Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Nakiri kuwa ni aibu sana kumueleza mtu kuwa unaskia njaa na unahitaji chakula,hivyo ukikutana na binadam mwenzako hajakuomba hela Wala hajakuomba chochote Ila kafikia hatua ya kuvua aibu zote na kakuomba chakula tu tafadhali kama unaweza kumsaidia usimuache Wala usimuone chizi mnunulie/mpe chakula

Dunia ina adhabu nyingi sana ila miongoni mwa adhabu zake ni njaa huku ukiwa hauna pesa wala msaada wowote tulio wahi kupitia hiyo hatua tunajua.
 
Guest gani mkuu maana Mimi nipo makete
 
Du..mwandishi mzuri sana!
Huyu ni mtunzi mzuri/msimuliaji

Ila kuandika si mzuri sana.

Hadithi ni tamu mno.

Ila masuala ya sarufi, Aya,neno na neno yanampiga chenga,

Ila nimependa jinsi anavyoishia kwenye kila episode,anaishia kwenye Aya ambayo inatia hamu zaidi kusoma.

Yote kwa yote hongera na nimpongeze kwa kuwa inspire vijana wenzie ambao pengine walidhani Dunia imewatenga,

Wajifunze uvumilivu/na subira katika mapito yao.
 
Wakala wa Nini???? Na ilikuwa mwaka gani??
 
Mwandishi ana power of imagination na kuhadithia situation.
Hadithi nzuri.
 
Uko sahihi..hawezi kuwa vizuri kwenye kila kitu..ndiyo maana kunakuwepo na wahariri.
 
Guest gani mkuu maana Mimi nipo makete
Sijui ni guest gani fikiria ni 2011 mwezi wa 2 huko. Kama umetoka makete unakuja njombe ilikuwa mkono wa kushoto. Kabla ya kwenda guest nilipanga kulala upande uleule mbele kidogo upande wa kushoto nilishuka chini hivi kulikuwa na pagale.
Nilipojaribu kulala pale palikuwa na baridi kali sana na kimvua kilikuwa kinanyesha.
Ikabidi niende kwa huyo dada guest kuomba msaada wa kulala ambapo alikubali bila hiyana kabisa nikalala bure.

Kabla ya hapo nililala sehemu moja wanaita Zambia nadhani ni kabla ya kipagalo. Hapo sikuwa na cash, mhudumu wa guest nilimrushia vocha ya 3000 alikubali, nikalala. enzi hizo MPESA unaikuta mjini tu! tigopesa au airtel money ilikuwa haijazaliwa nadhani.

Pale zambia njia panda upande wa juu kidogo palikuwa na kilabu cha ulanzi kuna jamaa alikuwa anauza ulanzi. Huyu nilinunua ulanzi lita 2 na viazi vimechanganywa na mboga vya mia 2 nikamrushia vocha ya mia 5, akawa na faida ya 100.
 
Bulongwa Hyo mkuu
 
Hapo kilwa day ulibahatika kumuona mwalimu Hussein?!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…