Taarifa kwa umma kuhusu kukamilika kwa zoezi la uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Spika
1.0 Zoezi la Uteuzi wa Wagombea wa Uchaguzi wa Spika limekamilika tarehe 10 Novemba, 2025 saa 10:00 Alasiri. Napenda kuchukua nafasi hii kuwafahamisha yale yaliyotokana na zoezi hili na mchakato mzima toka tulipoanza, tulipo na tunapoelekea.
2.0 Uchaguzi wa Spika unafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 86 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Kanuni ya 9 na Nyongeza ya Kwanza ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2025.
3.0 Ili kukidhi matakwa hayo, tarehe 4 Novemba, 2025 nilitoa Tangazo namba 14824A katika Gazeti la Serikali Toleo Maalum Namba 11 kuvijulisha vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu vinavyokusudia kusimamisha mgombea katika uchaguzi huo kufanya mchakato na kuwasilisha jina la mgombea husika ofisini kwa Katibu wa Bunge Dodoma kabla ya saa 10.00 jioni ya tarehe 10 Novemba, 2025 ambayo ndiyo siku ya uteuzi.
4.0 Hadi kufikia saa 10:00 Alasiri leo tarehe 10 Novemba, 2025 Wagombea waliowasilishwa na Vyama vyao ni kama ifuatavyo:–
Mussa Azzan Zungu kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM);
(b)
Ndg. Veronica Charles Tyeah kutoka Chama cha
National Reconstruction Alliance (NRA);
(c)
Ndg. Anitha Alfan Mgaya kutoka Chama cha
National League for Democracy (NLD);
(d)
Ndg. Chrisant Nyakitita kutoka Chama cha
Democratic Party (DP);
(e)
Ndg. Ndonge Said Ndonge kutoka Chama cha
Alliance for Africa Farms Party (AAFP); na
(f)
Ndg. Amin Alfred Yango kutoka Chama cha
Alliance for Democratic Change (ADC).
View attachment 3499953
View attachment 3499952