Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Nakiri kuwa ni aibu sana kumueleza mtu kuwa unaskia njaa na unahitaji chakula,hivyo ukikutana na binadam mwenzako hajakuomba hela Wala hajakuomba chochote Ila kafikia hatua ya kuvua aibu zote na kakuomba chakula tu tafadhali kama unaweza kumsaidia usimuache Wala usimuone chizi mnunulie/mpe chakula

Dunia ina adhabu nyingi sana ila miongoni mwa adhabu zake ni njaa huku ukiwa hauna pesa wala msaada wowote tulio wahi kupitia hiyo hatua tunajua.
 
Stori ya jamaa imenifanya niende nikafukue ofisini namba ya simu ya dada fulani pale makete ili nimlipe fadhila, bahati mbaya namba alishapewa mtu mwingine.

Imagine huyu dada nilifika pale makete nilikuwa sina hata mia na ishakuwa jioni. Nikaenda gesti kwa sababu chimbo nililopanga kulala palikuwa na baridi kali sana. Yule dada mhudumu wa gesti nilivyoanza kumpiga sound tu akanikatisha, akasema usiendelee kuongea akasema nifate.
Akanionesha chumba nililala bure kabisa nilipewa na maji ya moto japo sikuoga.
Wanaume tunapitia mengi jamani asikwambie mtu.
Guest gani mkuu maana Mimi nipo makete
 
Du..mwandishi mzuri sana!
Huyu ni mtunzi mzuri/msimuliaji

Ila kuandika si mzuri sana.

Hadithi ni tamu mno.

Ila masuala ya sarufi, Aya,neno na neno yanampiga chenga,

Ila nimependa jinsi anavyoishia kwenye kila episode,anaishia kwenye Aya ambayo inatia hamu zaidi kusoma.

Yote kwa yote hongera na nimpongeze kwa kuwa inspire vijana wenzie ambao pengine walidhani Dunia imewatenga,

Wajifunze uvumilivu/na subira katika mapito yao.
 
Kuharakisha maisha tu, nyumbani sikuwa na shida yoyote ile kila kitu uhakika, na niliaga vizuri tu japo walisikitika kwa maamuzi yangu. Baada ya kumaliza fm 4 nikaona kula vya bure nyumbani inatosha, nikasema nitafute changamoto mpya.

Mambo yalivyokuwa magumu nikapiga simu kwa mama anitumie hela japo sikufanikiwa kuitoa kutokana na changamoto ya mawakala kutoka makete hadi ikonda sikuona wakala. Kutoka Makete hadi Ikonda nilitembea masaa matano kwa mguu.
Wakala wa Nini???? Na ilikuwa mwaka gani??
 
Huyu ni mtunzi mzuri/msimuliaji

Ila kuandika si mzuri sana.

Hadithi ni tamu mno.

Ila masuala ya sarufi, Aya,neno na neno yanampiga chenga,

Ila nimependa jinsi anavyoishia kwenye kila episode,anaishia kwenye Aya ambayo inatia hamu zaidi kusoma.

Yote kwa yote hongera na nimpongeze kwa kuwa inspire vijana wenzie ambao pengine walidhani Dunia imewatenga,

Wajifunze uvumilivu/na subira katika mapito yao.
Mwandishi ana power of imagination na kuhadithia situation.
Hadithi nzuri.
 
Huyu ni mtunzi mzuri/msimuliaji

Ila kuandika si mzuri sana.

Hadithi ni tamu mno.

Ila masuala ya sarufi, Aya,neno na neno yanampiga chenga,

Ila nimependa jinsi anavyoishia kwenye kila episode,anaishia kwenye Aya ambayo inatia hamu zaidi kusoma.

Yote kwa yote hongera na nimpongeze kwa kuwa inspire vijana wenzie ambao pengine walidhani Dunia imewatenga,

Wajifunze uvumilivu/na subira katika mapito yao.
Uko sahihi..hawezi kuwa vizuri kwenye kila kitu..ndiyo maana kunakuwepo na wahariri.
 
Guest gani mkuu maana Mimi nipo makete
Sijui ni guest gani fikiria ni 2011 mwezi wa 2 huko. Kama umetoka makete unakuja njombe ilikuwa mkono wa kushoto. Kabla ya kwenda guest nilipanga kulala upande uleule mbele kidogo upande wa kushoto nilishuka chini hivi kulikuwa na pagale.
Nilipojaribu kulala pale palikuwa na baridi kali sana na kimvua kilikuwa kinanyesha.
Ikabidi niende kwa huyo dada guest kuomba msaada wa kulala ambapo alikubali bila hiyana kabisa nikalala bure.

Kabla ya hapo nililala sehemu moja wanaita Zambia nadhani ni kabla ya kipagalo. Hapo sikuwa na cash, mhudumu wa guest nilimrushia vocha ya 3000 alikubali, nikalala. enzi hizo MPESA unaikuta mjini tu! tigopesa au airtel money ilikuwa haijazaliwa nadhani.

Pale zambia njia panda upande wa juu kidogo palikuwa na kilabu cha ulanzi kuna jamaa alikuwa anauza ulanzi. Huyu nilinunua ulanzi lita 2 na viazi vimechanganywa na mboga vya mia 2 nikamrushia vocha ya mia 5, akawa na faida ya 100.
 
Sijui ni guest gani fikiria ni 2011 mwezi wa 2 huko. Kama umetoka makete unakuja njombe ilikuwa mkono wa kushoto. Kabla ya kwenda guest nilipanga kulala upande uleule mbele kidogo upande wa kushoto nilishuka chini hivi kulikuwa na pagale.
Nilipojaribu kulala pale palikuwa na baridi kali sana na kimvua kilikuwa kinanyesha.
Ikabidi niende kwa huyo dada guest kuomba msaada wa kulala ambapo alikubali bila hiyana kabisa nikalala bure.

Kabla ya hapo nililala sehemu moja wanaita Zambia nadhani ni kabla ya kipagalo. Hapo sikuwa na cash, mhudumu wa guest nilimrushia vocha ya 3000 alikubali, nikalala. enzi hizo MPESA unaikuta mjini tu! tigopesa au airtel money ilikuwa haijazaliwa nadhani.

Pale zambia njia panda upande wa juu kidogo palikuwa na kilabu cha ulanzi kuna jamaa alikuwa anauza ulanzi. Huyu nilinunua ulanzi lita 2 na viazi vimechanganywa na mboga vya mia 2 nikamrushia vocha ya mia 5, akawa na faida ya 100.
Bulongwa Hyo mkuu
 
-------SEHEMU YA SABA - - - - -

Nilipopewa msaada wa kuoga ikabidi nibadilishe nguo za kuvaa japo zimejikunya wale wadada wakacheka kidogo wakakausha, sikuwaomba ila kwa moyo mkunjufu wakasema nizivue wanipigie pasi nilitabasamu Kisha nikaingia maliwato kubadili nguo nikaenda kuwapa wakazinyoosha wakanipa. Niling'aa kwa kweli nilipendeza nikawa mtu. Baada ya hapo akili ikawa inawaza kwenye lengo lililonileta kilwa japo popote akili ingenituma siku Ile ya safari ningeenda yaani ningeikosa gari ya kilwa ila ipo ya masasi ningepanda pia lengo nisiwepo Dar Es Salaam. Nikaona kujiajiri au kuomba kazi na ugeni huu sio jambo jepesi ila inabidi tu nijitoe ufahamu pia nisahau yote yanayonisibu. Nikaulizia wapi Kuna shule ya sekondari ya karibu wakasema labda kilwa day. Nikabeba begi langu nikaenda kwa kuuliza mpaka nikafika japo Kuna kaumbali kiasi, nilipofika pale nikawakuta non. Stuff members waliopo nje maana ilikuwa ni jumamosi hivyo walimu walikuwa majumbani nilipowakuta wahudumu wa pale nadhani wapishi na walinzi nikasema nimekuja hapa nina shida na mwalimu either mwalimu mkuu, makamu au academic yule mlinzi akasema yupo makam tu ngoja nikuitie kaa hapo.

Nilikaa sana kama masaa matatu hivi makamu wa shule ya Kilwa day akaja, tukaingia ofisini kuzungumza nikamwambia mimi nimekuja hapa kuomba kufundisha japo nimeishia form six, alitabasamu Kisha akasema aone vyeti alipoangalia akasema wana uhitaji wa mwalimu wa physics ila hana ruhusa ya kuniweka ili nifundishe bila ridhaa ya mkuu wa shule na mkuu wa shule anaumwa ana zaidi ya mwezi hayupo kwahiyo akirudi tutaongea. Nilichoka sana mwishowe nikasema mm nikipata pa kula na kulala tu nafundisha bure, akasema hawezi kuniweka bila uwepo wa mkuu wa shule kwa hiyo ngoma ikawa imebuma mwili wote upo hoi. Ikabidi nibebe begi niondoke Ile nabeba tu Kuna mwalimu mmoja kutoka shule ya mtange sekondari jinsi alivyojitambulisha Kwangu akawa amefika kilwa day secondary yule makamu akasema vipi huko kama mna shida ya mwalimu wa physics huyu hapa hataki hata Mia yako yeye apate pakula na kulala tu. Mkuu wa shule mtange sekondari akasema ninao wakutosha walimu wakuajiriwa wamekuja wapya na watatu wanafundisha physics.

Nikasema basi tena lakini yule makamu akasema ngoja ampigie simu mwalimu wa kivinje sekondari, hii shule ipo kilwa kivinje. Yule mwalimu mkuu akasema yupo njiani ametokea shinyanga kwenye msiba ila baada ya masaa matatu atakuwa yupo kilwa kivinje. Sijui alitumia usafiri upi kufika kivinje maana Kuna watu humu mtasema shinyanga mpaka kilwa huwezi kufika mchana. Yule makamu akasema nijiandae niende tukakutane lakini pia nimwachie namba yangu ya simu kwahiyo nikampa namba ila nikamwambia simu sina niliuza ili nipate nauli, akanipa pole akafunga ofisi tukaagana nikamuuliza huyo mkuu nyumbani kwake ni wapi akasema yupo pale pale kivinje sekondari. Nikaenda stend ya kilwa masoko mida ya saa nane hivi kufika pale baadhi ya watu walioniona asubuhi nikiwa rafu wakaanza kunishangaa tena juu ya usafi wangu [uchafu walishangaa usafi wanashangaa pia.. Hii ndo kilwa].. Mm nikawa nipo straight forward na mambo yangu Sasa pale Kuna hiace na tax tu zinaenda kilwa kivinje gharama ni buku mbili, pesa ikaanza kupungua nikapanda nikasubiri ijaze siti zote tukaamsha. Kufika kivinje bodaboda haoo unaenda wapi nikasema siendi.

Nikamuuliza jamaa mmoja anauza samaki akasema kivinje sekondari nimbali sana kufika kule kwa mguu na Hilo begi sidhani kwahiyo nichukue tu bodaboda hamna namna, nikachukua bodaboda nikasema nina buku hataki natembea kwa mguu, yule bodaboda akasema panda tukafika kivinje sekondari ikawa ni saa kumi na robo hivi kufika pale yule mkuu wa shule akawa bado yupo njiani ila nikamkuta mkewe akapiga simu akamwambia nisiondoke mda si mrefu atafika. Walikuwa ni wasukuma sio wamwera kwahiyo nilikaribishwa ugali na maziwa ya mgando na nyama ya utumbo la tauro nikala nikashiba, nilipumzisha shida zangu kwa mda huo. Saa kumi na mbili jioni akawa amefika mkuu wa shule ya kivinje alipofika tukasalimiana na maongezi kiasi baada ya hapo nikamwambia kiwango cha elimu yangu, akasema ooh sihitaji wa form six mm nikajua umehitimu chuo either diploma au degree maana afisa elimu kata hataki kabisa mtu afundishe bila kuwa qualified. Ikawa imebuma nasiwezi kufosi.

Akaniambia amechoka sana anahitaji apumzike nikamwambia saizi ni saa kumi na mbili na nusu giza limeingia mm huku ni mgeni naomba nilale hapa, akasema pole ila hata mm hii nyumba Ina Vyumba viwili tu na jiko na hapa sebleni, vile Vyumba wanalala watoto wangu na hapa sebleni haturuhusu maana sio sehemu ya usingizi ni sehemu ya kupumzika na kupata dinner and lunch. Kule kivinje sekondari hakuna bodaboda unless umchukue mjini na simjui bodaboda yoyote kwahiyo nikawaaga nikaondoka, ilinibidi nitembee kwa mguu nikiwa nimechoka sana kutoka kivinje sekondari mpaka kilwa kivinje ni umbali wa kilometer 7 kama sio saba basi 8.saa mbili usiku nikawa nipo kilwa kivinje.

Mfukoni nikawa nina 27000 ni nyingi sana kwa kipindi kugumu nilichokuwa napitia. Kufika pale stend nikaona yule bodaboda alienipakia mwanzo akapita kuniuliza vipi unahitaji usafiri? Nikamwambia hapana ila nimeteseka sana kupata bodaboda kivinje sekondari ikabidi niukanyage, akasema pole ila mbona mkuu wa shule ana namba yangu kwanini hakunipigia nije nikuchukue, Sasa mm ilinibidi tu nikae kimya maana nilipandwa sana na hasira sijui aliona akimwita bodaboda atadaiwa yeye ndoalipe nauli? Kilwa ni sehemu ngumu sana ukiweza kuishi Kilwa basi hata jangwani panakufaa. Kiustarabu kabisa nikasema ampigie ili nimwambie nimefika kilwa kivinje salama alipopiga nikaongea nae akasema ngoja ajaribu shule moja ipo lindi mjini yule mwalimu wanajuana sana nae anaupungufu wa walimu wa physics, nadhani huwa wanakutana kwenye vikao vya wakuu wa shule au wanajuana. Nikamwambia Sawa japo nikataka kuanza kukata tamaa ila nikasema ngoja nijipe uvumilivu kama mwanajeshi aliepo vitani.

Yule bodaboda akapigiwa tena na bahati nikuwa tulikuwa bado tunapiga nae stori za hapa na pale, akapokea yule mkuu wa shule akasema mbona huyo kijana hajanitumia namba nikachukua simu sikioni mwa yule bodaboda nikasema mkuu mimi sina simu ila nitachukua namba yako nitakuwa naazima ukipata connection utaniambia. Akasema yule mwalimu mkuu kakubali ngoja nikutumie namba yake muongee nae nikasema Sawa. Dakika tatu hivi akawa ametuma namba tukampigia akasema kesho niende nikamwambia mm ni form six sio chuo akasema hatuwezi ongea kwenye simu serious matter kama hii inabidi kesho niwe lindi mjini niende shuleni kwake, akasema yeye ni mwalimu mkuu wa shule ya sekondari kineng'ene ipo manispaa ya lindi.

Dakika kadhaa baadae yule dogo wa bodaboda akapata kichwa akaniaga akasepa ikawa mida ya saa tatu hivi nikaona bus la MASHALAH limefika kilwa kivinje kutoka Dar Es Salaam sijui kwann Lilichelewa siku hiyo nikasema nikipanda hili Gari kwenda kilwa masoko ni kupoteza tu mda na pesa zangu naenda kufanyaje. Nikapotezea ila akiri ikanijia kwani Gari za kwenda lindi mjini zipo wapi? Wenyeji wakasema nikitaka hata mida hii napata inabidi nipande bodaboda maana mida hii hakuna hiace wala tex lakini pia hiace na tex kituo huwa kipo kule hospital ya wilaya na mda huu kupata ngumu kwa hiyo njia pekee ni bodaboda ili inipeleke sehemu moja inaitwa NANGURUKURU pale ndokuna mabus ya kutoka mikoa ya mbali naweza Pata au malori ya kwenda lindi mjini. Yule dogo wa bodaboda nilitaka nimuungishe lakini akawa ameondoka nikachukua bodaboda nyingine ila nauli iliniuma sana maana kila mtu alisema mwisho 4000 ikabidi tuondoke mpaka NANGURUKURU ikawa ni saa nne usiku nipo NANGURUKURU kuona kama nitapata usafiri wa kwenda Lindi mjini mda huo.


-------inaendelea usichoke.........
Hapo kilwa day ulibahatika kumuona mwalimu Hussein?!!!
 
Back
Top Bottom