“Sitasahau Kazi Niliyoipata ya Kuuza Vyombo Mtaani

Zerock

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2026
Posts
853
Reaction score
1,701
Nakumbuka siku moja nikija kwenye msoto na ukata + jobless,nimekaa zangu nasikiliza redio flan kipind cha michezo. Mara likatolewa TANGAZO LA KAZI,nikaona fursa hii hapa,nikanakiri zile namba.

Baada ya kumaliza kipindi cha michezo nikaamua kuipiga ile namba....mara nikasikia saut ya kike...kama kawaida salamu baada ya hapo nikamuuliza ofisi yao iko sehemu gani,akanielekeza...kwa vile muda ulikuwa ushaenda sana nikaamua kwenda kesho yake.

Nilipofika ofisin kwao.... Nilishangaa kidogo kutokana na mazingira ya ofisi... ....nikafanya interview kidogo,nikapewa fomu ya kujaza kila kitu Nikaambiw nipeleke barua ya (sheha) kesho yake,nikasema sawa 👍.

Katika safari ya kurudi nyumban,nikaongozana na jamaa nae alikuwa anatoka hapo ofisin, lakin yeye alishtuka zaidi yangu....

Jamaa: Husikute hawa jamaa ni wale wanaowapa vijana wa kinyamwezi mabeseni,masufuria,majagi,sumu za panya na mende wanazunguka huko mitaani wakiuza.
Mimi:🤔 inawezekana eeh...!??

Jamaa: Mimi sirudi tena,hiyo siyo kazi,kulanda na vyombo kuanzia asubuh hadi jioni na hauna uhakika wa kuuza...

Mimi:kweli siyo dili,mimi nilikuw sijui haya makampuni, kumbe ndo yanayowaajiri wanyamwezi.

Baada ya kufika kituon,tukaachana kila mtu akashika njia yake. Sikurudi tena kwenye ile kampuni.
Kumbe ilikuwa ya kuuza vyombo vya ndani.

Wanakupa vyombo unaenda kuuza mitaani,kipato chako kinapanda kutokana na mauzo yako.
Kazi za kiha na wanyamwezi
 
🥸🥸🥸
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…