bornagain
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 3,383
- 1,357
Leo tarehe 28/06/2013 ndiyo nimeamua kutokuchangia tena damu kwa hao watu wanaojiita sijui Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS).Nimechukua pia jukumu la kuwashawishi hata ndugu zangu wasichangie tena damu na kama ni kosa basi nisamehewe tu.
Kisa chenyewe ni kwamba nina mgonjwa kalazwa Amana Hospital katika Manispaa ya Ilala, tokea wiki iliyopita amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa ambao unahitaji upasuajia mdogo, sasa daktari ni kila siku anamuambia kuwa inatakiwa apate watu wa kumchangia damu la sivo upasuaji hautawezekana maana Amana nzima hawana damu hata lita moja kwa hiyo mgonjwa inatakiwa atafute ndugu wa kumuongezea damu, tumeenda kwa ajili ya kuchukuliwa damu pale kwa ajili ya mgonjwa wetu tulipofika hospital bahati nzuri kuna daktari namfahamu yeye yupo Temeke nikampigia kumuuliza inakuweje hospitali ya Amana hawana damu,akaniambia nimpatie jina la daktari anaedai kuwa damu hamna.
Nilivompatia jina la daktari ni kwamba fasta mgonjwa wangu hakudaiwa tena damu na mambo yote yamekamilika sasa, baada ya kupeleleza nikaambiwa kuwa damu ni dili pale ilitakiwa mgonjwa atoe kama 20,000 mpaka 50,000.
Sasa kama kweli wananchi wanajitolea damu bure kwa nini hospitali wazifanye kama ni deal? Kuanzia leo sitochangia damu kwenye hao watu wanaojiita damu salama nitachangia specific kwa mgonjwa na sio kupitia hizo kampeni zao za kiwiziwizi tu