Sitosahau mapacha wa Antivirus walivyoomba msamaha clouds

Hakuna chenye mwanzo kisichokuwa na mwisho,Radio One ,Radio Free leo zipo wapi na kama mfuatiliaji mzuri Clouds nguvu yao imepungua sababu ya EFM na kama Wasafi wakija na program nzuri basi itaendelea kushuka zaidi .Mapacha naona waliamua kulegeza sababu Captain mwenyewe Sugu alimalizana na Ruge baada ya Ruge kuwaomba MBOWE na MCHIMBI wamsaidie kumaliza utata wake na Sugu (Sugu alikuwa anawachana sana bungeni kuhusu unyonyaji wao kwa wasanii kupitia FIESTA na kuna mwaka akaandaa tamasha mbeya kiingilio bure siku ilele ambayo nayo FIESTA inafanyika ,wakaona anawaharibia kwani walipata hasara) na ndio maana wasanii wengi ktk antivirus nao wakaamua kusanda.Ila hiyo Radio ni swala la muda tu watu wataichoka EFM wapo vizuri sana.
 
Pamoja na kujidharilisha vile kwa kuomba msamaha ON AIR lkn bado Ngoma zao hazipigwi!!! Naungana nawe mtoa hoja BORA WANGEKAUSHA TU maana hakuna tofauti yoyote ya kabla na tangu walipoomba msamaha.
Tena wangekausha wangekuwa mashujaa wa ile vita kwa kusimamia katika msimamo wao
 
Hata wasafi radio
 
Kwa,kweli inatia uchungu unapandishwa jukwani unaimbishwa ata mia akuna siku ukifanikiwa kutoka kwa jitiada zako wanataka wakupangie show wakulipe shiling ngapi
Sasa msanii kama harmonize halipwi fiesta je hapo wengine inakuaje
 
Ruge ni mtu makini sana,vijana huwa wanapandikizwa ujinga wanaanza kumrushia maneno wakianza kudidimia wanaenda kuomba msamaa sasa ngoja tusubiri ligi yake na wasafi maana efm wamesha sanda na muda ndio utatupa majibu.
Vipi kuhusu kwa sugu na jd
 
Ruge ni mtu makini sana,vijana huwa wanapandikizwa ujinga wanaanza kumrushia maneno wakianza kudidimia wanaenda kuomba msamaa sasa ngoja tusubiri ligi yake na wasafi maana efm wamesha sanda na muda ndio utatupa majibu.
RUGE NI MAKINI KWENYE KUHARIBIA WASANII NA KUWANYONYA,LAKINI NAONA THIS TIME HANA BAHATI,AMEWANYONYA WENGI NA AMEHARIBU NDOTO ZA VIJANA WENGI MTAANI KISA TU KUTAKA UMUNGU MTU,YANI AKITAKA KUKUTOA KWENYE MCHIRIZI WA RIZIKI ANAKUTOA,DAAH!!I ILA INAUMA SANA,,FIKIRIA, PRO J,NGWEA,RAMA D,T .I.D,NA WENGINE KIBAO..
 
Dah!!!wengine hapo walisha fanikiwa wakajiingiza kwenye anasa za dunia lawama anatupiwa Ruge,mbona vijana wenzao kama J mo wamefanya kazi na Ruge na wanaendelea kufanya nae kazi sasa hivi wako vizuri kwenye maisha yao na wanamafanikio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…