Sitasahau biashara ya uchimbaji ilivyonifilisi

Mkuu kwanza nikupe Hongera kwa kuthubutu....
Coz siku zote wanaojaribu na kufanya ndo Wanaofanikiwa.... Kama huwezi kujaribu na kupoteza huwezi kufanikiwa....
Hata hao unaowasema kuwa Wananunua Magari kama Ndala, wamepitia changamoto nyingi na kupoteza sana....

Kama kuna Watu waongo basi ni Wachimbaji wa Madini..... Wanaweza kukutia Moyo kwa kitu ambacho hakipo.... Wakikupigia hesabu wanakwambia hapa Mizamo 3 tumeufikia Mwamba tunaanza kuzarisha.... Wanapokupigia hesabu za kudhamini duara hawakupi hesabu kamili, wanakukadiria hesabu Ndogo tu ya Chakula na Vitendea kazi vichache wastani wa 200,000 ambapo utaona ni ndogo na unaweza kumudu..... Baadaye mkishaanza ndo wanaleta hesabu za vitu vingine.....

Ushauri wangu kwako usiache, Ungewaacha wenyewe waende kwa Waganga n.k ila Wewe ungefanya kazi kitaalam.... Mfano mlipoufikia Mwamba ungepeleka Sample Maabara, ingesoma Kiwango cha Dhahabu kilichomo, then baada ya kuchimba Mita kadhaa ungechukua tena sample Maabara ingekupa majibu kuwa kadri unavyokwenda kiwango cha Dhahabu kinaongezeka ama vipi!?

Kuna sehemu unasema jamaa walipiga chabo ikasoma Dhahabu kidogo na Copper nyingi means ukienda chini zaidi Copper itaanza kupungua na Dhahabu kuongezeka!

Omba Ushauri kwa Wazoefu pia unaweza kuleta Geologist kwenye Duara lako akakushauri.
All in all Hongera na usiache, kusanya nguvu rudi tena, ila fanya kazi kisasa..
 
AHHAHHAHAHHAH imagine umechimba shimo uko furi 50 halafu anakuja mganga anakuambia mbona madini yapo juu umepitiliza,,,,,, pole sana boss.
 

Asante mkuu.
AqSio copper ni silver.
Ule mwamba ulibadilika na kuwa westi ambapo kitaalamu dhahabu ipo mbali sana. Kwa mtu mdogo huwezi kufika
 
Hahahaaa kiukweli kazi ya machimbo yahitaji msuli na uvumilivu sana

Kuna washkaji walipata gema moja linatoa kinyama pande za chunya maeneo ya swiswi

Wakaingiwa tamaa wakashauriana watanue liwe kubwa halafu washushe kimo kirefu kwenda chini ili kuzinyaka

Walitumia gharama nyingi sana kwa kudhani kua watazifidia endapo wakifika chini walikopanga kufikia

Lakini walipofika chini walikuta uwazi mkubwa, ambao unaonesha kua kuna fonka ilipigwa chini kwa chini na wazee wazamani

Walichoka maana hakukuwa na tumaini tena ikabidi wasande warudi home kupiga mishe zingine ili walipe madeni ya watu

It's Scars
 
Asante mkuu.
AqSio copper ni silver.
Ule mwamba ulibadilika na kuwa westi ambapo kitaalamu dhahabu ipo mbali sana. Kwa mtu mdogo huwezi kufika
Okay... Kila la heri.
 
Ivi jamani naombeni kuuliza hao wachimbaji mfano wamechimba wakapata dhahabu kweli hapo unaichukuaje wakati na wao wanaitamani,kwamaana nauliza ivyo kwakuwa mnaliona dini lipo hapo si ndio mwanzo wa kuuliwa hapo ama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…