Sitasahau tulivyonunua TV na deki mwaka 1989, hakuna kuigusa na inalala chumbani

wewe ni miongoni mwa wachache wenye bahati sana,1989 nyumbani kuna tv?????

Sent using Jamii Forums mobile app
Lazima ulikuwa familia mambo safi, hiyo miaka kumiliki tv ni sawa na leo kuwa na gari rav4,kruger,vanguard,brevis,
miaka hiyo mtaani kwetu sinza kwa remmy karibu na makazi ya kocha wa simba abdala kibaden, kulikuwa na jamaa wawili tu Wenye TV, tulikuwa tunasmbiwa ni mabaharia, muvi za Arnold, komando joni, za kihindi tulizicheki huko ama kwa kukaribishwa sebuleni au kuchungulia dirishani.
Ushamba WA luninga uliendelea Sana mpaka 94,wakati itv na radio one zinaanza!!
Tumetoka mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio national yale ya zamani lipo kama kabati la maandazi hivi, tuning yake ni kuzungusha kama redio mkulima, picha ni black n white, baadaye yakaanza ingia makaratasi fulani unabandika mbele ya kioo kuona rangi...

Inakuwa kama ya mbao hivi!
 
Kilichonivutia kwenye hii thd ni jinsi Baba yako alivyokua na roho nzuri na utu, hakua na majivuno,aliruhusu mpaka majirani kujumuika nanyi kuangalia movie,alijitolea tv yake ili watu wafuatilie msiba wa Baba wa taifa,

Kama mshua yupo hai mpe big up sana toka kwangu,
hivyo ndivyo tunatakiwa kuishi na walimwengu,majivuno hayafai,Dunia ni mapito tu.
 
Shikamooo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu shikamoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli age ni namba tu mtu wa 89 uko shule mm sijazaliwa vizuri ila leo wooote ni familia moja humu na watu wanapendana na kutukanana pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini hata majirani wazamani walikuwa wazuri, ila wengi wasasa hawachelewi kukubebea vitu ndani
karibisha ndani kila siku uone mpaka masufuria ya jikoni yataondoka, vijiko ndiyo usiseme

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…