Sitasahau!!!

Sitasahau!!!

Amanda

thanks my dia!!
 
PAS,niwaellyester1,Derimto!!

nawashukuru wote kwa kunitia moyo!!!
 
dada pole sana kwa hayo mambo uliyopitia lakini yote ni mipango ya mungu ila usipende kuikumbushia historia yako maana hautakua na roho ya kusamehe cha msingi samehe hayo yote alafu tunaomba utueleze ni jinsi gan ulivyo fanikiwa...
 
Mwantui nitawaeleza usijali!!
 
Oh! Mungu wangu........................imenipelekea roho ya maombi - yes ngoja mchana wa leo niwaombee Yatima wote na Wajane wote -

Kumbuka kuwa: WATU WOTE AMBAO MUNGU AMEWAINUA PANAPO NAFASI - WAMEPITIA MAGUMU MENGI - IWE MANYANYASO, MAGONJWA ETC. MSHUKURU MUNGU - WEWE NI MMOJA WAPO NA MUNGU ATAKUINUA ZAIDI YA HAPO - ENDELEA KUFANYA KAZI YA MUNGU, JENGA KITUO CHA YATIMA NA MUNGU AKUPE MAONO YA KUFANYA MAMBO MENGINE MAGUBWA. KAMA ALIVYOKUFUTA MACHOZI WEWE - AKUTUMIE KUWAFUTA WENGINE MACHOZI.

KAMA UTAWEZA - ANDIKA KITABU KIDOGO - MWANZO WA MANYANYASO HADI MUNGU ALIVYOKUTOA - KITAWAJENGA WENGI WANAOPITIA MAJARIBU - KUWA TUNAYE MUNGU ANAYE WINUA WANYONGE TOKA JALALANI NA KUWAKETISHA PAMOJA NA WAKUBWA.

MUNGU AKUBARIKI SANA SUSY.
 
  • Thanks
Reactions: LD
yatima, nimekupata, tupo katika harakati hizo za kujenga kituo.
 
Pole sana tena sana. tuambie umefikaje hapa ulipofika? natamani kuendelea kuijua stori hii ili endeleaje?
 
Pole sana Suzy kwa yote, ila katika yote God has never left you. He wanted you to learn something and am sure through all the struggles God has been Merciful and graceful to you and your siblings.

The Bible tells us to be thankful at all times no matter what the situation we have to thank Him. By doing so He will stretch fourth His hand and bless you with his riches.

One thing do not have a heart of vengeance treat all who did you wrong with kindness, that will be your vengeance to them.
 
LD namshukuru Mungu kwa sasa tunajenga kituo cha watoto yatima kule kibamba!! hatuwezi kusahau!!
Kwanza poleni sana dada na masahibu yote yaliyowafika, na namshukuru Mungu kuwa hatimaye mmenyanyuka na kusonga mbele.. Kwa kweli mmeobarikiwa, kwani wanyanyasaji wengi ni wale walionyanyaswa udogoni wanapokuwa wakubwa wanalipa visasi. Kwa hiyo nyinyi Mungu kuwajaalieni uwezo kidogo na kuwakumbuka mayatima hiyo ni baraka kubwa. Endeleeni na Mungu atawasaidieni zaidi na zaidi.
Mungu Asifiwe

Pili, hongera sana kwa kupata ujasiri wa kuiweka hii mada hapa. Naamini wapo wengi waliopitia mateso na manyanyaso kama yenu.
 
MAMMAMIA

nakushukuru my dia!!
 
KAMA UTAWEZA - ANDIKA KITABU KIDOGO - MWANZO WA MANYANYASO HADI MUNGU ALIVYOKUTOA - KITAWAJENGA WENGI WANAOPITIA MAJARIBU - KUWA TUNAYE MUNGU ANAYE WINUA WANYONGE TOKA JALALANI NA KUWAKETISHA PAMOJA NA WAKUBWA.

MUNGU AKUBARIKI SANA SUSY.[/COLOR][/B][/QUOTE]

YATIMA, mawazo yako mazuri sana. Nilikuwa na wazo kama hili lakini badala ya kutoka kwa mtu mmoja tu, kikawa ni "testimonials" za wengi. Tayri jana tulisikia ya Lizy, leo za Sussy na wengineo, na naamini tupo wengi ambao ama yametufika moja kwa moja au ndugu, jamaa na majirani zetu. Ni wazo langu tu, tusubiri mawazo ya wengine.
 
lakini bado mnasema akina mama ni watu wenye huruma. Ukweli ni kwamba akina mama wengi wapo kama huyo wifi yako

Mimi sifikiri hivyo, angalau +90% ya mama zetu si kama huyu wifi, tatizo ni kuwa hao kidogo wanaofanya hivyo matendo yao yanaonekana wazi zaidi kuliko mema wanayofanya wengine. Na hii ndio kawaida ya binadamu; mtu anaweza kutenda mema sehemu kubwa ya maisha yake lakini wema wote ukafunikwa tendo moja tu la uovu ikiwa tendo hilo ni la kukusudia au la nia mbaya. Lakini Mungu ana uwezo wa kulainisha roho zao. Tuwaombee!
 
Pole mama, samehe na sahau yooote yaliyopita, tugange yajayo.
Katika maisha yako, tenda mema wakati wote na Mwenyezi Mungu atakubariki
 
Mungu ni mkuu hakuna linaloshindikana kwake. Wasamehe wote walio kukwaza kwa njia moja au nyingine kwa sababu mungu amekuinua kutoka kwenye unyonge. Kumbuka adui yako ni adui wa mungu mwachie mungu apambane nae, mungu amesema mpende adui yako, wewe wasamehe then utaona baraka za mungu zitakavyo kushukia. Mimi baba alifariki nikiwa darasa la saba nilipitia changamoto nyingi ila nilimtumaini mungu bila kuwa na kinyongo na mtu yeyote leo hii ni mtu mwenye thamani mbele ya jamii inayo ni zunguka. Nimefurahi sana ushuhuda wako, mungu anapo tubariki ni lizama tusimame na kushuhudia ili kila mwanadamu ajue mungu tunaye mwabudu ni mwema siku zote. Mungu akubariki na akupe roho ya kusamehe ili neema na baraka zake ziendeleekuwa juu yako.
 
  • Thanks
Reactions: LD
Pole sana mpendwa Mungu ni mkubwa afadhali umepata na muda wa kutoa ushuhuda, wapo humuhumu wanaotesa watoto wa wenzao watasoma watapata ujumbe fulani hata unaweza ukawabadilisha watu. Uwe na amani
 
Susy kuna wimbo naupenda sana bila shaka unaujua;

Muombee adui yako aishi siku nyingi............Asije akafa kabla hajaona baraka ambazo Mungu ameweka juu yako. Kwa yanayokutokea ni Mungu anadhihirisha uumbaji wake. Na ww unapaswa kumtukuza na kumsifu maana amekuinua toka kwa watesi wako. Ni watu wengi wamepitia mambo mengi sana, lakini Mungu ni mwaminifu na anawapigania kila siku.[/QUOTE]

Last edited by a moderator:
Mungu ni mkuu hakuna linaloshindikana kwake. Wasamehe wote walio kukwaza kwa njia moja au nyingine kwa sababu mungu amekuinua kutoka kwenye unyonge. Kumbuka adui yako ni adui wa mungu mwachie mungu apambane nae, mungu amesema mpende adui yako, wewe wasamehe then utaona baraka za mungu zitakavyo kushukia. Mimi baba alifariki nikiwa darasa la saba nilipitia changamoto nyingi ila nilimtumaini mungu bila kuwa na kinyongo na mtu yeyote leo hii ni mtu mwenye thamani mbele ya jamii inayo ni zunguka. Nimefurahi sana ushuhuda wako, mungu anapo tubariki ni lizama tusimame na kushuhudia ili kila mwanadamu ajue mungu tunaye mwabudu ni mwema siku zote. Mungu akubariki na akupe roho ya kusamehe ili neema na baraka zake ziendeleekuwa juu yako.

Last edited by a moderator:
LD nakushukuru sana, nimesikiliza nyimbo zako!!!! zinatia moyo sana!! thanks my dia!
 
Pole sana mpendwa Mungu ni mkubwa afadhali umepata na muda wa kutoa ushuhuda, wapo humuhumu wanaotesa watoto wa wenzao watasoma watapata ujumbe fulani hata unaweza ukawabadilisha watu. Uwe na amani

ukimshuhudia Mungu anakuinua zaidi!!
 
Back
Top Bottom