Mkuu sawa lakini kumbuka ni ruhusa na si wajibu....na itakuwa vema ukaoa mjane nadhani hii ruhusa ilitolewa kutakuwa na resson behind na sio kimatamanio zaidi tafuta mjane mstiri ana mkeo atafurahi.... wenye dini watanisahihisha hapa...!
good luck
Mapambano ni sehemu ya raha! Mimi ni mpambanaji na nahisi nimpe afuweni mwenzangu!huyo mmoja una mridhisha? isije kuwa unajiongezea matatizo....
Inshalla nitajijuwa zaidi kuwa ninao uadilifu hapo nitakapoowa wa pili. Unajuwa uhakika unakuja uwanjani wakati wa mechi sio mazoezi.Awali ya yote Mabrouk! Ila nakusia nafsi yako na yangu pia katika kuwa muadilifu kaka! Allah akutangulie katika hilo, akupe mke mwenye imaan, awaja'alie wote afya njema, rizk ya halal na watoto wema InshaALLAH!
Hiyo hela kwa nini usiwasaidie watoto yatima.Manake ndo nyie mkifa mnaacha watoto wengi mtaani wakipata shida.
ongeza mwaya, hata 3 na kuendelea ongeza!
nipo tayari
Nadhani hujanipata vizuri, mapenzi kwangu ni nafsi wala si maslahi!! So siwezi kuteketeza wala kunung'unisha nafsi yangu kisa maslahi hasa kwa kugawana penzi la mume!! Vile vile mapenzi/ndoa sio kazi hata niletewe assistant, kumbuka mimi kuolewa haimaanishi kwamba ni koloni la mtu na wala similikiwi to the extent niendelee kuchekelea tu bwana akiteka na kuendelea kuongeza makoloni mengine na mie nibaki kurundikwa tu...........so kunijia na kuniambia habari za kuongeza mke ni sawa na kunitusi!!! Hivi ni nini hasa kinachokufanya uongeze mke wa pili, tatu......kama sio tamaa zako tu na kiburi cha uzima??
Inaruhusiwa kaka ila tu kama unaweza kuwatimizia kila kiru EQUALLY. vinginevyo utajichumia dhambi tu.
Kwa huo umri wa zaidi ya miaka 40 unatakiwa ufanye vizuri tathimini ya kipato chako kama kinaweza kuwahudumia wake wawili na kusomesha watoto watakaozaliwa na mke mdogo kwa zaidi ya miaka 20 ijayo ambapo wewe utakuwa una umri zaidi ya miaka 60 na uwezo wako wa kufanya kazi utakuwa umepungua wakati wanao bado wanakutegemea. Kama uwezo wako kifedha ni mzuri na unaona bado unaweza kumudu majukumu ya ndoa kwa wake wawili na mkeo mkubwa ameridhia unaweza kuoa.
Kuboresha dhamira yangu kwa mfano!Ushauri wa nini wakati inaonekana umedhamiria tayari
Mwenye kujaribu hajuti kukataliwa.Tafadhali baba, mimi sio waya hata unitafutie pacha wangu na kutuconnect kwenye receiver moja kwa manufaa yako binafsi!!! Na kama wasiwasi unatolewa kwa namna hiyo, basi ni heri nijikung'unte mwenyewe udondoke!
sababu za kutaka mke wa pili ni kwa sababu za tamaa za mwili au mengineyo,,kama mmoja hajaweza kukutosheleza wa pili unadhani anaweza?
Swahiba wangu,kinachofanya niseme unataka kuoa kwa kuongozwa na tamaa zako za kimwili na sio kwa kufuata lengo halisi lililoelekezwa na mwenyezi Mungu ni maneno yako mwenyewe hayo ya rangi ya blue.Wewe unatumia vibaya hii ruhusa kugeuza ufuska na kuuita ndoa.Au maneno yako hapo ndivyo Quran takatifu inavyoagiza hivyo kuwa muoe wake wengi sbb dunia ni kubwa na wazuri ni wengi?
Ofa yako ya kutaka kunifanya mke wa pili iwapo bado sijaolewa naikataa kwa jina la Yesu.Kamwe siwezi kuwa mke wa pili,sbb naamini mim ni malkia mwenye hadhi ya kuwa na himaya yangu peke yangu.Bora niwe bachelor maisha yangu yote kuliko kushiriki mume na mwanamke mwenzangu.
mkuu wangu hata hivyo naona kama nimekutupia shutma nyingi nikasahau kuwa wewe sio mwenye makosa,wenye makosa ni hao wanawake wanaokubali kuolewa uke wenza.Wangekua wanakataa sidhani kama mngepata nafasi ya kuona kuwa wanawake ni kama mashati,ukiona ya kwanza yamepauka hayana mvuto tena unakwenda dukani kutafuta zuri linalovutia.
Nakutakia kila la kheri mkuu wangu ktk ndoa yako ya pili,usinisahau ktk pilau.
umepima afya? huna kisukari usije ukatusumbua kwa kutafuta dawa za kuongeza nguvu kwa kawaida mke wapili huwa ananguvu kwa mwanzo.
ila maisha magumu ebu vumilia
Nafsi mchumba wangu ndio inayoleta yote hayo! Nafsi yako inapokuwa haijazidiwa ni rahisi kuona waziwazi lakini nafsi hiyo hiyo ikipenda inaweza ikawa haioni sawsawa na watu wanaweza wakashangaa yale unayoyavumilia.
Sasa mwenzangu iwapo nafsi yangu imeshataka niongeze mke, mke wangu wa kwanza amekubali kuiridhisha nafsi yangu na kuna muhusika wa tatu ambaye kama mke wangu wa kwanza ameshakubali hiyo unayoiita kugawa mapenzi kuna ubaya gani?
Unaweza ukanipa sababu za msingi katika hayo maamuzi yako?? Nafsi yako inakutumaje kwa huyo mke wa pili utakaemuoa?
umechemka mkuu kuongeza mke nisehemu ya tatiyo unalojijiongezea ushauri wangu kuliko uogenye nibora umuache kwanza huyo japo pia sikushauri umuache tafuta chanzo isije kua wewe nichanzo huyoMapambano ni sehemu ya raha! Mimi ni mpambanaji na nahisi nimpe afuweni mwenzangu!
Mimi ndio nataka kuowa sio pesa yenye kutaka kuowa! Kama fedha ndio kuowa basi Kina Reginald Mengi wangeowa wengi tu. Suala la kuowa ni uamuzio sio pesa!