Sitamani kufuga kuku tena.

Tumia AKHEIR POWDER itamaliza hao wadudu
Kinachonishangaza ina maana huyu Mdau hakufanya home work yoyote kabla kufuga? maana utitiri haipaswi kuwa ni changamoto kubwa kwa mfugaji mwenye nia ya dhati.
 
Hahahaha,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuku watamu hawa!
 
Siku utitiri ukihamia kwenye nyumba yako ya kulala utatamani kuihama hata nyumba maana hautalala.
 
Hakuna mfugaji hapo. Huyu jamaa kaniudhi sana.
sawa na tuseme fundi magari anaogopa kuchafuka kwa oil. Au mwenye shamba anaogopa magugu.

Namshauri aachane na hiyo kazi akauze vitumbua ndo saiz yake.

Kuna watu wanatia hasira Sana.
 
Changamoto ndogo ndogo ndyo zikufanye uhairishe kufuga kuku kweli? Labda kuna lingine, zingatia usafi Wa banda, huo utitiri sometimes hutokea ikiwa kuna maganda ya mayai(after kuku kutotoa na hayajatolewa, kinyesi chao pia ).BTW una miguu amaizing(mifupiii)
 
Nisipopata solution sifugi tena, hiyo ndo dhamili yangu maana sio kwa kero hii ya utitiri
Mkuu kwa nini wadudu wadogo namna hiyo na wasiyo na akili wanataka kukushinda maarifa. Utitiri ni rahisi sana kuumaliza. Kwanza nikukumbushe: hasara ya utitiri siyo wewe kuwajikuna tu ila hata kuku wanadhoofika sana. Hao utitiri huenda wanakuja na kuku unaonunua kwani sehemu za vijijini ni wengi. Dawa ya utitiri ni 1. Usafi kwenye banda la kuku: Usiacha matakataka mengi na jaribu kumwagilia maji kila siku ili kupunguza vumbi kwani utitiri kamwe hawawezi kuishi kwenye unyevu. Nguzo na kona zote za banda hakikisha hazina mavumbi. (ila usitengeneze tope) 2. Kuna dawa ya unga unashika kuku mmoja mmoja unamnyunyizia na kuhakikisha dawa imeingia kwenye manyoya yote. Rudia zoezi kulingana na matumizi ya dawa mpaka uhakikishe wameisha. Hata wakiisha zingatia usafi na kunyunyizia dawa. Utitiri ni rahisi sana kuudhibiti.
 
Kisichokuua kitakuimarisha!
 
Akheir pouda inauzwa 2,000 inafaa sana tena unaweza kuitumia hatá mwaka mzima .iko poa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…