Sitakufa, bali nitaishi

Sitakufa, bali nitaishi

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!

Leo ni jumapili njema sana, hatimaye tumeungana tena na mpendwa wetu ndugu Philip Mpango.

Ametupa ujumbe wa Leo Kutoka kitabu cha (Zaburi 118:17) usemao:

SITAKUFA,BALI NITAISHI, NIUSIMULIE WEMA WA BWANA.

Na kuusimulia wema wa Mungu ni katika Nchi Walio hai, maana imeandikwa pia, Kuzimu haitakusifu.

Amesema kuwa, KAZI iliyomleta duniani, hajaikamilisha Bado hivyo hawezi kufa kabla ya wakati.

Usisahau kuwakumbusha wote wenye kukuchulia kifo, Kwa kuquote kifungu hiki Cha BIBLIA, ukiwaambia kuwa SITAKUFA, BALI NITAISHI. (Zaburi 118:17).

Mungu atubariki sote. Jumapili njema.

Amen
 
Naomba kujua maana halisi ya huo mstari wa sitakufa bali nitaishi ikiwa kuanzai adam kiumbe wa kwanza kuumbwa hatunaye na kila Leo watu wanakufa na hakuna kiumbe kitachobakia
 
Salaam, Shalom!!!

Leo ni jumapili njema sana, hatimaye tumeungana tena na mpendwa wetu ndugu Philip Mpango.

Ametupa ujumbe wa Leo Kutoka kitabu cha (Zaburi 118:17) usemao:

SITAKUFA,BALI NITAISHI, NIUSIMULIE WEMA WA BWANA.

Na kuusimulia wema wa Mungu ni katika Nchi Walio hai, maana imeandikwa pia, Kuzimu haitakusifu.

Amesema kuwa, KAZI iliyomleta duniani, hajaikamilisha Bado hivyo hawezi kufa kabla ya wakati.

Usisahau kuwakumbusha wote wenye kukuchulia kifo, Kwa kuquote kifungu hiki Cha BIBLIA, ukiwaambia kuwa SITAKUFA, BALI NITAISHI.

Mungu atubariki sote. Jumapili njema.

Amen
Weka video
 
Dr. Phillip Isdor Mpango. Mpole. Humble. Kiongozi!

Tulikutana Dodoma Julai mwaka huu tukaongea kishikaji sana utafikiri napiga stori na classmate tu.

Mungu Akushike mkono na kukuvusha katika changamoto yo yote inayokukabili. Taifa letu bado linakuhitaji hata kama unaonekana kuwa tishio kwa baadhi ya watu kuelekea 2025/2030.

Kweli hutakufa bali utaishi ili uje uusimulie wema wa Bwana. Tunakuombea!🙏🏿🙏🏿🙏🏿

Naomba kujua maana halisi ya huo mstari wa sitakufa bali nitaishi ikiwa kuanzai adam kiumbe wa kwanza kuumbwa hatunaye na kila Leo watu wanakufa na hakuna kiumbe kitachobakia
Maana ya mstari huo ni kuwa wamwaminio Mungu, hawafi kabla ya wakati wao. Lazima watimize kusudi lao duniani Kisha waendelee na maisha ya milele Mbinguni.

Mungu ni Mungu wa Walio hai,

Elia Hadi Leo Yu hai Mbinguni, Mussa Yu hai Mbinguni , nk nk

Mwamini Yesu uishi milele

Amen
 
Dr. Phillip Isdor Mpango. Mpole. Humble. Kiongozi!

Tulikutana Dodoma Julai mwaka huu tukaongea kishikaji sana utafikiri napiga stori na classmate tu.

Mungu Akushike mkono na kukuvusha katika changamoto yako ya kiafya inayokukabili. Taifa letu bado linakuhitaji hata kama unaonekana kuwa tishio kwa baadhi ya watu kuelekea 2025/2030.

Kweli hutakufa bali utaishi ili uje uusimulie wema wa Bwana. Tunakuombea!🙏🏿🙏🏿🙏🏿
AFYA Si sababu,

Ikiwa muda wako haujafika, watakufa wazima, watakuacha.

Lowwassa ni funzo kwetu pia.
 
tulihitaji tu taarifa, sisi watanzania wote ni ndugu, kutoonana wiki moja tu lazma tuulize mwenzetu yuko wapi, kama ni mgonjwa tunaombeana na kusaidiana, kama ana changamoto tunashirikiana... kwa mapenz tuliyonayo kwa mzee Mpango, hakuna aliyekuwa anatamani kusikia limempata lolote baya, ila kutoonekana na ukimya wa mamlaka ulituweka mashakani, na mashaka haya yaliongozwa hasa kutokana na kumbukumbu mbaya tulionayo kuhusu siku za mwisho za mzee Magufuli, kwahyo kukuona tena hadharani ni furaha kwetu.
Tumsifu Yesu Kristu
 
Binadamu aliyezaliwa na mwanamke, kifo ni lazima, ila lini umauti utakupata ndio fumbo kubwa la kila mmoja wetu, so asipanic, wala maneno ya watu yasimpe stress, as long ni public figure watu kukuongelea kwa baya au zuri ni lazima.
 
Amina,sitakufa bali nitaishi,hadi nitimize kusudi la Mungu duniani
 
Binafsi nikimsikia mkristo akitamka huo mstari,ninajua kwa hakika anamshuhudia Mungu kwa kupita kwenye bonde la uvuli wa mauti. Kuna Zaburi nyingi sana za kushuhudia ukuu wa Mungu,ukiona kachagua inayogusia kuwa Mungu ndiye aliyebeba uhai na hivyo ukuu wake ataushudia,jua kuna la wanadamu limefeli. Alipomalizia kuwa hajakamilisha kusudi ndio kabisaa nimethibitisha kuna mkono ulitaka kumtoa kwenye kuthibitisha kusudi analoamini ni lake amepewa na Mungu. Ni tafsiri yangu.
 
Amemwambia Mh Rais Samia kuwa,nadhani unaniona, Niko mzima kabisa, hata sijapungua popote.

Alikuwa na furaha sana.

Mungu anatupenda Watanzania.

Tuzidi kuwaombea na kuwabariki viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom