Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Mtoa simulizi nilikwambia,ukifika sehemu ya demu iruke hujanielewa,unaona sasa yaan kwa kutaja demu tu ushaanza kupoteza ladha na watu pia wataanza tena kuitilia shaka hadthi yako kwasbb haingii akilini ngumu sana kuwaza mwanamke kwenye situation ile,hiyo moja , pili ni kwamba ulitumiwa hela 20000,simu ya makamu ulikuwa nayo wewe na uliulizwa una shngap ukasema huna hela so ile twenty uliotumiwa ulipokea kwa mtindo gani?
 
We naepunguza munkali,asidinde vipi?Basi maskini wasingezaana...na kuhusu Simu amesema ameuza,ila line kabaki na line zake!
 
Kwa matatizo yote uliyokuwa nayo bado ulikuwa na nyege?
 
Inawezekana maana kuna wayahudi walikuwa wamewekwa kwenye kambi wakisubiri kuuawa, walikuwa wamechanganywa na wanawake ila wakawa wanapigana mambo

Halafu pia jamaa alikuwa katumiwa 20k na mzee wake, alikuwa amehakikishiwa kupata chakula na sehemu ya kulala kwa siku kadhaa, so stress zilikuwa zimeshuka kiasi cha kutosha kuwa na nyege 😂😂
 
Bro nimekuamini maana haya maeneo unayotaja nayafaham yote na hiyo shule ya Chinongwe naifaham vizuri...Pole sana bro
 
Hahaha Machinga!! ni kweli mkuu machinga linapitaga,luchelegwa,mbecha huko linaenda kutokea nanganga linaunga Lindi mpaka Dsm...Pole ila ukiwa ugenini jitahidi usiingize tamaa za kimwili
 
Kwanini niiruke Kati ni moja ya tukio Zito halafu pesa nilitumiwa kwenye line yangu ndio maana aliponipa simu ndogo nilikaa nayo kwa mda ni kaweka line humo ndokuna namba nyingi za ndugu jamaa na marafiki niliokuwa nikiwapigia kuomba msaada, alipokuja makamu nikachomoa line yangu nikampa simu yake
 
Hao waliokusaidia hapo Kijenge walikuwa ni ndugu zako?

Inaonekana ndugu yako wa Dar hakuwa muaninifu eeeh?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…