ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
Nafungua ubongo natoa fikra za utumwa kichwani/ kipawa cha toka Kwa mola na wala sija tumia ubani/ sister p kupata chart watu wanadhani langu utani/ Rap biashara bwana ila angalia usipate Hasara/ kuuza vitumbua ,pipi & maandazi zote biashara/ usi dharau hizo biashara watu wataku Angushia msala/ wasomi wengi wamesoma kwa kutumia hizo biashara/ mashairi sibahatishi na nitauza nyingi nakala/ na sio utani nyota kwangu imeonakana biashara/ wandago ni rafiki zangu tena wa kina wewe uliza maswali mengi majibu mi sina/ nakupa Rap shule mashairi yangu yana vina....
Hii verse inapatikana katika wimbo wa sister p akiwa na msanii wa muziki aina ya dansi Ally choki a.k.a mzee wa farasi lamoja na Rap mad brain.
Ni sehemu pia ya maishairi yalikuwa ni kama majibu kutoka kwa Raper sister p kwa msanii Mwana fa kwa kile kilichoonekana kwenye jamii kupitia ngoma yake inaitwa " ingekuwa vipi" akiwa na jay moe project iliyofanyika " mawingu studio" kwa producer Bonnie luv
Kama diss track kwa baadhi ya wasanii hasa wasanii kutoka mtaa wa Temeke. Ambao walifahamika zaidi kama " koo la walume ndago "
Walume ndago ilikuwa ni muunganiko wa makundi mbalimbali muziki Enzi hizo pamoja na wasanii ambao walifanya muziki kama solo Artist nje makundi..
Baadhi ya makundi yaliounda koo hii ya walume ndago ni pamoja na
• Wachuja nafaka
▪︎ gangwe mobb
• wandago family
Lakini kubwa zaidi ni pamoja na msanii sister p nae alikuwa ni sehemu ya wasanii waliounda koo hii ingawa alikuwa akai temeke enzi hizo..
Tafsiri halisi ya neno walume ndago ni Aina fulani ya majani ambayo yanavumilia sana shabani nakuwa kikwazo kwa mkulima katika uzalishaji wa mazao kwa mkulima huyo shabani , kwa kifupi ni mavumilivu hayafi ovyo ama kiurahisi. Yalikuwa yanaitwa ama yalifahamika kwa jina la " ndago"
Kwahiyo chanzo cha neno " walume ndago ndio hiyo.
Wasanii wengi wa Temeke walipenda kutumia jina hilo kwa sababu ya ugumu wa maisha ama mazingira wanaoishi temeke lakini hakikuwa kikwazo kwao cha kuwafanya washindwe kuendelea kuishi temeke , kama ilivyo kuwa ngumu kwa majani aina ndago kufa shabani.
Mwana fa na jay moe katika ngoma ya ingekuwa vip wanasikika wakisema.
Mwanafalsafa: Ingekuwa vipi, maisha ya Temeke yangekuwa juu kidogo?
Unadhani wasanii wangejiita walume ndago?
Jay moe : Ingekuwa vipi Bongo Records isingekuwa ya Halfani?
Watu kama flani-flani tusingewasikia hewani!
Tasfri yake je? Maisha ya temeke yangekuwa ya kishua wao kama wasanii wangejiita " walu ndago"
Ndio sister p nae akamjibu fa kwa kusema. ( achana nao)
wandago ni rafiki zangu tena wa kina wewe uliza maswali mengi majibu mi sina/ nakupa Rap shule mashairi yangu yana vina....
Itaendelea....
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202