swali langu la msingi ni hii hulka ya kuona kila kiongozi analofanya ni sawa na wote kukaa kimya litaisha lini?

Inawezekana, baadhi ya viongozi wangependa kukosolewa au kupata mawazo mbadala ila hulka inagoma. Nakumbuka hata Mh. Rais wetu Mama Samia alipoingia madarakani alisema wazi kuwa angependa kila mtu ashiriki kutoa maoni ya kuijenga nchi yetu na siyo kutegemea mtu mmoja.

Swali langu la pili ni je,nini kifanyike kuondoa hulka hii tegemezi tofauti na nchi nyingine?

Mimi ni muumini wa mawazo huru yasiyovunja sheria za nchi.
 
Inasababishwa na Katiba mbovu tuliyonayo, tumekuwa watumwa wa kutegemea fadhila za Rais aliyeko madarakani, badala ya Rais afanye mambo kwa kufuata misingi iliyowekwa kisheria na ajue mipaka ya utekelezaji wa majukumu yake.
 
Its a sad truth kua jana ktk hotuba za viongozi hakuna amlie mu acknowledge alieanzisha jitihada za kulifufua hilo shirika or alieagiza hio mindege, wanataka tuamini kua wao ndio wametenda.

Bt angalau mabeberu waliacha ile slogani ya Hapa kazi tu kuonesha ilinunuliwa awamu iliyopita.
Wanasiasa wa kitanzania ni wanafiki sana na wana uhamishia unafiki wao kwa wanainchi, miezi 8 iliyopita kila hotuba walizokua wanazitoa walikua wanamtag JPM jana ht kumu acknowlegde tu walishindwa, hii inamaanisha ht mama akiondoka watamfanyia the same, she need to be careful na wapiga mapambio yake.
 
Ama umebaki peke yako au aina hiyo ya watu hapa petu Tanzania imeanza kuwa adimu hasa kwa vijana wetu. Wahusika wanadhani akisha tangazwa kiongozi basi ana akili, hekima na busara kuliko wote anawaongoza.

Pia vijana wetu vilaza wasomi wa Phd wengi wao wanafikiria hivyo! Nenda kwenye wizara zenye Waziri mwenye Phd umsikie mwenyewe anachosema na anachojua! Tuna safari kubwa ya kurudi nyuma. Sijajua itakoma lini. Hotuba zao kama insha ya darasa la nne.

Ni mpangilio wa maneno ya Kiswahili. Nani anatunza hotuba ya kiongozi kwa kufanya cutting kwenye gazeti siku hizi?

Bado tunarudi nyuma mpaka tutakaposhtuliwa wakati rumechokaa wakati wenzetu wanachemka na uhalisia pia mawazo mapya. Sikiliza Bungeni kama una muda kidogo wa kupoteza halafu niambie!!
 
Magufuli alikuwa mpenda sifa ndiyo maana wateule wake kama Palamagamba, Agrrey Mwanri na Kangi Lugora walimuona ni kama mungu wao. Kutwa walikuwa wanamsifu na kumuabudu.

Pili alikuwa hapendi kuambiwa amekosea, ukimkosoa anaweza kukupoteza kama alivyomuua Ben Saanane au kama alivyommiminia risasi 16 Tundu Lissu.

Ndiyo maana watu waliamua kumsifia tu, but it wasn't genuine
 
Watanzania ndivyo tulivyo.

Shida kubwa ni umasikini wa akili na mali, elimu ndogo na mambo kama hayo.
 
Lakini tuna Maprofessor wengi sana tena wa Kimataifa. Nenda SUA,UDOM,UDSM . Sikubaliani na wazi la ujinga, labda umasikini,hata hivyo bado ukiwa masikini leo siyo ticket ya milele
 
Sisi Watanzania tunayo sifa moja tofauti na wenzetu. Humsifia kila Rais anayekuwepo madarakani na kumpa majukumu ya kufikiria kila jambo kwa niaba yetu! Akiondoka madarakani tunaanza kulalama tena kichinichini kwa woga . Kuwa hili na lile hakutenda sawa.
Dr. Magufuli alinunua midege,tukamsifia sana,alipotwaliwa, hata Mh. Spika akamsema hadharani kuwa mradi wa ndege haukuwa na tija. Na ripoti kadhaa zikaonyesha namna ndege zinavyoiingizia nchi hasara.
Jana,tumeona ndege mbili zikishuka Zanzibar na kupokelewa na Rais wa Zanzibar. Katika hotuba nzima ya mapokezi sikumsikia akitaja jina la Magufuli,ila alizisifia sana na kusema bado nyingine 5 zinakuja jumla zifike 16 .
Ninaamini,siku Marais hawa watakuwa hawapo,tutaongea mengi sana ambayo kwa sasa tunaogopa au kwa hulka yetu tunaona siyo wajibu wetu!
Na kwa bahati nzuri au mbaya kila Kiongozi anayeingia gia ya kwanza ni kuweka mfumo ambao utahakikisha hulka yetu ya kutokosoa jambo unaendelezwa. Siyo bungeni,siyo uraiani na kila pande.
Swali langu la msingi ni hii hulka ya kuona kila kiongozi analofanya ni sawa na wote kukaa kimya litaisha lini?
Inawezekana,baadhi ya viongozi wangependa kukosolewa au kupata mawazo mbadala ila hulka inagoma. Nakumbuka hata Mh. Rais wetu Mama Samia alipoingia madarakani alisema wazi kuwa angependa kila mtu ashiriki kutoa maoni ya kuijenga nchi yetu na siyo kutegemea mtu mmoja.
Swali langu la pili ni je,nini kifanyike kuondoa hulka hii tegemezi tofauti na nchi nyingine?
Mimi ni muumini wa mawazo huru yasiyovunja sheria za nchi.
Wenye tabia ya kusifia ni wa kutoka Singida, Nzega Tabora, Western Province yote, Pwani, Mikoa ya kusini na ni watu ambao hawana mawazo yao wenyewe. Utawala ni taasisi si mawazo ya mtu mmoja
 
Sisi Watanzania tunayo sifa moja tofauti na wenzetu. Humsifia kila Rais anayekuwepo madarakani na kumpa majukumu ya kufikiria kila jambo kwa niaba yetu! Akiondoka madarakani tunaanza kulalama tena kichinichini kwa woga . Kuwa hili na lile hakutenda sawa.
Dr. Magufuli alinunua midege,tukamsifia sana,alipotwaliwa, hata Mh. Spika akamsema hadharani kuwa mradi wa ndege haukuwa na tija. Na ripoti kadhaa zikaonyesha namna ndege zinavyoiingizia nchi hasara.
Jana,tumeona ndege mbili zikishuka Zanzibar na kupokelewa na Rais wa Zanzibar. Katika hotuba nzima ya mapokezi sikumsikia akitaja jina la Magufuli,ila alizisifia sana na kusema bado nyingine 5 zinakuja jumla zifike 16 .
Ninaamini,siku Marais hawa watakuwa hawapo,tutaongea mengi sana ambayo kwa sasa tunaogopa au kwa hulka yetu tunaona siyo wajibu wetu!
Na kwa bahati nzuri au mbaya kila Kiongozi anayeingia gia ya kwanza ni kuweka mfumo ambao utahakikisha hulka yetu ya kutokosoa jambo unaendelezwa. Siyo bungeni,siyo uraiani na kila pande.
Swali langu la msingi ni hii hulka ya kuona kila kiongozi analofanya ni sawa na wote kukaa kimya litaisha lini?
Inawezekana,baadhi ya viongozi wangependa kukosolewa au kupata mawazo mbadala ila hulka inagoma. Nakumbuka hata Mh. Rais wetu Mama Samia alipoingia madarakani alisema wazi kuwa angependa kila mtu ashiriki kutoa maoni ya kuijenga nchi yetu na siyo kutegemea mtu mmoja.
Swali langu la pili ni je,nini kifanyike kuondoa hulka hii tegemezi tofauti na nchi nyingine?
Mimi ni muumini wa mawazo huru yasiyovunja sheria za nchi.
Msingi wa umasikini umejengeka hapa.
Umasikini wa fikra ni mbaya zaidi ya ule wa mali.
 
Taifa limejaa full of wanafiki, wachumia stomach, praise and worship mwanadam team, sifia sifia bila kutumia akil na utashi wao.
 
Watanzani wangapi? Wote? Wengi? Wachache?

Back
Top Bottom