SITASAHAU ; Mkesha wa mwaka mpya 2001.

SITASAHAU ; Mkesha wa mwaka mpya 2001.

trudie

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
3,668
Reaction score
8,745
Habari wanaJF, natumai tunajiandaa kuumaliza mwaka 2022, na kuupokea mwaka 2023 salama na kwa amani tele. Leo nashea kakisa kadogo kalikonipata wakati mtoto miaka kadhaa nyuma.

Miaka 21 imetimia sasa toka nilipopata kisa hiki nikiwa mtoto mdogo. Miaka ya 2001 nikiwa binti wa pekee nina miaka 8 nilikuwa naishi na mama yangu. Kipindi hicho mzee alikuwa anakaa sana site ( shughuli za magari) na mara nyingine anakuwa nyumbani.
Basi kutokana na mama kuwa na biashara zake siku nyingine anachelewa kurudi nikawa naogopa kukaa mwenyewe ananikuta namsubiri nje usiku. Hivyo akamuomba baba mkubwa mtoto wake mmoja wa kiume aliyenizidi miaka kama 3 au 4 tuishi nae kuondoa upweke.

Basi siku zikaenda ikafika siku mwisho wa mwaka 31.12.2001 siku ya mkesha wa kuupokea mwaka mpya 2002. Usiku ulipofika mama akatuaga anaenda kanisani kwa ajili ya mkesha na akatusihi tutulie ndani tufunge mlango mpaka atakaporudi tukatii. Basi mida imeenda kufika saa 4 usiku shamra shamra zikaanza ngoma na nyimbo zinapigwa nje.
Mikesha ya zamani ilikuwa na vibe sana sio kama miaka hii kila mtu anatulia ndani. Watu wa rika mbalimbali walikuwa wanajichanganya kuimba na kupiga ngoma na madumu huku wakicheza mtaa kwa mtaa.
Tumekaa ndani tunasikiliza tuu shangwe nje zinaendelea, kaka yangu akaniambia kwanini tusiende na sisi tukacheze nikamwambila ila mama katukataza tusifungue mlango kuna wezi na watekaji wa watoto tusije tukauawa. Kaka yangu akaniambia acha woga vaa koti na viatu halafu kila mtu atabeba kisu ndani ya koti atakayejaribu kututeka tunamuua.
Basi nikavaa koti langu na viatu vya boot ( siku hizi wanaziita American boot) wanavaa sana wanaume ila enzi zile tulikuwa tunavaa hadi watoto wa kike na soksi na gauni fresh. Tukaweka visu ndani ya makoti, tukamwaga maji kwenye madumu, beba madumu hao funga mlango funguo nikaweka mfukoni tukatoka kufwata ngoma za mkesha huku ma sisi tunapiga madumu na kuimba.

Sent using Jamii Forums mobile app
View attachment 2464313
 
Basi tukaungana na ngoma, vibe za kutosha wadada na wamama mpaka wanamwaga radhi kabisa. Tulizunguka mitaa mingi sana muda unazidi kwenda kuelekea mwaka mpya.
Baadae ngoma ikazunguka mpaka tukatokea mjini ambapo kuna stendi na makanisa yapo karibu tukakutana na watu wengi sana tunaowajua na tusiowajua.
Huku ngoma zimeungana sasa na wengine na saa 6 imeshafika shangwe mji mzima, kaka yangu akaonana na marafiki zake anaosoma nao akanifwata kuniaga anaenda kucheza gemu na karata na marafiki zake hivyo akanikabidhi dumu lake akaniambia wewe fwata ngoma mpaka itakapofika mtaa wa nyumbani uingie ndani mimi nitarudi kesho nalala huko huko.

Kaka akaondoka ngoma zikacheza baadae tukaanza kutawanyika kwa vikundi kurudi mitaani kwetu na mimi nikafwata kikundi nilichokuja nacho. Huku tunapiga ngoma watu wakaanza kupungua. Mtu akifika mtaani kwao anaingia ndani mara tukabaki wachache halafu bado sana kufika nyumbani. Baada ya muda nikanikuta nimebaki mwenyewe watu wa mwisho wananiaga na kuingia ndani. Kumbe ngoma haikuwa ya mtaani kwetu bali mtaa wa ng'ambo.
Hapo nipo mtaa wa pili kufika kwetu ambao umetenganishwa na daraja na msitu mkubwa sana unaitwa msitu wa Makinda, una miti imeshonana minene na makaburi ndani yake.
Huu ni msitu wa mtu binafsi hivyo kulikuwa na makaburi ya ukoo. Njia imepita katikati ya msitu na makaburi panatisha kweli kweli.

Kulikuwa na stori za kutisha kuhusu msitu huo kwamba una mauza uza na lile daraja kuna majini hivyo watu walikuwa hawapiti kizembe usiku hata mchana wanapita wawili kuendelea. Na kufika nyumbani ni lazima nivuke daraja, nipite msituni. Na ukiangalia nina funguo za nyumbani mama lazima amerudi toka kanisani. Nilidata na kuanza kulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ningefikiria mapema kutoka kanisani mpaka nyumbani ni njia ambayo haitishi na watu wanapita, nyumba nyingi ila akili ya utoto sikuwaza nikafwata ngoma ambayo ilizunguka hadi kutokea mtaa mwingine.
Baada ya kulia na kujishauri wee nikaona bora nijipe ujasiri nirudi tuu nyumbani.

Nikaanza kutembea pole pole huku nalia na kusali salamu maria za kutosha hapo natetemeka sana na
madumu mawili yangu mkononi.
Baada ya mwendo mbele yangu naliona daraja na mwanzo wa daraja kuna nyumba moja ambayo imejitenga na nyingine haikaliwi na watu kabisa, stori za watu wanasema hiyo nyumba ina mauza uza sana na ndio makazi ya majini huwezi pita hapo salama bila kuona maajabu.

Nililia na kutetemeka ila safari inaendelea nikafika karibu na nyumba yenye mauza uza mwili unasisimuka na nywele kama zinasimama natetemeka mpaka nashindwa kutembea vizuri kuna muda najikwaa sababu miguu inagongana na madumu. Nilianguka kutokana na kujigonga na madumu nimelala chini nahisi kama kuna watu wanapita ila siwaoni, nikainuka kutembea nikahisi nimepishana na mtu na kanigusa kabisa lakini simuoni mtu. Nikaendelea na safari huku nalia na kusali.

Basi nikaipita nyumba na kuvuka daraja bila shida yoyote ila mbele ndio naingia msituni ambapo lazima upite makaburini. Woga ulizidi. Nikatembea hadi naanza kuyaona makaburi hapo salamu maria haikakuki mdomoni uso umelowa machozi. Ghafla mbele ya makaburi nikaona kama mtu kasimama anaangalia ninapotokea mimi ikabidi na mimi nisimame nikajua ni jini nikimbie. Mara akasimama mtu wa pili pale pale wakawa kama wanataka kuja upande wangu nikarudi nyuma.

Ndani ya sekunde wakasimama watu wengi kama kikundi hivi ( nikifikiria sasa hivi ni kama scene ya wimbo na mkongwe Michael Jackson Thriller wale mazombi walivyokuwa wanaibuka makaburini). Wote wakasimama wanaangalia upande niliosimama mimi, basi nikarudi nyuma tena hatua chache hapo nimeshajikojolea kitendo cha kurudi nyuma wale watu wakatimua mbio kila mtu uelekeo wake.

Nahisi hao watu walijua we ni mzimu wa mtoto.maana ni nadra kukuta mtoto anatembea mwenyewe gizani.sa ujasiri wako wa kutokimbia wakajua mzimu.[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Back
Top Bottom