SoC01 Sitaki umasikini, ni zamu ya mabadiliko

SoC01 Sitaki umasikini, ni zamu ya mabadiliko

Stories of Change - 2021 Competition

Steccystar

New Member
Joined
Sep 12, 2021
Posts
1
Reaction score
2
SITAKI UMASIKINI, NI ZAMU YA MABADILIKO.

Habari wana Jamii Forum katika jukwaa la story of change.
Andiko hili limelenga kuonesha nini tufanye ili kuondokana na umasikini wa aina zote hasa wa kifikra ambao ndio hupelekea aina zingine zote za umasikini .
Karibu.

SITAKI UMASIKINI
Sitaki umasikini ni kazi mradi ambayo inahusu vijana na kuwalenga moja kwa moja, hasa makundi makuu mawili; wanafunzi na vijana waliokaa mtaani bila shughuli maalumu kwa maana hawa ndio waliopo katika nafasi nzuri ya kufikiwa kirahisi na ndio wahusika wa kiasi kijacho.

KWA NINI KAZI MRADI HII.
Imeonekana katika jamii zetu kuwa vijana wengi walio mitaani na wale walio shule wanashindwa kupata na kufanikiwa kimaisha, ambapo hupelekea kupata matokeo hasi na yasiyoridhisha hatimaye kupelekea kubaki nyuma na kuliendeleza gurudumu la umasikini. Na sababu kubwa inaonekana ni kukosa ushauri sahihi kwa wakati husika na maongozi bainishi wakati wa mapambano.

Hivyo vijana walio wengi wanapoteza tumaini hasa maeneo ya vijijini na asilimia kubwa wale wanaotokea familia masikini. Kwa sababu kunakuwa hakuna wa kuwaongoza, kuwa tia moyo, na kuwahamasisha kwa namna moja au nyingine , na ukiangalia mazingira na watu wanaowazunguka wanaona hali ni ileile na wanalazimika kukubali hali ile , maana wanapoteza tumaini wakiwa kwenye michakato na kuishia kuakata tamaa ambayo ni funguo kuu ya umasikini.


MALENGO YA KAZI MRADI HUU
● Kutokomeza umasikini
Kupandisha ufaulu wa watoto mashuleni kwa kuwasaidia vijana kufika mbali kielimu ambapo wataweza kujisimamia.
● Kusaidia vijana kupata shughuli rasmi.
● Kuwasaidia vijana kuishi kwa kufuata malengo ili hatimaye kutimiza ndoto zao
● Kutengeneza jamii yenye mtazamo chanya kuhusu maendeleo.

KWA NAMNA GANI TUNAWEZA KUFIKIA MALENGO
● Kutembelea vijana mashuleni na kutoa semina za uhamasishaji, kuwashauri ili kuwatia moyo.
● Kuwasaidia kuweka malengo na kujiongoza na kuishi katika malengo na ndoto zao ili hatimaye wafike mahali pazuri.
● Kutembelea vikundi vya vijana mitaani, kusemezana nao, kujua changamoto zao na kuwapa elimu itakatowafanya wajione bado jamii inawategemea, taifa linawategemea na dunia pia.
● Kuwasaidia vijana kuondoa mawazo hasi katika fikra zao kuwapa semina mbalimbali.

JE, NANI AHUSIKE KATIKA HILI
Watu wafuatao wana nafasi kubwa sana ya kubadilisha fikra za vijana na kuzifanya kuwa chanya.
● Viongozi wa aina zote kama vile viongozi wa serikali , viongozi wa dini na viongozi katika mashirika mbalimbali .
● Watu waliofanikiwa kimaisha.
Wanachuo.
● Jamii nzima kwa ujumla kwa sababu wote ni wahusika.

Hivyo basi; Kwa kufanya hivo tutaweza kuondoa umasikini katika jamii zetu kwa kubadilisha mitazamo yetu kwa maana mitazamo ndiyo hupelekea jinsi tunavyoishi.
 
Upvote 4
hongera mkuu ni wazo zuri,ila impact yake itakuwa kubwa kama mitaala inayofuundishwa shuleni itabadilishwa iendane na kasi ya karne ya 21. Kuwatia moyo vijana wasome kwa bidii mambo ambayo hayatawasaidia kwangu mimi ni kupoteza muda,wazo zuri lakini linahitaji mambo kadhaa yaongezewe liwe lenye tija.
 
Back
Top Bottom