Sitaki kutukanwa, nataka nishauriwe

kuoa wake wengi ni roho mbaya za baadhi ya wanaume sbb wanakua wanapuuzia kuwa mke wa kwanza anakua ktk maumivu makali ya moyo kuona kipenzi chake kikiwa si chake peke yake.

Vipi kama mke wa kwanza ameridhia?
 
Vipi kama mke wa kwanza ameridhia?

hakuna mwanamke anayependa,wanaridhia baada ya kuona hamna jinsi,kwa mwanaume hamna u turn ndio afanyeje in short wanakubali shingo upande....mtu uliyempenda huwezi kumruhusu awe na mtu mwingine period.
 
Vipi kama mke wa kwanza ameridhia?

NN mfano dini ingekua inaruhusu na wanawake tuolewe na wanaume wengi.
Mkeo anakujia,"mume wangu Ngabu unajua kiasi gani nakupenda,mpenzi wangu naomba unipe ridhaa yako niongeze mume mwingine,muwe wawili,hana shida ni mtulivu cha msingi umheshimu tu na kumpenda,utapata rafiki wa kushangilia naye mechi za MAN U pia atakusaidia mambo mengi si unajua tena we umeshaanza kuwa mtu mzima na yeye bado ni kijana."
Kama kweli utaridhia kwa moyo wako bila kushurutishwa basi ujue kuna wake wa kwanza wanaoridhia ila kama moyo wako utakataa basi ujue hakuna mwanamke anayeridhia hii kitu.
 

Mimi nakataa sweeping generalizations. On a case by case basis, wapo watu ambao huwa wanaridhia. Katika hali kama hiyo, sioni ubaya wowote wa mtu kuongeza mume ama mke.
 
hakuna mwanamke anayependa,wanaridhia baada ya kuona hamna jinsi,kwa mwanaume hamna u turn ndio afanyeje in short wanakubali shingo upande....mtu uliyempenda huwezi kumruhusu awe na mtu mwingine period.

Are you every woman?
 
Mimi nakataa sweeping generalizations. On a case by case basis, wapo watu ambao huwa wanaridhia. Katika hali kama hiyo, sioni ubaya wowote wa mtu kuongeza mume ama mke.

NN mim nilikuomba wewe ujibu kama wewe.UNGEMKUBALIA?
 
Binafsi nisingemkubalia. Lakini pia, mimi sio every man and neither am I a spokesman for ever man out there.

Ngabu nilijua huwezi kukubali,hata ungesema ungekubali bado ningejua unadanganya,sbb najua haiwezekani.
Nakuomba utuambie kwanini wewe moyo wako umeona kwamba usingemkubalia.
 
Ukioa nakushauri wasikae mbali,manake kuna Mdingi namfahamu anao watatu,mmoja anakaa Tanga,mwingineKibaha,mwingine Dar.
Kwa hiyo inabidi karibu kila wiki adrive kutoka Tanga kuja either Dar au Kibaha,ili kuhakikisha anawapa haki yao sa si shughuli hiyo?
 
Ngabu nilijua huwezi kukubali,hata ungesema ungekubali bado ningejua unadanganya,sbb najua haiwezekani.

Hii ya kusema haiwezekani ndiyo sikubaliabi kabisa na wewe. Kama wewe na mimi hatuwezi hiyo haina maana wengine hawawezi.

Nikupe mfano, mimi siwezi hata kufikiria kutoka na mwanamke ambaye ni mcheza filamu za ngono. Lakini huko Hollywood kuna wacheza filamu za ngono ambao wameoa na kuolewa na watu ambao hawachezi hizo filamu na hao wenza ambao hawachezi hizo filamu wanazichukulia hizo kazi za wenza wao kama ajira tu zingine.

Sasa haya mambo ya kujumlisha binadamu wote katika kundi moja mimi siafikiani nalo. Nikuulize, wewe unaweza hata kutoka na Mandingo (yule mcheza filamu za ngono)?

Nakuomba utuambie kwanini wewe moyo wako umeona kwamba usingemkubalia.

Kwa sababu siamini katika kuchangia mapenzi na mtu mwingine ambaye ni zaidi ya mpenzi/ mwenza wangu. Hiyo ni imani yangu.
 
Mimi nakataa sweeping generalizations. On a case by case basis, wapo watu ambao huwa wanaridhia. Katika hali kama hiyo, sioni ubaya wowote wa mtu kuongeza mume ama mke.

ukiona anaridhia kirahisi ujue hakupendi anasema bora liende
 
Kwani mmoja hakutoshi???? Au keshachuja kwani miaka 20 mingi ati!
 

Siwezi kutoka na mandingo hata kama akinambia aliaacha hiyo kazi miaka kumi ilopita.

NN mim pia sipendi generalisation,lkn ukiwa kama binadamu unaweza kujua kitu ambacho ni kigumu binadamu mwingine kufanya,au ukiwa kama mwanamke unaweza kujua ni nini mwanamke mwenzio anaweza kufanya au kutofanya sbb na wewe unafanana nao,japo kila mmoja ana tabia zisizofanana na mwenzie.

Mfano binadamu yeyote wa kawaida anajua kuua binadamu mwingine ni kitu kigumu sana,hata kama sisi sio every human being lkn tunajua kuua binadamu mwingine ni kitu kigumu sana na wengi hatuwezi lkn wapo wachache wetu wanaweza kufanya,na wanapofanya tunawashangaa kuwa wana mioyo ya aina gani mpaka wameweza kufanya hivyo.

hivyo sihitaji kuwa every woman kujua kuwa haiwezekani kwa mwanamke aridhie mpenzi wake ampende mwanamke mwingine.


btw uncle wako anasema hi.
 
kipipi vipi kama utabembelezwa utoe ridhaa yako.Halafu jamaa anakuhakikishia kuwa atakupendeni sawa sawa.

Kwangu mimi kuniongezea mke mwingine au kufanywa mke wa pili ni tusi wala sio mapenzi (samahani kwa wale mtakaokerwa/kukwazwa na maneno yangu)! Siamini katika kupendwa sawa kwa sawa hasa kwa pendo kama hili linalohitaji attention, care na hisia za dhati toka moyoni. Na pia sipendi kupangishwa foleni kwenye penzi langu.....so nikitoa ruhusa basi itakuwa kwa mimi kuachia ngazi coz najua siwezi kuridhia kabisa!!
 
Siwezi kutoka na mandingo hata kama akinambia aliaacha hiyo kazi miaka kumi ilopita.

Heheheee nilijua tu huwezi.


Kwamba kuna baadhi ya mambo ambayo watu wengi huwawia vigumu, hiyo ni kweli. Kwa hiyo nimekuelewa.


btw uncle wako anasema hi.

I say hi too. Nataka nimnunulie personalized sipper cup ya Disney ila nataka kujua favorite Disney character wake...
 

hata mim mtu kunijia eti ananiomba aongeze mwenzangu nitaona kanitukana na nitamkubalia kisha natimua zangu nimuache na ampendae.

Wanawake wanaokubali kuna sababu nyingi zinazofanya wakubali ikiwa ni uoga wa kwenda kupata shida,hawa ni wale wanawake wavivu wasiojiamini wanaoishi hapa duniani kwa support ya mwanaume,bila mwanaume kanga nzuri hawezi kuvaa au bila mwanaume watoto wake watapata shida eti anabaki kwa faida ya watoto wake,au wengine ushirikina unafanya abaki huku akihangaika kwa waganga akidhani iko siku penzi lililohamishiwa kwa bi mdogo litarudi kwake.
Kubaki ktk ndoa ya hivi ni kutojua thamani yako,hata kama sizai siwezi kukuruhusu uoe mke mwingine eti ili upate watoto,je ingekua ni yeye mwanaume ndo hana uzazi angeniruhusu nikazae nje ili aitwe baba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…