Sitasahau!!!


Pole sana Suzy, hakika story yako imenikumbusha mbali sana.
Nilivyokuwa nasoma nasoma nikadhan ni mimi. Mimi baba yangu mzazi alifariki kwa ajali ya gari hata darasa la kwanza nilikuwa sijaanza. Kaka yangu mkubwa ndio kwanza alikuwa darasa la saba. Na mimi ni mtoto wa nne nikifauatiwa na wawili bahati mbaya wa mwisho alifariki miaka michache baada ya kifo cha baba. Mama yangu yeye alikuwa ni mama wa nyumbani. Kwa kweli ndugu wa upande wa baba ye2 hawakutendea haki kuanzia Babu, bibi mza baba, baba wadogo na mashangazi wote kwa ujumla. Ila kabla ya kifo cha baba kweli tulipendwa sana na hao ndugu.
Ni kwamba baada ya ajali walichofanya ni kuzuia account bank, tulikuwa na gari(landlover) yenyewe ilichukuliwa na babu ye2 ikawa inamsaidia kazi zake kijijini, mashine (ya kusaga) mpya ambayo ndo kwanza ilikuwa imewasili wiki mbili kabla ya kifo cha baba, babu ye2 akasema hiyo mashine alimuagiza mwanaye(marehemu) hivyo na yenyewe ikapelekwa kijijini. Ng'ombe km 22 hivi wakachukuliwa na babu ye2 akasema aliwaweka kwa mtoto wake kwa sababu hakuwa na nafasi kijiji alikuwa na n'gombe wengi. Kwa ufupi nguo, saa, viatu vyote vya marehemu vilichukuliwa kwa kisingizio kuwa watoto bado ni wadogo mpaka wakaukue vitu vitakuwa vimeharibika. Issue ikaja kwenye nyumba, ilikuwa ni kesi kubwa sana, ilikuwa na kati ya mama na ndugu wote upande wa baba yetu. Kesi hii ilichukua miaka zaidi ya sita, nakumbuka wakati wanaenda mahakamani mama alikuwa anatuambia unaona hiyo suruali aliyovaa baba yako mdogo, saa aliyovaa babu yako, koti n.k ni vya baba yenu. Mama yangu alikonda sana, kwa kipindi hicho cha kesi walimuambia mama aende kwako na hakutakiwa akae kwenye hiyo nyumba, ila kwa sisi aliambiwa atuache hapo labda yule mtoto mdogo kabisa ndo aende naye. Kipindi hicho nilikuwa na miaka kama saba hivi, siku zote nilikuwa natembeza vitumbua kuuza, siku ya jumamosi dada yangu na kaka yangu ndo ilikuwa zamu yao kupeleka vitumbua kuuza joshoni (sehemu ya kuoshea ng'ombe). Kwa kipindi hicho chote babu ye2 alikuwa anatupumbaza kuwa amepata taarifa kutoka upande wa kina mama kuwa mama yetu amekuwa kichaa, eti anaokota vitu majararani hiyo yote ilifanyika ili tusimjue kabisa mama yetu.
Hatima ya kesi, baba zetu wadogo walihonga sana mahakamani, mwisho wa siku wakawa wameshinda kesi tukaambiwa tuhame twende kwenye nyumba za zamani( baba yetu alikuwa na nyumba mbili). Hii waliyoshinda kesi ndo ilikuwa ya kisasa zaidi. Ukifika huo mkoa (jina kapuni) ukiuliza wenyeji wa hapo wengi sana wanaielewa hii kesi ilivyotikisa kwa sababu ni mkoa mdogo na baba yetu alikuwa anafahamika sana.
Baada ya hiyo kesi ndo tuaanza sasa kukaa na mama yetu katika hiyo nyumba ya zamani, mama ndo akawa anatujenga sasa kisaikolojia kuwa sisi ni ndugu tuishi kwa kupendana. Sasa toka hapo mama ndo akawa anafanya fanya biashara tukawa tunasoma hivyo hivyo kula ikawa shida sana, siku zingine ni mlo mmoja, majirani waliokuwa wanajua mkasa wetu wakawa watusaidia pamoja na ndugu wa mama. Mungu akatujalia tukawa tunafanya vizuri kwenye masomo, tukawa tunafaulu vizuri. Shule zenyewe tulizokuwa tunafauli ni boarding ilikuwa ukienda shule unakaa huko huko hakuna kurudi nyumbani, kweli ilikuwa ni mbali sana nauli na ada ilikuwa ni issue. Mfano mimi vyeti vyangu vya A-level nimevikomboa baada ya kupata mshahara wangu wa pili mara baada kumaliza chuo hapo mlimani. Namshukuru mungu kwa kweli last year nimemaliza master's yangu huku Ulaya baada ya kupata scholaship miaka mitatu iliyopita na nafanya kitu kingine hapa kwa ajili course ingine. Huwa namshukuru sana mama yangu kwa yote na sitamuangusha kamwe kwa lolote, naamini angekuwa wa kukata tamaa angetukimbia. Nawapenda sana akina mama wote. Na huwa sipendi napoona mwanamke yoyote anapokuwa anapata tabu au kunyanyasika. Baba zetu sasa ile nyumba ndo wanagombana kila siku. Kwa kweli hata sitaki kusikia lolote toka kwako, siijui hata shilingi tano yao. Na hata nikikutana hawanikumbuki kabisa kama ni mimi maana miaka mingi kidogo imepita. Nipo naandika kitabu kwa ajili ya hii stori, mambo ni mengi sana. Basi huwa tukikutana na ndugu zangu huwa tunakumbushana ya zamani tuliyopitia kwa kweli mara nyingi ndugu upande wa baba huwa ni matatizo.

Jamani ukiona mtu anakusimulia aliyopitia unaweza kusema ya kwako ni afadhari, nimeandika kwa uchungu sana na roho yangu imetulia kwa sasa.
 

Another machozi aahhhh jamani dunia hii
 
sirgeorge

nakupa pole!!! pia nakupa hongera kwa hatua uliyofikia!!!
 

ooooh sirgeorge! Pole sana jamani.
 

Pole SIR! Dunia kweli ni tambala chakavu!
 

Hii mikasa Jamani!!!Its too bad,But Yote ni mapito na yote ni mema.To God be the Glory
 
Poleni wapendwa kwa story zenu,hayo yote ni mapito tu MUNGU AWAJAZE NGUVU.
 
u strong enough to share this story with us...pole sanaaa.daima mungu yupo na wewee.TUWAPENDE YATIMAAAA
 


Pole sana George, hawa ndo binadamu. Daima huwezi furahia mali ya dhuluma kwani kuna damu inaililia haki yako. Ila wasamehe na waombee kwa Mungu.
 
Very touching story! Poleni sana kwa yote.
Mwenyezi Mungu ni mwema sana na muweza wa yote. Ndio maana Waswahili wakasema aliye juu mngoje chini; yametimia.
Mafunzo kwetu ni kuwa tusiwe wenye kuwanyanyasa waja wa Mwenyezi Mungu kwani kesho ipo!
 
Pole sana Suzy
endelea kuamini Mungu yupo maana amekupigania sana!
 
Pole Dada yetu!!!!, PLiz FORGIVE but dont FORGET!!!, Ni mitihani ya mwenyezi Mungu, na ukipita huwa analo zuri atakupa/keshakupa.
 
Poleni wote mliotendwa na hii dunia. Hakika Mungu atawafuta machozi wote...
 
Poleni sana kila mtu ana mikasa katika maisha yaani acheni tu.

Nikiandika yalionikumba Mungu tu pekee anajua ni maumivu makubwa mpka dakika hii nikikumbuka huwa sipo okay... Mungu ni muweza wa yote

RIP waliotutangulia
 
niliapa kuwa sitawasamehe hasa yule wifi yangu, ila leo Mungu amenifundisha kusamehe!!! nawapenda sana! najua dhahabu safi lazima ipite kwenye moto!!

Walau umejifunza upendo ni kitu gani Susy
 
Poleni sana kila mtu ana mikasa katika maisha yaani acheni tu.

Nikiandika yalionikumba Mungu tu pekee anajua ni maumivu makubwa mpka dakika hii nikikumbuka huwa sipo okay... Mungu ni muweza wa yote

RIP waliotutangulia

Yaani we acha tu halafu wanaotesa watoto sio wengine ni ndugu wa damu
 
Bwana ndiye mchungaji wangu,sitapungukiwa na kitu,katika malisho ya majani mabichi hunilaza,kando ya maji ya utulivu huniongoza, hunihuisha nafsi yangu;na kuniongozakatika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naamu,nijapopita kati ya bonde la uvuli na mauti,sitaogopa mabaya;kwa maana wewe upo pamoja nami,gongo lako na fimbo yako vyanifariji,waandaa meza mbele yangu,machoni pa watesi wangu,umenipaka mafuta kichwani pangu,na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zanifuata siku zote za maisha yangu;nami nitakaa nyumbani kwa BWANA milele
 

Pole sana. Mshukuru Mungu kwa kuwawezesha kuyashinda majaribu. Katika stori zote hizi zimenikumbusha wimbo wa Msondo Ngoma unaosema KWENYE MSIBA WA FUKARA MAMBO HUWA SHWARI, LAKINI KWA MWENYE MALI NI MATATIZO. Ukitaka kujua ndugu zako na hata marafiki zako wa ukweli ni pale unapokuwa kwenye matatizo!!
 
My Dia Susy, Nilifikiri ni mimi peke yangu nimepitia haya.
U have the story lyk mine lakini mimi Baba alinitosa baada ya Mama kufariki nikiwa darasa la 1!!!
Sasa hivi maisha yamemfunza anakuja kuomba msaada kwangu na ndugu walionitesa wanaomba msaada.

MUNGU YU MWEMA kwa kila mtu!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…