SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Mbumbumbu wa Rage ni wale walioleta vipengele. Uzi huu umejaa vipengele vilivyoletwa na Uto.Kwani
Wasio na akili ni mbumbumbu wa Rage walikimbia mechi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbumbumbu wa Rage ni wale walioleta vipengele. Uzi huu umejaa vipengele vilivyoletwa na Uto.Kwani
Wasio na akili ni mbumbumbu wa Rage walikimbia mechi
Mimi ni shabiki wa Simba.Binafsi nitakuwa mtu wa nwisho kuamini eti sababu ya simba kususia mechi, na pia bodi ya ligi kuwaunga mkono; ilikuwa ni kuzuiliwa kuingia uwanjani na makomandoo wa Yanga!
Tena wakifika uwanjani bila ya kutoa taarifa kwa mtu yeyote yule! Eti tu kwa sababu ni haki yao kufanya mazoezi hapo uwanjani, siku moja kabla ya mechi!!
Hapa kulikuwa kuna sababu mbili za msingi! Kutengeneza tukio la kuonesha wamezuiliwa ili wasusie mechi, au kutaka kuingia ili kufanya vitendo vya kishirikina, na ambavyo havikubaliki kwenye mpira wa miguu! Full stop.
Umenichekesha sana 🤣Ile barua mlioindikia caf kuhusi goli mlilonyimwa dhidi ya mamelodi mlijibiwa?
Anyway wenye akili ni wawili tu upande huo
Kanuni sheria ya kuhairisha mcezo kanuni kipengere cha 3:1Kanuni Gani ilifuatwa?
Hoja zipi kiazi wewe...kwq mtu mwenye akili timamu hakuna hoja ambayo Bodi ya ligi na ukoloni mnaweza kuzitoa. Mechi ilikuwa planed kuhairishwa ndio maana simba akatoa barua!!.Wajinga wa aina yako ndio mtaji mkubwa wa chama tawala nchini.
Ukisoma content nzima imeandikwa kwanza kishabiki na imeegemea upande mmoja..ushabiki maandazi unaharibu vichwa Hadi thinking capacity inakua ni ndogo mno...
Nilitamani nikujibu kwa hoja ila naona hapa ntakua najisumbua Bure kumuelimisha mjinga/shabiki oyaoya.
Kuna mambo ya msingi unayasahau.Fifa na Cas hawana muda huo wa kupoteza kuchunguza na ripoti ya bodi ya ligi ipo sasa wachunguze nini?
Kwaakili zenu kabisa mnaamini Fifa waache kuamini bodi ya ligi ya Tanzania na TFF yenye weledi na viongozi bora badala yake iamini klabu yenye kesi lukuki huko Fifa za kutaka kudhulumu wachezaji haki zao karibia kila mwaka na kesi mpya si chini ya 6
Yanga na viongozi wake ni watu wasiojua sheria kabisa lakini ni ajabu kila wakiguswa hukimbilia sheria matokeo yake hudhalilika kila mara.
Imekuwa kawaida sasa kila mwaka lazima kuwe na kesi angalau mbili za Yanga za kuchekesha na watakazoishia kushindwa tu na kudhalilika
Yanga acheni kupoteza gharama zenu na muda Fifa haiwezi kusikiliza matapeli kuweni watiifu kwa bodi msubiri tar ya mchezo na kama mnabisha tupo hapa tutakumbushana
Tamko lao la awali waliposema mechi iko palepale liliwaingiza watu chaka zaidi kama LBL. Bodi ya ligi ni matapeli wanaoangalia maslahi yao wenyewe na washirika wao. Huenda Wasingetoa tamko mapema asubuhi kuwaaminisha watu mechi ipo kuna ghalama nyingi zingeepukwa.Bodi ya Ligi walifanya uamuzi wa kipuuzi kabisa. Swali ni je, nini kiliwasukuma kufanya maamuzi yale? Kanuni gani na sababu zipi ziliwapa uhalali wa kuahirisha mechi iliyokuwa imebakiza masaa tu ianze?Kulikuwa na udharura gani au sababu ipi yenye uzito wa kiwango hicho?
Na kinachofurahisha zaidi mechi ya mzunguko wa kwanza, Yanga hakuruhusiwa kufanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea kwenye ile mechi! Wakachukulia kama ni jambo la kawaida. Ila ilipotokea kwa simba, moja kwa moja wakatangaza kususia mechi, na bodi ya ligi nayo ikawaunga mkono.Mimi ni shabiki wa Simba.
Kilichotokea ni Simba tumezingua ila kwa kuwa watu wamejawa mapenzi ya timu wanaona waipambanie kwa namna yoyote hata kama timu imekosea.
Kisheria, haki inatekelezwa kwa njia ya haki na busara, na kuna matarajio ya kawaida kwamba pande zote husika zitahusiana kwa njia inayowezesha utekelezaji wa haki hiyo.
Halikadhalika, sheria haitumiki kwa namna ya kulazimisha upande mmoja kushindwa kwa sababu ya makosa ambayo ungeweza kuepuka.
Simba anajua fika kuwa mpinzani anatakiwa kukuandalia mazingira ya uwanja lakini yeye (Simba) hakuchukua hatua yoyote kuhakikisha hilo linafanyika.
Madai ya Simba hayana mashiko na ni kwa sababu, unaweza kushindwa kudai kuwa hukutimiziwa haki yako kwa sababu hukufuata taratibu muhimu na za kawaida za kuhakikisha haki yako inatekelezwa. Kwa hili Simba wamefeli kwa sababu misingi ya haki huwa inaangalia na usawa.
Simba kusema kwamba ni takwa la kanuni ni haki yao bado hoja yao ni mufulisi: Kwa mfano, una haki ya kutoa maoni ama kujielezea lakini huwezi kuitumia kwa kuvunjia heshima wengine hata kama hakuna utaratibu maalumu uliyowekwa. Utekelezaji wa haki unapaswa kwenda sambamba na kanuni za kijamii pia.
Kimsingi, Simba kukataa kucheza mechi ni madai dhaifu sana kwa kuwa yeye mwenyewe hakufanya juhudi yoyote kuhakikisha haki yake inatimizwa. Kisheria, haki yako huwezi kuifuata kiholela bila kufuata utaratibu, hata kama sheria hizo haizjaeleza hizo taratibu moja kwa moja.
Njia sahihi, Simba walitakiwa kuwasiliana na Yanga ili haki yao kikanuni iweze kutekelezwa na taarifa hiyo ingewafikia wasimamizi wa uwanja ili kuhakikisha haki yao inatekelezwa ipasavyo.
Hitimisho:Wakosefu hapa ni Simba na viongozi wa bodi ya Ligi. Hili suala Yanga wakilivalia njuga na kulifikisha juu ni baya sana kwa Simba, bodi ya ligi na TFF kwa ujumla. Vilevile ligi yetu itashuka hadhi. Ni busara za Yanga tu ndizo zitakazoamua hili suala liishe vyema.
Umeandika maandishi mengi lakini inaonesha hujui mazingira halisi yaliyokuwepo.Ni kweli Simba hawakuwasiliana na Yanga na viongozi wa uwanja, lakini walipofika uwanjani meneja uwanja alipigiwa simu na kufika,aliwafungulia geti lakini makomandoo wa Yanga waliwazuia na kuleta vurugu.Hili la vurugu si wewe wala viongozi wa Yanga wanalizungumzia, lakini kwenye ripoti ya bodi wameliweka kwa kupokea ripoti ya Afisa Usalama wa mechi,hiyo pia wametaja kuwa ni sababu ya kuahirisha mechi na si Simba kushindwa kufanya mazoezi.Wametumia kanuni ya 34:1(1.3) inayowapa mamlaka ya kuahirisha mechi.Huyu hapa mmoja wa mabaunsa wa Yanga anakiri waliwazuia SimbaKuna mambo ya msingi unayasahau.
Katika muktadha wa kisheria, haki si jambo la kutekelezwa kiholela bali linahitaji kufuata taratibu maalumu ili kuhakikisha linatendeka kwa usawa na haki.
Hii ina maana kwamba, hata kama sheria inakupa haki fulani, utekelezaji wake unapaswa kufuata utaratibu wa busara unaoeleweka katika mazingira husika.
Katika mfumo wa haki kuna misingi ya mawasiliano na ushirikiano wa pande zote zinazohusika. Sheria inatambua utaratibu wa mawasiliano na unaheshimiwa.
Kwa mfano, kanuni inamtaka Yanga amwandalie Simba kabla ya mechi ili aiangalie pitch na sababu nyenginezo zinavyoeleza.
Simba kuja bila taarifa hapo uwanjani kisheria hoja yake inabaki kuwa ni dhaifu na ni kwa sababu sheria inatambua utaratibu wa mawasiliano na unaheshimiwa. Yaani, Simba alifanya jitihada yoyote ya mawasiliano ili hilo litimizwe?
Ikiwa kama Simba haikufanya hivyo na ikadai yeye amefuata kanuni kama inavyoelekeza bado sheria itamtupa mkono kwa sababu, haki haiwezi kutekelezwa nje ya utaratibu.
Yaani, sheria imempa Simba haki fulani, lakini sheria inataka utekelezaji wake unapaswa kufuata utaratibu wa busara unaoeleweka katika mazingira husika. Kwa nini? Kwa sababu, katika muktadha wa kisheria, haki si jambo la kutekelezwa kiholela bali linahitaji kufuata taratibu maalumu ili kuhakikisha linatendeka kwa usawa na haki.
Kwa nini kwa usawa na haki? Sheria haitumiki kwa namna ya kulazimisha upande mmoja kushindwa kwa sababu ya makosa ambayo ungeweza kuepuka. Huwezi ukaja ghafla tu ukiwa hujatoa taarifa, kisha ukadai kuwa umenyimwa haki yako. Sheria pia hutegemea na nia njema na busara pia.
Ukija kwenye hoja ya kughairisha mechi, kwa kuwa Simba ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa tamko, Je, kuna kifungu chochote ambacho kinalinda dai lake awali na kufanya kuighairishwa kwa mechi? Jawabu ni hakuna!
Pengine inaweza kutoka hoja nyengine kuwa Simba si aliyeghairisha mechi, bali ni bodi ya ligi.
Ikiwa hali ni ya namna hii na yakifanyika marejeo ya asili ya madai ya Simba na kwa kuwa hakuna madai ya msingi kisheria kwa Simba kususia mechi kuna mambo yataibuka nayo ni bodi ya ligi au mamlaka ya mpira inamlinda badala ya kuchukua hatua stahiki.
Mazingira haya yanaweza kisheria kuitwa willful blindness yaani kufumbia macho ukiukwaji wa kisheria.
Katika muktadha wa mpira wa miguu hali hii inaweza kuangukia kwenye makosa yafuatayo:
1) Upendeleo wa wazi (Bias/Favoritism)
Yaani bodi ya ligi inamlinda mhusika badala ya kuhakikisha sheria na kanuni zinaheshimiwa (zinafuatwa bila upendeleo).
2)Rushwa au mgongano wa maslahi (Corruption/Conflict of interest)
Yaani, bodi ya ligi inamlinda mhusika kwa sababu ya maslahi fulani binafsi au kuwa na ukosefu wa dosari za kimaadili (rushwa)
Na sababu nyenginezo zinaweza kuwekwa na wengineo!
Mimi ni shabiki wa Simba, lakini hili suala ukiliangalia kisheria na hata kimuktadha wa sheria za mpira wa miguu madai ya Simba ni dhaifu. Ikiwa kama Yanga wakilivalia kidete na kulipeleka mamlaka za juu kabisa za mpira Simba lazima rungu lishuke kwake!
Si Simba tu, bali bodi ya ligi nayo pia. Ikiwa TFF ikashindwa kusimamia ipasavyo na kisha Yanga ikaamua kulipeleka ngazi za juu kama Uzi zitende haki hilo rungu litaathiri mpaka ligi yetu, mfano halisi ligi ya Italia rungu walilopigwa, kwa sababu Simba itaashibiwa na TFF itaadhibiwa pia na ligi yetu itakuwa mashakani.
Ni busara za Yanga pekee ndiyo zitakazoinusu ligi yetu.
Wachunguzwe huenda wamelambishwa asali.Tamko lao la awali waliposema mechi iko palepale liliwaingiza watu chaka zaidi kama LBL. Bodi ya ligi ni matapeli wanaoangalia maslahi yao wenyewe na washirika wao. Huenda Wasingetoa tamko mapema asubuhi kuwaaminisha watu mechi ipo kuna ghalama nyingi zingeepukwa.
Lakini kwa vyovyote vile walishiriki kuvuruga kanuni.
Shida ipo hapo kwenye kuchunguzwaWachunguzwe huenda wamelambishwa asali.
Ambapo hatuelewani ndugu ni sehemu ndogo sana.Kuna mambo ya msingi unayasahau.
Katika muktadha wa kisheria, haki si jambo la kutekelezwa kiholela bali linahitaji kufuata taratibu maalumu ili kuhakikisha linatendeka kwa usawa na haki.
Hii ina maana kwamba, hata kama sheria inakupa haki fulani, utekelezaji wake unapaswa kufuata utaratibu wa busara unaoeleweka katika mazingira husika.
Katika mfumo wa haki kuna misingi ya mawasiliano na ushirikiano wa pande zote zinazohusika. Sheria inatambua utaratibu wa mawasiliano na unaheshimiwa.
Kwa mfano, kanuni inamtaka Yanga amwandalie Simba kabla ya mechi ili aiangalie pitch na sababu nyenginezo zinavyoeleza.
Simba kuja bila taarifa hapo uwanjani kisheria hoja yake inabaki kuwa ni dhaifu na ni kwa sababu sheria inatambua utaratibu wa mawasiliano na unaheshimiwa. Yaani, Simba alifanya jitihada yoyote ya mawasiliano ili hilo litimizwe?
Ikiwa kama Simba haikufanya hivyo na ikadai yeye amefuata kanuni kama inavyoelekeza bado sheria itamtupa mkono kwa sababu, haki haiwezi kutekelezwa nje ya utaratibu.
Yaani, sheria imempa Simba haki fulani, lakini sheria inataka utekelezaji wake unapaswa kufuata utaratibu wa busara unaoeleweka katika mazingira husika. Kwa nini? Kwa sababu, katika muktadha wa kisheria, haki si jambo la kutekelezwa kiholela bali linahitaji kufuata taratibu maalumu ili kuhakikisha linatendeka kwa usawa na haki.
Kwa nini kwa usawa na haki? Sheria haitumiki kwa namna ya kulazimisha upande mmoja kushindwa kwa sababu ya makosa ambayo ungeweza kuepuka. Huwezi ukaja ghafla tu ukiwa hujatoa taarifa, kisha ukadai kuwa umenyimwa haki yako. Sheria pia hutegemea na nia njema na busara pia.
Ukija kwenye hoja ya kughairisha mechi, kwa kuwa Simba ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa tamko, Je, kuna kifungu chochote ambacho kinalinda dai lake awali na kufanya kuighairishwa kwa mechi? Jawabu ni hakuna!
Pengine inaweza kutoka hoja nyengine kuwa Simba si aliyeghairisha mechi, bali ni bodi ya ligi.
Ikiwa hali ni ya namna hii na yakifanyika marejeo ya asili ya madai ya Simba na kwa kuwa hakuna madai ya msingi kisheria kwa Simba kususia mechi kuna mambo yataibuka nayo ni bodi ya ligi au mamlaka ya mpira inamlinda badala ya kuchukua hatua stahiki.
Mazingira haya yanaweza kisheria kuitwa willful blindness yaani kufumbia macho ukiukwaji wa kisheria.
Katika muktadha wa mpira wa miguu hali hii inaweza kuangukia kwenye makosa yafuatayo:
1) Upendeleo wa wazi (Bias/Favoritism)
Yaani bodi ya ligi inamlinda mhusika badala ya kuhakikisha sheria na kanuni zinaheshimiwa (zinafuatwa bila upendeleo).
2)Rushwa au mgongano wa maslahi (Corruption/Conflict of interest)
Yaani, bodi ya ligi inamlinda mhusika kwa sababu ya maslahi fulani binafsi au kuwa na ukosefu wa dosari za kimaadili (rushwa)
Na sababu nyenginezo zinaweza kuwekwa na wengineo!
Mimi ni shabiki wa Simba, lakini hili suala ukiliangalia kisheria na hata kimuktadha wa sheria za mpira wa miguu madai ya Simba ni dhaifu. Ikiwa kama Yanga wakilivalia kidete na kulipeleka mamlaka za juu kabisa za mpira Simba lazima rungu lishuke kwake!
Si Simba tu, bali bodi ya ligi nayo pia. Ikiwa TFF ikashindwa kusimamia ipasavyo na kisha Yanga ikaamua kulipeleka ngazi za juu kama Uzi zitende haki hilo rungu litaathiri mpaka ligi yetu, mfano halisi ligi ya Italia rungu walilopigwa, kwa sababu Simba itaashibiwa na TFF itaadhibiwa pia na ligi yetu itakuwa mashakani.
Ni busara za Yanga pekee ndiyo zitakazoinusu ligi yetu.
Mkuu, haya mambo inabidi tuyaongelee kwa uwazi tusiyaongelee kiushabiki.Umeandika maandishi mengi lakini inaonesha hujui mazingira halisi yaliyokuwepo.Ni kweli Simba hawakuwasiliana na Yanga na viongozi wa uwanja, lakini walipofika uwanjani meneja uwanja alipigiwa simu na kufika,aliwafungulia geti lakini makomandoo wa Yanga waliwazuia na kuleta vurugu.
Sawa, tukubaliane kwambi hili ni kosa. Tuje kwenye kanuni ambazo ndizo mwongozo wetu zinasemaje.kufika,aliwafungulia geti lakini makomandoo wa Yanga waliwazuia na kuleta vurugu.Hili la vurugu si wewe wala viongozi wa Yanga wanalizungumzia,
Kanuni ya 34:1 (1:3)Afisa Usalama wa mechi,hiyo pia wametaja kuwa ni sababu ya kuahirisha mechi na si Simba kushindwa kufanya mazoezi.Wametumia kanuni ya 34:1(1.3) inayowapa mamlaka ya kuahirisha mechi.
Kwa hapa ni sawa, nakubaliana na wewe, kwa mazingira ya Yanga kupewa point 3 ni magumu.Ambapo hatuelewani ndugu ni sehemu ndogo sana.
Ni kweli kisheria na kanuni Simba alikosea kugomea mchezo wake wa derby kisa kunyimwa fursa ya kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo
Lakini wakati Simba wamegomea mchezo, mechi husika ilighairishwa na bodi ya ligi
Yanga wanadai points 3 kwa kanuni gani na wakati mchezo haukuwepo?
Makosa binafsi ya bodi ya ligi yanaipaje Yanga points 3 na kuiadhibu Simba?
Je Yanga alifanya yanayohitajika siku hiyo ya mchezo ili aweze kupewa points za mezani? Kulikuwa na waamuzi,Kamisaa wa mchezo alikuwepo? Nani alianzisha na kumaliza huo mchezo baada ya Simba kutotokea?
Kama vitu vinavyopaswa kufanywa ili upewe points 3 havikufanyika wao Yanga wana uhalali gani kudai hizo points na wanatumia kanuni ipi?
Malalamiko yote ya Yanga yanaweza kuwa halali ikiwemo kulipwa fidia,kutaka baadhi ya viongozi wa bodi ya ligi wajiuzulu nk. Ila hili la kupewa points za mezani wanasimamia wapi?
Mkuu unaandika maandishi mengi yasiyo na mantiki kwani unanukuu kanuni ambazo hazipo, Unaweza kusema na kuinukuu hapaMkuu, haya mambo inabidi tuyaongelee kwa uwazi tusiyaongelee kiushabiki.
Mazingira halisi yanafahamika na yalishazungumzwa na tayari yalishawekwa kwenye ripoti tena kwa maandishi na bodi ya ligi ya kuwa Simba ilifika bila taarifa.
Binafsi mimi ni shabiki wa Simba, lakini kwenye ukweli tutauzungumza.
Simba kufika bila taarifa kisheria ni kosa na nimeshalizungumzia huko juu. Hili ni kosa la kwanza.
Mazoezi kabla ya maechi (pre match training) wachezaji na benchi la ufundi ndiyo wanaotakiwa kuingia pekee. Lengo ni kuwa, timu ya ugenini wanapata fursa ya kufahamu hali ya uwanja, mazingira, na hali ya hewa ili kujitayarisha vyema kwa mechi. Benchi la ufundi ni makocha, madaktari na wataalamu wa viungo.
Kwa nini timu yetu ya Simba ilitaka iingie na watu ambao hawamo kwenye benchi la ufundi? Huku si ukiukwaji wa kanuni? Na kama ni ukiukwaji wa kanuni wale wa getini wafanyaje? Wawaachie mvunje kanuni?
Uzuri clip uliyoiweka niliiona kabla ili nitafute ukweli kwenye hili. Wachezaji na benchi la ufundi waliruhusiwa kuingia, isipokuwa wasiyohusika walizuiwa kuingia. Hili halikufanyika kwa mapenzi binafsi, bali kwa mujibu wa kanuni.
Kwa nini hili tunalikwepa wana Simba?
Sawa, tukubaliane kwambi hili ni kosa. Tuje kwenye kanuni ambazo ndizo mwongozo wetu zinasemaje.
Kwa kuzingatia kanuni husika la mpira wa miguu TFF pamoja na miongozo ya FIFA, uamuzi wa kughairisha mechi inapswa kufanywa kwa kuangalia sababu zipi?
Kanuni ya 34:1 (1:3)
Kutokana na kanuni hii uliyoiainisha kimsingi ianelezea mechi inaweza kughairishwa kutokana na sababu za dharura au za msingi. Ina maana gani(?), ina maanisha kwamba, ikiwa kuna hali isiyotabirika inayoweza kuathiri usalama, utaratibu au ufanisi wa mchezo ulichokiandika hapo juu ndicho kinachoweza kutokea.
Ikiwa sababu ni usalama, na ndicho hicho kipengele timu ya Simba imekitumia, cha kufanya ni kurudi kwenye kanuni na mwongozo wa TFF na FIFA, vikizungumzia usalama vina maanisha ni usalama wa namna gani(?)
Vpengele muhimu vya usalama kwa maana neno usalama wa mechi vimefafanunuliwa ni usalama wa namna gani, ambavyo:
1. Hali mbaya ya hewa – Kama mvua kubwa, radi, au upepo mkali unahatarisha usalama wa wachezaji na mashabiki.
2. Matatizo ya kiusalama – Kama kuna vurugu, ugaidi, ghasia za mashabiki, au vitisho vya usalama.
3. Hali za kiufundi – Kama taa za uwanja hazifanyi kazi au kuna tatizo la uwanja ambalo linaathiri mchezo.
4. Magonjwa au majanga ya dharura – Kama kuna mlipuko wa ugonjwa (kama COVID-19) au majanga ya asili kama tetemeko la ardhi.
5. Kifo cha mchezaji au ofisa wa mechi – Katika hali maalum, mechi inaweza kuahirishwa ikiwa kuna kifo cha ghafla cha mtu muhimu katika mchezo. Mfano mzuri ni Barcelona baada ya kufiwa na daktari wao.
Tafadhali tuambie, Simba ilikosa usalama gani kwenye hivyo vipengele mpaka kughairisha mechi?
Wakikujibu ni tagMkuu, haya mambo inabidi tuyaongelee kwa uwazi tusiyaongelee kiushabiki.

Okay!Mkuu unaandika maandishi mengi yasiyo na mantiki kwani unanukuu kanuni ambazo hazipo, Unaweza kusema na kuinukuu hapa
1.Ni kanuni namba ngapi inasema timu ikitaka kwenda uwanjani lazima itoe taarifa kwa timu mwenyeji?
1
2.Ni kanuni no ngapi inasema ni wachezaji na bench la Ufundi tu ndio wanaruhusiwa kuingia uwanja wa mazoezi?
3.Kanuni namba ngapi inawapa mamlaka makomandoo wa Yanga kukagua huyu ni mchezaji,benchi la Ufundi na kufukuza wasiohusika?
4.Hivyo vipengele vinavyotoa maana ya Usalama vimefafanuliwa kwenye kanuni namba ngapi ya bodi?
5.Miongoni mwa maana uliyotoa kuhusu Usalama umeandika "vurugu" na miongoni mwa malalamiko ya Simba waliyopeleka kwenye bodi ni kufanyiwa vurugu na makomandoo wa Yanga,vipi kama nao Simba wakiamua kuja na makomandoo wao siku ya mechi na kuwazuia na kuwafanyia vurugu wachezaji wa Yanga wasipite kwenye geti lisiloruhusiwa unategemea amani na Usalama utakuwepo?
Uhu ujinga mnautoawapi wakati niwatu tunawaheshimu nyuma ya keybord??Simba aliandika barua kwa umma na akaandika bodi ya ligi akihainisha kinachofanya asiende uwanjani siku inayofuata sasa wewe hao uliowataja wanafuata nini wakati mwenye mamlaka na Mpira kaahirisha mchezo wewe uyanga wako unakuja na hoja chai!Kwa kutumia tu akili ya kawaida, ni wazi kuahirishwa kwa hii, mechi sio jambo lililozuka tu, bali kuna uwezekano mkubwa lilikuwa ni tukio la kupangwa na ndio maana Simba wakagoma kisha baadae Bodi ya Ligi nao wakaja na uamuzi wa kuahirisha mechi(mpango mkakati).
Kwa msingi huo, FIFA au CAS watahitaji kuchunguza kwanza ili waweze kutoa uamuzi na hii ni kwasababu Bodi ya Ligi teyari imejiingiza katika huu mgogoro, vinginevyo lilikuwa ni jambo rahisi tu la kuangalia kanuni zinasemaje na kutoa uamuzi.
Maamuizi ya Bodi kuahirisha hii mechi sio tu yatafanya iwe ni vigumu kwa FIFA au CAS kutoa uamuzi, bali watahitaji kujua ni kwanini Bodi ya Ligi walifanya blunder kama ile.
Wanaostahili kuchunguzwa/kuhojiwaa
1.Uongozi wa Club ya Simba
2, Viongozi wa Bodi ya Ligi
3. Meneja wa uwanja
4. Walinzi wanaodaiwa kuwazuia Simba kuingia uwanjani
5.Viongozi wa club ya Yanga(watahojiwa kama mashahidi).
Adhabu inaweza kwenda kwa Simba pamoja na Bodi ya Ligi.
Nimemaliza.