GE2025 Sita wachaguliwa kugombea nafasi ya Spika wa Bunge

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Taarifa kwa umma kuhusu kukamilika kwa zoezi la uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Spika

1.0
Zoezi la Uteuzi wa Wagombea wa Uchaguzi wa Spika limekamilika tarehe 10 Novemba, 2025 saa 10:00 Alasiri. Napenda kuchukua nafasi hii kuwafahamisha yale yaliyotokana na zoezi hili na mchakato mzima toka tulipoanza, tulipo na tunapoelekea.

2.0 Uchaguzi wa Spika unafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 86 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Kanuni ya 9 na Nyongeza ya Kwanza ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2025.

3.0 Ili kukidhi matakwa hayo, tarehe 4 Novemba, 2025 nilitoa Tangazo namba 14824A katika Gazeti la Serikali Toleo Maalum Namba 11 kuvijulisha vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu vinavyokusudia kusimamisha mgombea katika uchaguzi huo kufanya mchakato na kuwasilisha jina la mgombea husika ofisini kwa Katibu wa Bunge Dodoma kabla ya saa 10.00 jioni ya tarehe 10 Novemba, 2025 ambayo ndiyo siku ya uteuzi.

4.0 Hadi kufikia saa 10:00 Alasiri leo tarehe 10 Novemba, 2025 Wagombea waliowasilishwa na Vyama vyao ni kama ifuatavyo:–

(a) Mussa Azzan Zungu kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM);

(b) Ndg. Veronica Charles Tyeah kutoka Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA);

(c) Ndg. Anitha Alfan Mgaya kutoka Chama cha National League for Democracy (NLD);

(d) Ndg. Chrisant Nyakitita kutoka Chama cha Democratic Party (DP);

(e) Ndg. Ndonge Said Ndonge kutoka Chama cha Alliance for Africa Farms Party (AAFP); na

(f) Ndg. Amin Alfred Yango kutoka Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).

photo_2025-11-10_19-56-22.jpg

photo_2025-11-10_19-56-25.jpg
 
Taarifa kwa umma kuhusu kukamilika kwa zoezi la uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Spika

1.0
Zoezi la Uteuzi wa Wagombea wa Uchaguzi wa Spika limekamilika tarehe 10 Novemba, 2025 saa 10:00 Alasiri. Napenda kuchukua nafasi hii kuwafahamisha yale yaliyotokana na zoezi hili na mchakato mzima toka tulipoanza, tulipo na tunapoelekea.

2.0 Uchaguzi wa Spika unafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 86 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Kanuni ya 9 na Nyongeza ya Kwanza ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2025.

3.0 Ili kukidhi matakwa hayo, tarehe 4 Novemba, 2025 nilitoa Tangazo namba 14824A katika Gazeti la Serikali Toleo Maalum Namba 11 kuvijulisha vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu vinavyokusudia kusimamisha mgombea katika uchaguzi huo kufanya mchakato na kuwasilisha jina la mgombea husika ofisini kwa Katibu wa Bunge Dodoma kabla ya saa 10.00 jioni ya tarehe 10 Novemba, 2025 ambayo ndiyo siku ya uteuzi.

4.0 Hadi kufikia saa 10:00 Alasiri leo tarehe 10 Novemba, 2025 Wagombea waliowasilishwa na Vyama vyao ni kama ifuatavyo:–

Mussa Azzan Zungu kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM);
(b) Ndg. Veronica Charles Tyeah kutoka Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA);

(c) Ndg. Anitha Alfan Mgaya kutoka Chama cha National League for Democracy (NLD);

(d) Ndg. Chrisant Nyakitita kutoka Chama cha Democratic Party (DP);

(e) Ndg. Ndonge Said Ndonge kutoka Chama cha Alliance for Africa Farms Party (AAFP); na

(f) Ndg. Amin Alfred Yango kutoka Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).

View attachment 3499953
View attachment 3499952
Hivyo vyama vingine huwa vinaibuka kipindi cha uchaguzi tu?
 
Hapo ni zungu tu ndio spika, hao wengine ni wasindikizaji tu. Mtu huna hata mbunge mmoja halafu unagombea uspika, hivi si ni vituko?
 
Kila kitu kinachofanyika kufuatia ule ushenzi wa tarehe 29, ni uwendawazimu. Hatuna muda hata wa kujadili huo uharamia. Hao ni sawa na majambazi yanapokutana kumchagua kiongozi wao, watu wema hawatakiwi kujihusisha na chochote zaidi ya kufikiria namna ya kuyaondoa hayo majambazi katika mazingira yao.
 
Back
Top Bottom