Asalam aleikum!!!
Bwana Yesu asifiwe!!
Nimesoma thread ya Lizy kuhusu unyanyasaji wa watoto ikanikumbusha mbali sana, hakika imenitoa machozi!!
Nakumbuka miaka ya nyuma sana wakati nikiwa na miaka 4 tu, mama yangu alifariki kwa ugonjwa wa cancer, hatukukaa hata mwaka baba naye alifariki na ugonjwa wa figo, hapo ndipo nilipotamani dunia igeuke chini juu.
Nakumbuka dada yangu mkubwa alikuwa ndio kwanza yupo 4m3 na kaka yangu ambaye nafatana naye alikua yupo darasa la pili, tulinyang'anywa mali zote za baba yetu, tena tukarudishwa kijijini kabisa ambapo baba aliweka mifugo yake, baada ya muda bb mdg akaja akachukua ngombe wote wakagawana na watoto wa mama mkubwa.
Hakuna aliyetujali, tuliachiwa mbuzi tu pale kijijini, nakumbuka kaka yangu ilibidi aache shule aanze kuchunga hao mbuzi kwa taabu, mimi nilikua nachota maji na kufagia, hakuna aliyejua tunakula nini, tunavaa nini wala tunalala vipi. Dada yangu alichukuliwa na dada mtoto wa mm mkubwa na kugeuzwa house girl.
Nakumbuka wale rafikize baba walipoona hivyo, wakamlipia dada yangu ada tena kwa kuchangiwa na kijiji dada akarudi shule, jirani yetu mmoja akasema tuchanganye mbuzi zetu na zake ili kaka asiende kuchunga tena awe anaenda shule.
kutokana na baridi ya mkoa ambao tulikuwepo, na hatukuwa na blanket siku moja nilishikwa na naimonia ikiambatana na homa kali, yule bb mkubwa rafikiye baba akamtuma kaka yangu aende kwa ba-mdogo akamweleze, kaka yangu akapanda gari kwenda mjini kumwambia baba mdogo, baba mdogo akamwambia kama baba yake na mama yake wamekufa yeye anafaida gani, mwache afe akupunguzieni taabu!! kaka alirudi kijijini na kuomba msaada kwa yule rafiki yake na baba (ba-mkubwa) ndipo nikapelekwa hospitali na kulazwa, ikimlazimu kufanya vibarua vya kulima wakati akiwa mdogo ili kutupatia fedha za matumizi na kuniuguza.
kaka yangu mtoto wa m.mkubwa akaoa kule kijijini akatuchukua lakini niliona bora tulivyokuwa tunakaa wenyewe maana wifi alitunyanyasa sana, jina langu lilibadilika ghafla, nikawa naitwa mbwa, nakumbuka alikua ananiita hivi, "we mbwa mkubwa njoo hapa" ukifika tu unakutana na kibao kizito alafu ndio maagizo mengine yanafuatia!!!
Baada ya muda, wale wote waliotudhulumu alikufa mmoja baada ya mwingine, wale waliotunyanyasa kwa chakula leo ndio wanatuomba chakula, waliotulaza chini leo wanatembea wameinamisha vichwa vyao!!
"usimnyanyase yatima wala kumuonea mjane, mkono wa Mungu utakuwa juu yako"
Pole sana Suzy, hakika story yako imenikumbusha mbali sana.
Nilivyokuwa nasoma nasoma nikadhan ni mimi. Mimi baba yangu mzazi alifariki kwa ajali ya gari hata darasa la kwanza nilikuwa sijaanza. Kaka yangu mkubwa ndio kwanza alikuwa darasa la saba. Na mimi ni mtoto wa nne nikifauatiwa na wawili bahati mbaya wa mwisho alifariki miaka michache baada ya kifo cha baba. Mama yangu yeye alikuwa ni mama wa nyumbani. Kwa kweli ndugu wa upande wa baba ye2 hawakutendea haki kuanzia Babu, bibi mza baba, baba wadogo na mashangazi wote kwa ujumla. Ila kabla ya kifo cha baba kweli tulipendwa sana na hao ndugu.
Ni kwamba baada ya ajali walichofanya ni kuzuia account bank, tulikuwa na gari(landlover) yenyewe ilichukuliwa na babu ye2 ikawa inamsaidia kazi zake kijijini, mashine (ya kusaga) mpya ambayo ndo kwanza ilikuwa imewasili wiki mbili kabla ya kifo cha baba, babu ye2 akasema hiyo mashine alimuagiza mwanaye(marehemu) hivyo na yenyewe ikapelekwa kijijini. Ng'ombe km 22 hivi wakachukuliwa na babu ye2 akasema aliwaweka kwa mtoto wake kwa sababu hakuwa na nafasi kijiji alikuwa na n'gombe wengi. Kwa ufupi nguo, saa, viatu vyote vya marehemu vilichukuliwa kwa kisingizio kuwa watoto bado ni wadogo mpaka wakaukue vitu vitakuwa vimeharibika. Issue ikaja kwenye nyumba, ilikuwa ni kesi kubwa sana, ilikuwa na kati ya mama na ndugu wote upande wa baba yetu. Kesi hii ilichukua miaka zaidi ya sita, nakumbuka wakati wanaenda mahakamani mama alikuwa anatuambia unaona hiyo suruali aliyovaa baba yako mdogo, saa aliyovaa babu yako, koti n.k ni vya baba yenu. Mama yangu alikonda sana, kwa kipindi hicho cha kesi walimuambia mama aende kwako na hakutakiwa akae kwenye hiyo nyumba, ila kwa sisi aliambiwa atuache hapo labda yule mtoto mdogo kabisa ndo aende naye. Kipindi hicho nilikuwa na miaka kama saba hivi, siku zote nilikuwa natembeza vitumbua kuuza, siku ya jumamosi dada yangu na kaka yangu ndo ilikuwa zamu yao kupeleka vitumbua kuuza joshoni (sehemu ya kuoshea ng'ombe). Kwa kipindi hicho chote babu ye2 alikuwa anatupumbaza kuwa amepata taarifa kutoka upande wa kina mama kuwa mama yetu amekuwa kichaa, eti anaokota vitu majararani hiyo yote ilifanyika ili tusimjue kabisa mama yetu.
Hatima ya kesi, baba zetu wadogo walihonga sana mahakamani, mwisho wa siku wakawa wameshinda kesi tukaambiwa tuhame twende kwenye nyumba za zamani( baba yetu alikuwa na nyumba mbili). Hii waliyoshinda kesi ndo ilikuwa ya kisasa zaidi. Ukifika huo mkoa (jina kapuni) ukiuliza wenyeji wa hapo wengi sana wanaielewa hii kesi ilivyotikisa kwa sababu ni mkoa mdogo na baba yetu alikuwa anafahamika sana.
Baada ya hiyo kesi ndo tuaanza sasa kukaa na mama yetu katika hiyo nyumba ya zamani, mama ndo akawa anatujenga sasa kisaikolojia kuwa sisi ni ndugu tuishi kwa kupendana. Sasa toka hapo mama ndo akawa anafanya fanya biashara tukawa tunasoma hivyo hivyo kula ikawa shida sana, siku zingine ni mlo mmoja, majirani waliokuwa wanajua mkasa wetu wakawa watusaidia pamoja na ndugu wa mama. Mungu akatujalia tukawa tunafanya vizuri kwenye masomo, tukawa tunafaulu vizuri. Shule zenyewe tulizokuwa tunafauli ni boarding ilikuwa ukienda shule unakaa huko huko hakuna kurudi nyumbani, kweli ilikuwa ni mbali sana nauli na ada ilikuwa ni issue. Mfano mimi vyeti vyangu vya A-level nimevikomboa baada ya kupata mshahara wangu wa pili mara baada kumaliza chuo hapo mlimani. Namshukuru mungu kwa kweli last year nimemaliza master's yangu huku Ulaya baada ya kupata scholaship miaka mitatu iliyopita na nafanya kitu kingine hapa kwa ajili course ingine. Huwa namshukuru sana mama yangu kwa yote na sitamuangusha kamwe kwa lolote, naamini angekuwa wa kukata tamaa angetukimbia. Nawapenda sana akina mama wote. Na huwa sipendi napoona mwanamke yoyote anapokuwa anapata tabu au kunyanyasika. Baba zetu sasa ile nyumba ndo wanagombana kila siku. Kwa kweli hata sitaki kusikia lolote toka kwako, siijui hata shilingi tano yao. Na hata nikikutana hawanikumbuki kabisa kama ni mimi maana miaka mingi kidogo imepita. Nipo naandika kitabu kwa ajili ya hii stori, mambo ni mengi sana. Basi huwa tukikutana na ndugu zangu huwa tunakumbushana ya zamani tuliyopitia kwa kweli mara nyingi ndugu upande wa baba huwa ni matatizo.
Jamani ukiona mtu anakusimulia aliyopitia unaweza kusema ya kwako ni afadhari, nimeandika kwa uchungu sana na roho yangu imetulia kwa sasa.