SITASAHAU ; Mkesha wa mwaka mpya 2001.

SITASAHAU ; Mkesha wa mwaka mpya 2001.

Basi tukaungana na ngoma, vibe za kutosha wadada na wamama mpaka wanamwaga radhi kabisa. Tulizunguka mitaa mingi sana muda unazidi kwenda kuelekea mwaka mpya.
Baadae ngoma ikazunguka mpaka tukatokea mjini ambapo kuna stendi na makanisa yapo karibu tukakutana na watu wengi sana tunaowajua na tusiowajua.
Huku ngoma zimeungana sasa na wengine na saa 6 imeshafika shangwe mji mzima, kaka yangu akaonana na marafiki zake anaosoma nao akanifwata kuniaga anaenda kucheza gemu na karata na marafiki zake hivyo akanikabidhi dumu lake akaniambia wewe fwata ngoma mpaka itakapofika mtaa wa nyumbani uingie ndani mimi nitarudi kesho nalala huko huko.

Kaka akaondoka ngoma zikacheza baadae tukaanza kutawanyika kwa vikundi kurudi mitaani kwetu na mimi nikafwata kikundi nilichokuja nacho. Huku tunapiga ngoma watu wakaanza kupungua. Mtu akifika mtaani kwao anaingia ndani mara tukabaki wachache halafu bado sana kufika nyumbani. Baada ya muda nikanikuta nimebaki mwenyewe watu wa mwisho wananiaga na kuingia ndani. Kumbe ngoma haikuwa ya mtaani kwetu bali mtaa wa ng'ambo.
Hapo nipo mtaa wa pili kufika kwetu ambao umetenganishwa na daraja na msitu mkubwa sana unaitwa msitu wa Makinda, una miti imeshonana minene na makaburi ndani yake.
Huu ni msitu wa mtu binafsi hivyo kulikuwa na makaburi ya ukoo. Njia imepita katikati ya msitu na makaburi panatisha kweli kweli.

Kulikuwa na stori za kutisha kuhusu msitu huo kwamba una mauza uza na lile daraja kuna majini hivyo watu walikuwa hawapiti kizembe usiku hata mchana wanapita wawili kuendelea. Na kufika nyumbani ni lazima nivuke daraja, nipite msituni. Na ukiangalia nina funguo za nyumbani mama lazima amerudi toka kanisani. Nilidata na kuanza kulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asa wakati mnapita mnatoka nyumbani huakuuona huo msitu?? Harufu ya chai hapa
 
Na mimi nikatimua mbio nakimbia huku nalia nikafika mbele nikajikwaa kwenye jiwe nikaanguka na kujibonda uso kwenye jiwe kubwa, mawe yale tulikuwa tunaita "magangaluma" jiwe lipo kama Chuma asiee.

Hapo nilipokimbilia miti minene ya milingoti nimeipita sasa mbele unaanza miti ya mihanzi ambapo baadhi ya watu walikuwa wanagema ulanzi ( wenyeji wa Iringa watakuwa wanajua). Yale maumivu ya kujibonda kichwa nikatulia kwa muda kwanza yapoe nahisi pia nilichanganyikiwa na wale watu.

Baada ya muda akili ikarudi nasikilizia hakuna chochote nikainuka wale watu sijui walipotelea wapi na mbio zao nikaendelea na safari hadi nikamaliza msitu nikatokea barabarani sasa.
Hapo sasa ndio nikapata matumaini ya kufika nyumbani ingawa njia ilikuwa kimya na giza limetanda nikawaza hapa sasa sitembei tena bora nikimbie tuu. Nikakimbia mpaka nimefika nyumbani. Namkuta mama amekaa nje nae analia.

Basi kuniona na hali niliyokuwa nayo macho yamejaa machozi, mdomo una damu na nimepata nundu na madumu yangu mikononi akajua tulikuwa kupiga ngoma ikabidi anikumbatie kwanza na kuniuliza mwenzako yuko wapi nikamwambia yupo na marafiki zake. Basi tukaingia ndani, yeye akaenda kwa mjumbe kutaarifu kwamba mtoto mmoja amerudi kumbe alivyokuta hatupo akaenda kutoa taarifa kwa mjumbe akiwaza labda tumepatwa na maswaibu mabaya.

Mama hakunipiga wala kunikaripia nahisi na yeye alinionea huruma jumlisha kitete cha kukuta watoto hawapo.
Kaka yangu alikuja kurudi kesho yake mchana maisha yakaendelea kama kawaida. Ingawa nilisherekea mwaka mpya nimevimba uso na ndomo.

Basi nilivyomsimulia mama akaniambia kwenye makaburi usiku wahuni huwa wanakaa kuvuta bangi kwa hiyo wale watu watakuwa walikuwa wanavuta bangi ila walitishika na kuona mtu mfupi anakuja mbele yao usiku ule na watu wa kawaida hawapiti hivyo. Kipindi hicho nilikuwa mdogo halafu mfupi labda nao walihisi kibwengo tena kimebeba na mizigo ( madumu yale) wakatimua mbio. Miaka mingi mama alikuwa ananikumbusha na kunicheka.

Ule msitu bado upo ingawa sasa hivi miti imekatwa sana kwahiyo hautishi kama zamani ingawa sasa makaburi yanaonekana vizuri baada ya miti kukatwa. Tukio lilitokea Njombe, mtaa nilipoachwa na ngoma unaitwa Kihesa na ulitenganishwa na daraja na msitu ili kufika mtaa wa Mgendela.
Huo msitu wa Makinda ulikuwa maarufu sana zamani ni msitu wa ukoo wa yule Spika wetu wa zamani.

Ni miaka 21 imepita sasa nikikumbuka huwa nawaza ujasiri wa kupita pale ambapo ingenitokea ukubwani hivi ni bora ningelala kwa watu sio kurudi nyumbani. Watu wengi walishakutana na mauza uza hapo akiwepo mwanafunzi mwenzetu wa darasa moja kabisa.

Happy new year 2023!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahisi hao watu walijua we ni mzimu wa mtoto.maana ni nadra kukuta mtoto anatembea mwenyewe gizani.sa ujasiri wako wa kutokimbia wakajua mzimu.[emoji38][emoji38][emoji38]
Hata mama yangu aliniambia watakuwa walihisi ni kibwengo na ufupi wangu. Maana hata yeye alishawahi kutana na kamtu kafupi usiku saa 7 tena kakamsalimia kwa kumtaja jina lake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na mimi nikatimua mbio nakimbia huku nalia nikafika mbele nikajikwaa kwenye jiwe nikaanguka na kujibonda uso kwenye jiwe kubwa, mawe yale tulikuwa tunaita "magangaluma" jiwe lipo kama Chuma asiee.

Hapo nilipokimbilia miti minene ya milingoti nimeipita sasa mbele unaanza miti ya mihanzi ambapo baadhi ya watu walikuwa wanagema ulanzi ( wenyeji wa Iringa watakuwa wanajua). Yale maumivu ya kujibonda kichwa nikatulia kwa muda kwanza yapoe nahisi pia nilichanganyikiwa na wale watu.

Baada ya muda akili ikarudi nasikilizia hakuna chochote nikainuka wale watu sijui walipotelea wapi na mbio zao nikaendelea na safari hadi nikamaliza msitu nikatokea barabarani sasa.
Hapo sasa ndio nikapata matumaini ya kufika nyumbani ingawa njia ilikuwa kimya na giza limetanda nikawaza hapa sasa sitembei tena bora nikimbie tuu. Nikakimbia mpaka nimefika nyumbani. Namkuta mama amekaa nje nae analia.

Basi kuniona na hali niliyokuwa nayo macho yamejaa machozi, mdomo una damu na nimepata nundu na madumu yangu mikononi akajua tulikuwa kupiga ngoma ikabidi anikumbatie kwanza na kuniuliza mwenzako yuko wapi nikamwambia yupo na marafiki zake. Basi tukaingia ndani, yeye akaenda kwa mjumbe kutaarifu kwamba mtoto mmoja amerudi kumbe alivyokuta hatupo akaenda kutoa taarifa kwa mjumbe akiwaza labda tumepatwa na maswaibu mabaya.

Mama hakunipiga wala kunikaripia nahisi na yeye alinionea huruma jumlisha kitete cha kukuta watoto hawapo.
Kaka yangu alikuja kurudi kesho yake mchana maisha yakaendelea kama kawaida. Ingawa nilisherekea mwaka mpya nimevimba uso na ndomo.

Basi nilivyomsimulia mama akaniambia kwenye makaburi usiku wahuni huwa wanakaa kuvuta bangi kwa hiyo wale watu watakuwa walikuwa wanavuta bangi ila walitishika na kuona mtu mfupi anakuja mbele yao usiku ule na watu wa kawaida hawapiti hivyo. Kipindi hicho nilikuwa mdogo halafu mfupi labda nao walihisi kibwengo tena kimebeba na mizigo ( madumu yale) wakatimua mbio. Miaka mingi mama alikuwa ananikumbusha na kunicheka.

Ule msitu bado upo ingawa sasa hivi miti imekatwa sana kwahiyo hautishi kama zamani ingawa sasa makaburi yanaonekana vizuri baada ya miti kukatwa. Tukio lilitokea Njombe, mtaa nilipoachwa na ngoma unaitwa Kihesa na ulitenganishwa na daraja na msitu ili kufika mtaa wa Mgendela.
Huo msitu wa Makinda ulikuwa maarufu sana zamani ni msitu wa ukoo wa yule Spika wetu wa zamani.

Ni miaka 21 imepita sasa nikikumbuka huwa nawaza ujasiri wa kupita pale ambapo ingenitokea ukubwani hivi ni bora ningelala kwa watu sio kurudi nyumbani. Watu wengi walishakutana na mauza uza hapo akiwepo mwanafunzi mwenzetu wa darasa moja kabisa.

Happy new year 2023!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Story yako imejaa ujanja ujanja mwingi.
 
Dah
Ule msitu ulitishia sana enzi hizo
Sasa hivi hauskiki kama zamani, naona yale mauzauza yameisha.
Karibu tena njombe[emoji112]
 
Back
Top Bottom