Riwa
Platinum Member
- Oct 11, 2007
- 2,607
- 3,079
Nilivompatia jina la daktari ni kwamba fasta mgonjwa wangu hakudaiwa tena damu na mambo yote yamekamilika sasa, baada ya kupeleleza nikaambiwa kuwa damu ni dili pale ilitakiwa mgonjwa atoe kama 20,000 mpaka 50,000.
Sasa kama kweli wananchi wanajitolea damu bure kwa nini hospitali wazifanye kama ni deal? Kuanzia leo sitochangia damu kwenye hao watu wanaojiita damu salama nitachangia specific kwa mgonjwa na sio kupitia hizo kampeni zao za kiwiziwizi tu
Sasa wewe mgonjwa wako keshapata damu na 'mambo yamekamilika'...unataka kuwachochea wenzako wakatae kuchanga damu, wagonjwa wao wafe!?
Mapungufu ya mtu mmoja mmoja yapo kwenye idara za afya..wezi wapo...wala rushwa wapo..lakini sio kwa sababu ya mapungufu na uroho wa hao watu basi uhukumu wagonjwa wengine wafe kwa kukosa damu kwa kuchochea waTanzania wasichangie damu! Mbona hujasusa kulipa kodi na kuchohcea watu wasilipe kodi wakati unajua kodi zetu zinaibwa!
Jamani...tuchange damu, waTanzania wenzetu wanakufa kwa kukosa dawa hii hadimu wakati wengi wetu tumeibeba ya kutosha miilini mwetu. mapungufu ya mtu mmoja mmoja yapo, njia ya kutokomeza mapungufu hayo zipo kwa kutoa taarifa sehemu husika...TUSISUSE..WALA KUCHOCHEWA KUSUSA KUTOA DAMU NDUGU ZETU WAKAFA!