Sitafuti hela ya kula,natafuta maisha

maharage ya ukweni

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
1,415
Reaction score
3,213
Asalaam aleykum!
Wanabodi kama kichwa cha habari kilivyo hapo juu,mimi nina kazi lakini siku zote mshahara hautoshi kwahiyo nimeamua kujiingiza kwenye ujasiriamali.Kwa mtu yeyote ambaye ana friji au friza na yuko tayari kufanya biashara ya maziwa fresh ya ngo'mbe mimi niko tayari kumkabidhi mzigo wa maziwa hata lita elfu moja na tutagawana asilimia katika faida.
Kwayeyote ambaye anaishi dar na yuko tayari kufanya biashara na mimi basi ani PM,ambaye hana friji wala friza lakini anahitaji kufanya hii biashara nitamuwezesha kupata friji au friza.Tutaandikishiana kimkataba ili kuepusha shari.Kwa wale ambao hawana mtaji na wanataka kufanya biashara kama vile ndizi jumla na reja reja,viazi vya chipsi jumla na reja reja,karoti jumla na reja reja,maparachichi jumla na reja reja na wana sehemu nzuri ya kufanyia biashara nao pia nitawakabidhi mzigo then tutagawana asilimia katika faida.

NB;SITAFUTI HELA YA KULA, NATAFUTA MAISHA
 
Mkuu ningependa unipe maelezo kidogo ya haya maswala, wewe kwanza upo Dar sehemu gani,hayo maziwa ni ya Ng'ombe halisi au ni yale ya viazi na pia lita moja unauza tshs ngapi, pia utoe bei ikiwemo na ujazo wake za hizo ndizi,viazi,karoti na maparachichi.
 
Maziwa ni halisi ya ngo'mbe na lita ni 1800,ndizi ni kwa mkungu,viazi ni kwa gunia,karoti kwa ndoo ndogo ya lita kumi na maparachichi ni kwa ndoo ndogo ya lita kumi na bei hua inabadilika kulingana na msimu
 

Mkuu viazi unauzaje kwa gunia ?
 
Natafuta pesa ya kuwatengenezea future familia yangu na jamii kwa ujumla.
 
Lina ukubwa gani mkuu?na bei hii ni kwa hapa dar au mkoani?
Ujazo wa sasa hivi ni ndoo sita kubwa hakuna ushungi yani ukikutwa njiani na gunia lenye rumbesa kesi yake kama umeua.bei hiyo ni kwa hapa Dar
NB;mimi ni mkulima sio dalali wala mlanguzi
 
Hongera sana ndugu. Tunahitaji watu wenye hekima kama yako. Naamini wahusika wataona hii opportunity vyema.
 
Mm nna frezer kubwa sana ila sina office ningefanya[emoji24]
Kwahiyo hata sehemu ya kuishi huna?mbona hata hapo unapoishi unaweza kuuza!
kama uko tayari ni PM
NB:mimi ni kijana lakini mambo ya ajabu sipendi,kama kweli unastafuta maisha na sio kujaribu kutafuta maisha tuwasiliane
 
Mkuu upo nilikuwa nahitaji ntu kama wewe,ila naomba uzungumzie kuhusu usafiri.
Je mzigo utauleta mpaka mlangoni mie nipo Mombasa ya Dar,nahitaji Parachichi kwanza halafu baadae maziwa.
Shukran
 
Unapata wapi mazao? Ukihitaji Carrot na yale maharage machanga embu nishtue nkaongee na wadau nikupe mzigo.
 
Unapata wapi mazao? Ukihitaji Carrot na yale maharage machanga embu nishtue nkaongee na wadau nikupe mzigo.
Sikia kama unahitaji ni PM tufanye biashara maana mzigo upo tena ukifika msimu wa mapeasi nistue maana tuna mipeasi ya kutosha kuulisha mtaa wako wote kwa mda wa miezi mitatu mfululizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…