Nyanda Banka
JF-Expert Member
- Mar 14, 2023
- 304
- 1,054
Mfumo wa elimu wa wengi umewafunza kuomba nafasi mezani ilihali maisha yanataka mtu achukue(ak-claim) nafasi yake mezani kibabe.
Ukiomba unaweza kupewa ama kunyimwa, ukichukuwa nafasi yako mezani kibabe kila mtu atabaki akijiuliza, huyu ni nani? Nani yuko nyuma yake? Ametoa wapi ujasiri?
Hatahivyo, simaanishi matumizi ya maguvu bali matumizi ya maarifa, nidhamu, mahusiano bora na ujasiri. Unafanya mambo sahihi kwa wakati sahihi hadi pale ambapo meza haiwezi kamilika bila wewe kualikwa.
Kinachowafanya wengi kukata tamaa na kuishia kulalamika ni tabia yao ya kutegemea rehema; mezani hakuna rehema kuna kuchukua nafasi yako kwa bidii. Jipange, tambua ni sifa gani na vigezo gani unapaswa kuwa navyo ili uchukuwe nafasi yako mezani kibabe.
Anza kujifanyia matengenezo kujenga sifa na uwezo wa kukupa nafasi yako mezani. Kama ni shule, ongeza elimu; kama ni kujiamini ongeza kujiamini; kama ni maarifa, ongeza maarifa ukianza kuchangia mada unatoa mchango wa maana; kama ni heshima na nidhamu, jenga kujiheshimu na nidhamu.
Itafika mahali hawawezi kuanza kula bila kukuita, itafika mahali hawatafanya maamuzi bila kukushirikisha, itafika mahali wanakuongeza mshahara kabla ya wewe kuomba nyongeza, itafika mahali wanakupangia majukumu makubwa zaidi na na itafika mahali nafasi yako inakuwa bayana mezani.
Njia ya kuchukua nafasi mezani kibabe, ndiyo njia ambayo iko mkononi mwako na unaweza kuidhibiti. Itumie kujenga maisha yako katika kila eneo la maisha yako.
Katika biashara unapokuwa mbunifu, mvumbuzi, unatoa huduma nzuri, unakuwa na maarifa, mikakati na mbinu bora ndipo unapochukua nafasi yako mezani. Unapokuwa na nidhamu nzuri ya kutunza na kuzungusha pesa ndivyo unavyochukua nafasi yako mezani.
Nafasi ya mtu mezani huchukuliwa kwa yeye kuwa mtu bora zaidi, matumizi ya maarifa, mahusiano bora, mikakati na mbinu. Hakika anayesubiri kupewa rehema mezani hawezi kumzidi anayeichukua nafasi yake kibabe.
* Claim your sit on the table/ Chukua nafasi yako mezani
Kitabu Kipya: #BadilishoLaMtazamo
"Maisha huwatuza wenye maamuzi na hamu kali kuliko wale ambao hutegemea tumaini pekee."
Asante kwa kusoma na kushea 🙏🏿🙏🏿🙏🏿