Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 20,694
- 32,527
Moja ya vitu ambavyo hushangaza kwa sisi watu ambao tupo kwenye ulimwengu wa 3 ni namna tunavyofanya maamuzi.
Ukweli usiopingika ni kuwa tunahitaji wanasiasa watuongoze na ndio mfumo upo hivyo na wala sio jambo baya.
Siasa katika nchi zetu ni biashara kubwa pengine kuliko zilivyo biashara zingine na ndio maana wanasiasa hutumia pesa nyingi na kila aina ya mbinu ili wapate madaraka.
Ukweli ulio wazi kwenye nchi yetu moja ya watu ambao wanapata pesa nyingi ni wabunge (sidhani Kama mtu atabisha hili na ndio maana miaka na miaka watu wamekua wakilalamika malipo ya wabunge).
Hivyo kutokana na hoja nzito hapo juu, ni jukumu la mwanasiasa kujua anapopata pesa anatakiwa afanye nini na kwa wakati gani.
Ikatokea mwanasiasa yoyote akapata tatizo na amewahi kupata malipo Kama ya ubunge basi Ni jukumu lake kutumia vyanzo vyake vingine vya mapata kutatua matatizo yake.
Kama hana vyanzo vingine, hiyo nayo haituhusu ni uzembe wake.
Mwanasiasa ambae anauza maneno tu, Leo apate tatizo nimchangie? Hapana.
Mwanasiasa ni jukumu lako kutafuta namna ya kutunza kipato chako, Wala sio jukumu letu kukusaidia unapopata tatizo.
#kazi iendelee#
#T2025 SSH#