Wewe inaelekea unampenda kwasababu wadau wamekuomba namba yake ya simu ili wakusaidie kukuondolea usumbufu umekataa kuitoa, nasema hivyo kwasababu sijaiona. Kama humtaki muambie ukweli kwa busara sio kishari kwasababu kupendwa na kutamkiwa wazi kwa wanaume ni nadra sana ndugu yangu, hongera kwa hilo. Wanaume mara nyingi hatutamkiwi na mwanamke kwa mara ya kwanza ila ni baada ya mwanaume kuonyesha mapenzi kwa vitendo au kwa maneno, inawezekana kabisa ulimuonyesha mapenzi aidha kwa utani wa maneno au vitendo sio bure. Nachokushauri kama ulimtania mwenzio muombe msamaha na umuambie ukweli kwamba ulikuwa unatania hukumaanisha. Vinginevyo unajitafutia laana ya kucheza na mioyo ya watu na kuwapa msongo mbaya wa mawazo.