son of a teacher
JF-Expert Member
- Jul 30, 2017
- 541
- 1,449
Siku simba waliponipa elimu hii
Bahati nzuri huyu jamaa ambaye ni mwandishi wa habari za michezo ni mwanachama hai wa simba ,binafsi sikuwahi kufahamu kuwa ni mdau wa simba kwani hata mashabiki wa yanga wanampenda sana na huwa wanamtumia kwa mambo mengi na mimi binafsi nina urafiki naye mkubwa sana.
Alinitumia message kwanza ,aliniuliza bwana mdogo uko wapi? Kisha akaniambia twende ukajifunze maisha ya timu zetu tukiwa pemba wakati tunaelekea kijiji cha mganga mwenyewe,ghafla alitokea chatu ,binafsi nilipata hofu,lakini sharti kabla hatujaondoka Dar es salaam niliambiwa njiani tukiona chochote nitulie,Nilitulia ingawa hofu ilikuwa kubwa moyoni ,huku mwenyeji akiwa amenishika mkono kwa nguvu tulikutana na Mganga mwenyewe,ni mwenyeji wa Zanzibar lakini asili yake ni MOZAMBIQUE.
Alitandika ngozi ya simba na ngozi ya fisi na ndio mara yangu ya kwanza kuona ngozi ya simba sababu nimezaliwa Dar ,nimekulia Dar hivyo kuishi kwangu Dar sijawahi kushuhudia mnyama pori bali naishia kuwatizama kwenye luninga lakini siku hio niliona ngozi ya simba na fisi ikitandikwa.Baada ya muda kidogo alileta uji ambao ulikuwa wa rangi nyekundu akatutaka tuunywe kama maagano ya kutosalitiana kwa kile ambacho kitafanyika pale.
Wakati anaendelea na uganga wake yeye alikuwa anatumia mistari ya kiganja chake cha mikono katika unajimu wake na alikuwa anatumia jina la "CALMAN" katika kila jambo ambalo alikuwa analifanya ,huyu calman ni jini wa mbingu ya tano ambaye anahusika na maswala ya michezo tu,alitueleza kuwa mechi ni ngumu sana na tayari kuna wachezaji sita wa simba walikuwa na lengo la kuhujumu timu.
Akatupa masharti matatu ,kwanza wachezaji waletwe kwake kwenye kilinge ,cha pili alitaka maji ambayo yameoshewa maiti yaliyokaa siku tatu kwa sababu tayari yanga walikuwa na magoli na magoli matatu hata kabla ya mechi na la tatu alitutaka siku moja kabla ya mechi ipelekwe uwanjani maiti ya mama ambaye amefariki baada ya kitoto chake kufia tumboni Vitu vyote vilikamilika na wachezaji husika waliketwa Pemba cha ajabu kilichonishangaza walipoletwa wachezaji pale kwa mganga waliwekwa juu ya ungo kila mchezaji alikalia ungo wake wakiwa wanatokwa na majasho mengi kwaajili ya hofu na ungo zilipaa kidogo juu kama urefu wa mita mbili na kuganda.Ndipo mganga yule akaanza kuzungumza nao nakuwaeleza madhara ambayo watakutana nayo endapo wakiisaliti timu,mikononi wakiwa wameshikilia vibuyu ambavyo vilikuwa vinafuka moshi.Tulifunga safari ya kurudi Dar lakini alichonishangaza zaidi ni baada ya kuwakabidhi viongozi wa safari chupa ya maji ya kunywa ikiwa na mayai ndani mazima kama yalivyo,nilijiuliza mayai yale yameingiaje ndani ya chupa ile ilhali mdomo wa chupa ni mdogo nilipatwa na mshangao sana na masharti ya mganga siku ya mechi chupa lile la mayai lichomwe na lifukizwe
Nilijitahidi kupiga picha nyingi za vitu vya maajabu ambavyo niliviona pale
Mwisho wa mechi yanga walipata goli tatu na simba walipata goli tatu ,..mechi iliisha kwa sare
Nasikia simba wameenda Zanzibar kujiandaa na mechi dhidi ya yanga lakini kinachonishangaza zaidi kwanini tokea simba walivyoenda Pemba huku Dar mvua zinanyesha kwa mfululizo..ndugu zanguni yule mganga waki-mozambique ni fundi hatari hashindwi ,nina wasiwasi hii mvua ya dar sio ya tabia ya nchi huenda mganga waki- Mozambique aliyopo pemba anafanya yake