Sitaki kutukanwa, nataka nishauriwe

Sitaki kutukanwa, nataka nishauriwe

Mkuu sawa lakini kumbuka ni ruhusa na si wajibu....na itakuwa vema ukaoa mjane nadhani hii ruhusa ilitolewa kutakuwa na resson behind na sio kimatamanio zaidi tafuta mjane mstiri ana mkeo atafurahi.... wenye dini watanisahihisha hapa...!

good luck

Tumepewa sifa kama nne za kuamua kumuowa mwanamke na ile ya uzuri imetangulizwa! Uzuri unaleta hamu au siyo?
 
Awali ya yote Mabrouk! Ila nakusia nafsi yako na yangu pia katika kuwa muadilifu kaka! Allah akutangulie katika hilo, akupe mke mwenye imaan, awaja'alie wote afya njema, rizk ya halal na watoto wema InshaALLAH!
Inshalla nitajijuwa zaidi kuwa ninao uadilifu hapo nitakapoowa wa pili. Unajuwa uhakika unakuja uwanjani wakati wa mechi sio mazoezi.
 
Hiyo hela kwa nini usiwasaidie watoto yatima.Manake ndo nyie mkifa mnaacha watoto wengi mtaani wakipata shida.

Mimi ndio nataka kuowa sio pesa yenye kutaka kuowa! Kama fedha ndio kuowa basi Kina Reginald Mengi wangeowa wengi tu. Suala la kuowa ni uamuzio sio pesa!
 
Nadhani hujanipata vizuri, mapenzi kwangu ni nafsi wala si maslahi!! So siwezi kuteketeza wala kunung'unisha nafsi yangu kisa maslahi hasa kwa kugawana penzi la mume!! Vile vile mapenzi/ndoa sio kazi hata niletewe assistant, kumbuka mimi kuolewa haimaanishi kwamba ni koloni la mtu na wala similikiwi to the extent niendelee kuchekelea tu bwana akiteka na kuendelea kuongeza makoloni mengine na mie nibaki kurundikwa tu...........so kunijia na kuniambia habari za kuongeza mke ni sawa na kunitusi!!! Hivi ni nini hasa kinachokufanya uongeze mke wa pili, tatu......kama sio tamaa zako tu na kiburi cha uzima??

Nafsi mchumba wangu ndio inayoleta yote hayo! Nafsi yako inapokuwa haijazidiwa ni rahisi kuona waziwazi lakini nafsi hiyo hiyo ikipenda inaweza ikawa haioni sawsawa na watu wanaweza wakashangaa yale unayoyavumilia.
Sasa mwenzangu iwapo nafsi yangu imeshataka niongeze mke, mke wangu wa kwanza amekubali kuiridhisha nafsi yangu na kuna muhusika wa tatu ambaye kama mke wangu wa kwanza ameshakubali hiyo unayoiita kugawa mapenzi kuna ubaya gani?
 
Kwa huo umri wa zaidi ya miaka 40 unatakiwa ufanye vizuri tathimini ya kipato chako kama kinaweza kuwahudumia wake wawili na kusomesha watoto watakaozaliwa na mke mdogo kwa zaidi ya miaka 20 ijayo ambapo wewe utakuwa una umri zaidi ya miaka 60 na uwezo wako wa kufanya kazi utakuwa umepungua wakati wanao bado wanakutegemea. Kama uwezo wako kifedha ni mzuri na unaona bado unaweza kumudu majukumu ya ndoa kwa wake wawili na mkeo mkubwa ameridhia unaweza kuoa.

Sawa mdogo wangu kwani kila kitu ni mipango dunia ya sasa, lakini pia tukumbuke yuko mpangaji zaidi mwenye mipango ya jumla!
 
Tafadhali baba, mimi sio waya hata unitafutie pacha wangu na kutuconnect kwenye receiver moja kwa manufaa yako binafsi!!! Na kama wasiwasi unatolewa kwa namna hiyo, basi ni heri nijikung'unte mwenyewe udondoke!
Mwenye kujaribu hajuti kukataliwa.
 
sababu za kutaka mke wa pili ni kwa sababu za tamaa za mwili au mengineyo,,kama mmoja hajaweza kukutosheleza wa pili unadhani anaweza?

Kwani kama nina tamaa za mwili kwanini niowe si nitafute usiku mmoja na mchana mwengine? Hilo linawezekana vizuri!
 
Swahiba wangu,kinachofanya niseme unataka kuoa kwa kuongozwa na tamaa zako za kimwili na sio kwa kufuata lengo halisi lililoelekezwa na mwenyezi Mungu ni maneno yako mwenyewe hayo ya rangi ya blue.Wewe unatumia vibaya hii ruhusa kugeuza ufuska na kuuita ndoa.Au maneno yako hapo ndivyo Quran takatifu inavyoagiza hivyo kuwa muoe wake wengi sbb dunia ni kubwa na wazuri ni wengi?

Ofa yako ya kutaka kunifanya mke wa pili iwapo bado sijaolewa naikataa kwa jina la Yesu.Kamwe siwezi kuwa mke wa pili,sbb naamini mim ni malkia mwenye hadhi ya kuwa na himaya yangu peke yangu.Bora niwe bachelor maisha yangu yote kuliko kushiriki mume na mwanamke mwenzangu.

mkuu wangu hata hivyo naona kama nimekutupia shutma nyingi nikasahau kuwa wewe sio mwenye makosa,wenye makosa ni hao wanawake wanaokubali kuolewa uke wenza.Wangekua wanakataa sidhani kama mngepata nafasi ya kuona kuwa wanawake ni kama mashati,ukiona ya kwanza yamepauka hayana mvuto tena unakwenda dukani kutafuta zuri linalovutia.
Nakutakia kila la kheri mkuu wangu ktk ndoa yako ya pili,usinisahau ktk pilau.

La Hapana! Mbona sijasema kuwa ninaowa kwasababu ya hamu ya mwili. Ninachoona mimi ni kuwa wewe unafikiri ndowa inaishia kitendo cha ndowa. Si hivyo kama unavyofikiria wewe.
Kwanini usiniulize kwanini nataka kuowa mke wa pili nawe unaruka tu kuwa nina roho mbaya! Je iwapo mke wangu ana matatizo yanayomfanya asiweze kulea watoto, kwa mfano? Je iwapo mke wangu ananidharau? Bado utaniona mimi nina makosa? Hata hivyo hili la kuopwa ni uhuru wangu ambao hakuna anaeweza kuniingilia kama vile mke wangu anaposema kuwa hanitaki kwasababu zake, unafikiri nitamlazimisha? Tatizo la jamii yetu ni ngono na uhusiani wa jamii mbili unahusanishwa na ngono tu. Hili ndio tatizo kuwa kila mmoja hapa anaruka na kufikiri kuwa naowa kwa kutafuta ngono.
 
umepima afya? huna kisukari usije ukatusumbua kwa kutafuta dawa za kuongeza nguvu kwa kawaida mke wapili huwa ananguvu kwa mwanzo.
ila maisha magumu ebu vumilia
 
umepima afya? huna kisukari usije ukatusumbua kwa kutafuta dawa za kuongeza nguvu kwa kawaida mke wapili huwa ananguvu kwa mwanzo.
ila maisha magumu ebu vumilia

Nauthamini ushauri wako! Lakini usiwe na waswasi gari bovu halibururwi na bovu bali hubururwa na gari nzima! Kuhusu maisha ndio hayo hayo wala sina tamaa kuwa 2015 italeta mabadiliko!
 
Nafsi mchumba wangu ndio inayoleta yote hayo! Nafsi yako inapokuwa haijazidiwa ni rahisi kuona waziwazi lakini nafsi hiyo hiyo ikipenda inaweza ikawa haioni sawsawa na watu wanaweza wakashangaa yale unayoyavumilia.
Sasa mwenzangu iwapo nafsi yangu imeshataka niongeze mke, mke wangu wa kwanza amekubali kuiridhisha nafsi yangu na kuna muhusika wa tatu ambaye kama mke wangu wa kwanza ameshakubali hiyo unayoiita kugawa mapenzi kuna ubaya gani?

Unaweza ukanipa sababu za msingi katika hayo maamuzi yako?? Nafsi yako inakutumaje kwa huyo mke wa pili utakaemuoa?
 
Unaweza ukanipa sababu za msingi katika hayo maamuzi yako?? Nafsi yako inakutumaje kwa huyo mke wa pili utakaemuoa?

Kwa kuanzia nimempenda nae naamini ananipenda! Najaribu kutekeleza haki ya watu wawili mimi na yeye wala sitaki kupata dhambi kwani nimeshaona kuwa hatujiwezi.
 
Mapambano ni sehemu ya raha! Mimi ni mpambanaji na nahisi nimpe afuweni mwenzangu!
umechemka mkuu kuongeza mke nisehemu ya tatiyo unalojijiongezea ushauri wangu kuliko uogenye nibora umuache kwanza huyo japo pia sikushauri umuache tafuta chanzo isije kua wewe nichanzo huyo
 
huyo wa pili umeshampata?ushamuonja?kama ushampata umeshaikurubia zinaa na kama ushamuonja basi umeshazini!na wazinifu unapajua mahali pao bila shaka!achana na mawazo hayo ndugu!si vibaya mkajifunza kwetu tunaooa mke mmoja!
 
Mimi ndio nataka kuowa sio pesa yenye kutaka kuowa! Kama fedha ndio kuowa basi Kina Reginald Mengi wangeowa wengi tu. Suala la kuowa ni uamuzio sio pesa!

usipotoshe watu mkuu!huwa mnaambiwa unaweza kuoa zaidi kama unauwezo wa kuwatunza!na je kuwatunza ni nini ktk dunia ya leo kama si pesa au uwezo zaidi kipesa?
 
Back
Top Bottom