Unaweza fikiri labda ni utani lakini hili ni tukio lililonipata miaka zaidi ya kumi wakati nikiwa mfanyabiashara wa samaki
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumanne nikiwa nimeenda kuuza samaki kijiji kimoja cha huko Muleba nikiwa mimi na mjomba wangu
Kijiji hicho kilisifika kwa wizi & ujambazi hali iliyowafanya wafanyabiashara wengi kutopenda kufanyiapo biashara,nakumbuka wakati mimi na mjomba wangu tumepanga kwenda kuuza samaki kijijini humo tulionywa sana na wafanyabiashara wenzetu lakini kwa sababu ya tamaa tulilazimika kutia pamba masikioni na kuazimia kwenda kuuza samaki kijiji humo
Kuifanya story ndefu kuwa fupi siku hiyo ya jumnne tulikwenda kijijini humo na mizigo ya kutosha,tuliuza samaki zetu tena kwa kung'ang'aniwa,nakumbuka nilipata zaidi ya sh laki 6 & ½ na mjomba wangu alipata zaidi ya laki 5
Baada ya biashara tuliamua sasa tufanye utaratibu wa kurudi nyumbani lakini wakati tunasubiria usafiri nilikutana na rafiki yangu wa utotoni ambae nilikuwa na miaka zaidi ya 8 bila kumuona,alinishawishi sana nikalale nyumbani kwake halafu kesho yake yaani j5 ningeendelea na safari basi kwa kuwa nilimheshimu sana huyu mchizi wangu wa utotoni nilimkubalua ila kwa sababu ya kuhofia kupukutishwa ile pesa yangu ya mauzo nilimkabidhi mjomba wangu ambae yeye aliendelea kusubiria usafiri kwa sababu aligoma Kata kata kulala kijijini humo ambako kwa enzi hizo ilikuwa ni kama paradiso ya majambazi
Nilifika nyumbani kwa rafiki yangu ambae alikuwa akiishi nyumba ya shule,nilioga tukala tukapiga story mpaka zikatukinaisha akanionesha chumba cha kulala nikalala
Nilipata usingizi bila shida ila shida sasa ilianza nikiwa usingizini,nahisi kama vile ilikuwa ni saa 9 na madakika usiku nilikurupuka ghafla baada ya kuhisi kama mlango wa chumba nilichokuwa nimelala umevunjwa
Kabla ya hata sijajinyoosha nilimulikwa na mwanga mkali sana wa yale matochi ya kizamani huku nikipewa amri ya kukabidhi mauzo yote ya pesa niliyouza samaki au wanifanyie kitu kibaya kabisa kuwahi fanyiwa binadamu mwenye damu & nyama
Niliwaeleza ukweli wangu kuwa pesa yote nilimkabidhi mjomba wangu ambae kwa sasa atakuwa ameshaondoka humo kijijini
Nashukuru hawakunipiga ila wawili walienda wakanongonezana maneno ambayo sikuyasikia vizuri kisha ikatolewa amri ya kunipekua
Wale majambazi kiukweli kama ni kuwa na nuksi walikuwa na nuksi kwelikweli walikuta na shilingi mia tatu tu,ninaposema mia tatu namaanisha mia mia 3(300) tena ikiwa kwenye kamfuko kale kadogo ka jeans.Kumbe wakati namkabidhi mjomba ile pesa ya mauzo nilisahau kuchomoa pesa kidogo ya nauli kutokana na kunogewa na mazungumzo ya yule mchizi wangu wa utotoni
Walinitazama sana usoni kisha wakaniuliza dogo una uhakika hii ndio pesa pekee uliyobakiza nilijibu ndio,waliangua kicheko kikubwa halafu nikaamuliwa kulala kifudifudi nikatii amri ya kwa speed ya mwanga,nikasikia wakinongonezana halafu nikasikia harufu ya sigara,sikuthubutu kuinua kichwa bali uhai na marinda yangu nilimuachia Allah
Ikawa kama utani ikapita dakika tano bila kupigwa hata Kofi,Mara dakika 10 mara masaa nikaona ufala nikajigeuza taratibu du sikuamini macho yangu hakukuwa na MTU
Nikachukua suruari yangu kuipekua nikakuta ile mia tatu majambazi wamesepa nayo du kweli majambazi hayaachi kitu mpaka mia 3 wameshindwa kuniachia
Angalizo:asitokee mtu wa kuniuliza kuwa wakati majambazi wameniweka mtu kati rafiki yangu alikuwa wapi ?