Sitooa abadan asilan

Mtuache

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
256
Reaction score
658
Zamani ilikuwa mtu akiwa kwenye ndoa unaona enhee kweli jamaa anafaidi. Kuna vitu ulikuwa ili uvipate aidha kwa mwanamke au mwanaume lazima uingie kwenye ndoa.

Sikuhizi mambo yamekuwa vice versa.

Binafsi sijaona sababu ya kunifanya nioe. Rafiki zangu waliooa kila siku wananiambia matatizo wanayokumbana nayo. Leo hili kesho lile.

Haya basi usiseme sitaki kuoa kisa hizo shida lakini pia raha zao, raha wanazopata kwenye ndoa hata mimi nisiyeoa naweza kuzipata.

Sijui wanawake wamejirahisisha au ndo usasa? Naona vitu vimekuwa tofauti na zamani

Cha msingi ni kuwa na ela tu.

Ela ndo kila kitu ukiwa nazo utapata kila kitu anachopata mwanandoa tena bila karaha zake. Binafsi sijioni nikioa labda miaka inavyozidi kwenda nitabadili mtazamo wangu.

Ila kwa sasa BADO SANA.
 
Tuendelee kuzichakata mbususu Kwa kufanya ubunifu kwenye mbususu na kutafuta pesa daily
 
Kwa upande mwingine ongezeko la vijana wengi ambao hawaoni umuhimu wa ndoa.

Ni tafsiri ya kuwa wengi ambao hawaoni umuhimu wa ndoa isipokuwa ngono na kupata watoto basi wameanza kupukutika, kutokana na uwezekano wa kupatikana hayo hati pasi na ndoa.

Lakini hii haina maana kuwa ndoa haina thamani yoyote, hasha bali waliostaarabika na wanafahamu umuhimu wa ndoa basi wanaendelea kuoa na wanauona umuhimu wa ndoa.

Na migogoro katika ndoa fulani sio kipimo cha ubaya wa taasisi ya ndoa kwa ujumla wake.
 
Kijana Kuoa Ni Muhimu kuliko unavyofikiria.

Kama ww umetoka kwenye familia yenye Baba na Mama, na ukalelewa.
Kwann unataka watoto wako walelewe kiholela?..

Na Kama umetoka kwenye familia ya upande mmoja, najua umepitia changamoto nyingi. Unataka pia watoto wako wapitie Kama ww?..

Ukioa unakuwa na Maono ya kujenga na kutunza Familia.

Utaoa, utawajibika Kama baba, utapanga nyumba(utaacha kukaa gheto), utanunua kiwanja, utajenga, utaanzisha biashara nk nk.

Usipooa Sasa, maisha yako kila mwaka Inakuwa Ni kuhangaika na wanawake, Leo huyu, kesho huyu, miaka na miaka Ni kusuluhisha tu mpenzi.

Utakuwa Mwanaume hopeless kabisa.

Mimi nimeoa Nina miaka 6. Nina maendeleo ambayo naona kabisa ningekuwa mwenyewe Nisingekuwa hapa.
 

[emoji2][emoji2][emoji2][emoji1544]
 
Endeleeni kuzalisha nje badae mje muwaponde humu single mothers wa watu...kuoa au kuolewa utabaki kuwa na heshima yake hata mje maelfu kusema ndoa sio jambo jema..kuna kazi zingine mtazikosa au vyeo mtavikosa kisa tuu huna ndoa ya kisheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…