Nilikuwa darasa la 6 siku hiyo nikarudi nyumbani baba alikuwa Dar, jioni tukasikia honi ya gari nje ya nyumba tukatoka kumpokea, siku hiyo akasema tusiguse chochote tukae mbali akashusha box kubwa 1, box la saizi yakati 1 na box kubwa zaidi 1, badae akanipa mfuko wa Rambo ambao ulikuwa na waya mrefu nikataka kuingia nao ndani akasema nikae nao pale nje, basi bwana lile box kubwa kabisa likafunguliwa lilikuwa na jenereta akaliweka nje, (hapo hata hatujasalimiana vizuri na kujuliana hali) akaweka petrol lita 10 iliyokuwa kwenye dumu jeupe, akaweka na oil ilikuwa kwenye kichupa fulani hivi, akachukua ule waya mrefu akaufungua mpaka ndani.
Kule ndani alitwambia tukae mbali tusiguse chochote, akaniambia niangalie kwenye buti kuna box nililete haraka sana, nikatoa box halikuwa zito nikalipeleka akatoa ka kitabu na vimbao na ma tairi akasoma kidogo kijitabu kisha akaunganisha vijimbao na matairi si ikatokea stand, daah tuliona mzee ni mtaalamu sana akaijaribisha pale kuiendesha nikataka namimi niisukume kidogo nikala kofi la shingo, siku mind maana nilikuwa interested kujua kitakacho fuata.
Basi bwana juu kabisa ya ile stand aliweka dubwasha kubwa lililokuwa kwenye box na lilikuwa na kioo na lina chogo, kwakuwa sikuwahi kuliona kabisa maishani sikujua ni nini, nilihisi ni kama redio hivi, pale katikati akaweka kudude flani kama redio ila chenyewe ni kidogo, akaunganisha kila kitu akatoka nje akawasha jenereta (jenereta sikulishangaa maana tulikuwa na jingine dogo kwaajili ya taa na redio siku moja moja akifurahi.
Alivyowasha akachomeka ule waya akawasha swichi kule ndani taa ikawaka kwenye extension flani hivi ya duara, akaingia huku anapiga mruzi, akatoa kasha juu lina picha ya wanyama halafu ndani ya kasha akatoa dude kama kanda ya tape ila lenyewe kubwa akasema huu ni mkanda sawa? tukasema sawa akatwambia hii ni deki na hii ni SCREEN hakusema TV alisema SCREEN sasa nikamuuliza screen kazi yake nini? akasema ngoja uone.
Akawasha akachukua remote akaset tukaanza kuona wanyama, palepale nikatoka mbio hadi nyumba yapili nikawaambia wanaitwa home wakaja familia nzima, haikutosha nikavuka nyumba kadhaa nikaenda kwa mwalimu Stive nikamwambia anaitwa nyumbani, nilienda kwa mwalimu Stive maana alikuwa anachapa sana ukichelewa namba sasa kufuta hilo nilimwalika na chaajabu walivyokuja walivutiwa sana, sikuhiyo tulikaa nao mpaka sa 7 baba akawaambia tutaendelea kesho.
Kesho yake mwalimu alinipitia na baiskeli tukaenda nae shule kiroho safi na baada ya kurudi alikuja home tukala baba alivyorudi akaenda chumbani akaileta tukaangalia, baada ya siku chache watu walikuwa wanajaa sana akawa anaitoa nje na kila siku tulikuwa tunaangalia mkanda uleule wa wanyama.
Miezi michache badaye akanunua UNGO (Dish kubwa sana la nyavu, nikubwa kweli kweli) akaja na fundi toka dar kuufunga na akazungushia fensi ya senyenge pale kwenye ungo.
Alinunua pia antena ya samaki
Ratiba ya matumizi:
Baba akisafiri hakuna kuangalia
Hakuna mtu anayeruhusiwa kugusa chochote isipokuwa kwa ruhusa yake
Ukipiga kelele au kujifanya unajua zaidi ni tiketi ya kwenda kwenu
Kwenye msiba wa Mwalimu TV yetu ilipelekwa uwanjani watu wa vijiji kadhaa wakajumuika nasi kufuatilia msiba ule na kulikuwa na bonge la nguzo lilisimikwa kwaajili ya kufunga antena.
NASIKITIKA KWAKUWA SASA ILE TV HATA KUIMILIKI NI AIBU ILA BADO NI NZIMA HADI LEO, DEKI ILIKUFA, JENERETA IPO LAKINI UMEME UPO PIA.
Enzi zile TV ilinisaidia kuwa na watoto wazuri japo tulifanya kitoto ila walikuwa madem zangu.