Sitasahau

Sitasahau

primolut N

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2018
Posts
391
Reaction score
316
Nilipoyaanzisha kama na huyu binti.
Tarehe 11 mwezi novemba 2017 nikiwa ndo naanza muhula wangu wa mwisho pale chuoni.
Mdogomdogo tukaenda mpaka nikajua ndo mke wa ndoa. Kumbe tapeli tu na Mganga njaa?
Mpaka nikataka nimtambulishe nyumbani lakini nikasita.
Nikapata matatizo hakujali
Lakini nashukuru sana kanifundisha mno.

Kiuhalisia kwao in Mwanza. Kaja Moro kwa ajili ya Masomo.
Tukakutana chuoni.
Basis hio asubuhi nikiwa mimedoji kwenda kwenye clinical meeting nimekaa. Basi akaja mpaka pale nilipoketi kwa ajili ya kutaka kufaham mawili matatu kutoka kwa mkongwe Mimi. Basi baada ya salamu akajitambulisha nami pia nikajitambulisha kwake.
Tukakubaliana jioni tukutane tupeane uzoefu wa namna yeye atakavyokabili chuo.
Lakini siku hip ikashindikana na siku nyingine tena ikashindikana na tena na tena.
Ilikuwa ijumaa nikamtembelea kwake nikapiga nae stori sana na mwisho nikaingiza wazo langu la kuwa nampenda.
Hakujibu lolote zaidi ya kuniambia kuwa hataki kuingia kwenye mapenzi tena kwa sababu alikuwa na mpenzi akamuumiza sana.
Kama kawaida ni vigumu kumkuta mwanaume anakubali kumkosa demu kwa sababu ndogo kama hio.
Kesho nikamchukua tena kwenda kuongea nae lakini aliishia kulia na Mimi nikamruhusu aondoke.
Siku nikambushia akaniambia haiwezekani basi nikamwacha kumfuatilia nikendelea na maisha yangu kama kawaida.
Roommate akaniomba nimpime ujauzito kwa ikanilazimu kwenda chumbani kwao tena.
Ile nafika nikamkuta ni mgonjwa anaharisha akahitaji nimsaidie.
Nikatafuta flagyl lakini akasema bila limao hawezi meza ikabidi usiku huo na umeme umekata nukahangaike kwenye miti ya limao.
Nikafanikiwa kupata mbili tatu hivi kumchukulia soda na maji kwa gharama zangu.
Nikamsimamia ikiwa in pamija na kumlazimisha ameze zile dawa usiku huo alafu nikaenda kulala.
Kesho take akaenda darasani kama kawaida
Baada ya kama siku mbili akagua UTI ikabidi nimhudumie tena kwa gharama zangu.
Ikawa ndo maisha jioni anatka nimwagizie msosi hata mchana wakati huo sisi sote ni wanafunzi.
Nikaja kupata kashkash Fulani na polisi hivi wala hakuwahi kuja kutia mguu wake.
Like nikalimaliza nikamuuliza vipi mbona hukuja kuniona? ananiambia
Nipotezee.
Kwelii Nikapotezea.


Dah! Aisee!!
 
Nilipoyaanzisha kama na huyu binti.
Tarehe 11 mwezi novemba 2017 nikiwa ndo naanza muhula wangu wa mwisho pale chuoni.
Mdogomdogo tukaenda mpaka nikajua ndo mke wa ndoa. Kumbe tapeli tu na Mganga njaa?
Mpaka nikataka nimtambulishe nyumbani lakini nikasita.
Nikapata matatizo hakujali
Lakini nashukuru sana kanifundisha mno.
Matatizo ya kuandikia thread chooni
 
Maumivu yakiisha rudi... Hata Biblia iliagiza tuishi nao kwa jicho la tatu.
 
Hahahahahhahahaaahahahahahahaaaaaaaa⇧⇧⇧⇧⇧⇧⇧⇧⇧⇧⇧
 
Bila shaka story haijaisha..halafu mkuu MTU umekutana nae November 2017 na akakuzungusha kukubali ....na sasa n February 2018 so uhusiano hauzid miez 3 tayari ulikua unataka kwenda kumtambulisha!...nasubir part 2!
 
Yaani huyu jamaa ndo maana aliahirisha clinical meeting


Hata kuclark wagonjwa ni shida

Teh
 
Bila kumalizia story yako inaonesha demu alikuchapa vijisent vingi sana
 
Back
Top Bottom