----------SEHEMU YA PILI - -----
Safari ya kuelekea Kilwa ikaanza. Nililipa nauli ya Dar Es Salaam to Kilwa shilling 13000 mfukoni mpaka na panda bus nikawa nimebakiwa na 70000 tu kutokana na pesa nyingine Jana usiku Nililipa gest 4000 asubuhi kabla ya kwenda kukata ticket nilienda saloon kunyoa kwa 2000 baadhi ya pesa nilikula mihogo na maji ya kunywa njiani. Ubovu nikuwa kwenye siti nilikuwa nimekaa na mtoto mdogo wa kike ambae alipakiwa na mzazi wake ila yeye huyo mzazi hakuwa anasafiri sasa akaniambia kuwa nimsaidie kumwangalia lakini pia konda alikuwa amepewa taarifa kimsingi ni mtoto ambae huenda ni miaka 11 au 12 huyu dogo yeye alikuwa anashukia somanga. Kwahiyo nikakosa hata msaada wa kuanzia nikifika kilwa itakuwaje maana nilikuwa nategemea labda mtu nitakae kaa nae atanipa mawazo namna ya mji ulivyo na jinsi ya kuhendo swala langu. Tukiwa safarini ilibidi nimuulize huyu dogo endapo anaijua kilwa ili tu nipate pakuanzia dogo akasema yeye hajawahi fika anaishiaga tu somanga maana ndo kwao. Nikapiga moyo konde nikajisemea moyoni kuwa liwalo na liwe itajulikana.
Tukiwa safarini niliona kibao kimeandikwa IKWIRIRI gari likasimama kwa dakika chache nikajiuliza kulikoni tena kumbe Kuna wa mama walisimamisha wakapanda lakini cha ajabu walikuwa wananuka shombo ya samaki na mabeseni yao. Kuna mmoja alikuja kusimama karibu yangu nikamuuliza kama Ana samaki akasema Sina mwanangu samaki zimeisha. Nikakausha huku mawazo ya kwenda nisipopajua yanakuja nakunikosesha raha kabisa. Mungu yumwema baada ya dakika chache nilipata usingizi mzito sana hii nikutokana na siku ya jana kutokupata usingizi wa kutosha namm kulala Kwangu nikupumzisha mawazo. Nilikuja kushtuka kutokana na makerere mengi yawafanyabiashara wadogo wadogo hususani wanaouza biskuti, korosho, mahindi ya kuchoma na kadharika, kuangalia pembeni dogo simuoni niliyeambiwa nimwangalie nikasema kulikoni tena nikaamka chapu kwenye siti nikaenda kumuuliza konda dogo niliekaa nae yuko wapi??. Konda akasema nina mambo mengi kaka huyo dogo ni yupi? Nikamwambia nilikuwa nimekaa nae siti moja mm nikalala lakini cha ajabu simuoni konda akasema keshashuka. Nikamuuliza kwani somanga tumepita maana mm ni mgeni konda akasema nipande kwenye bus hapo tulipo ndosomanga yenyewe na dogo kashapokelewa na wazazi wake tayari.
Nikapanda kwenye gari. Bus likaiacha somanga na safari ya kwenda kilwa ikawa imewaka moto, niliona bus limejaza wa mama ambao walikuwa wanauza samaki kwenye bus. Kwa kuwa nilikuwa na njaa sana nikasema hapa samaki ni bei sana nilifanya mistake kutokununua muhindi wa jero somanga anyway nitauliza kama ana samaki hata wa buku mbili hata kambale nitatafuna usabato nauweka pembeni.
Nikiwa nasubiri afike Kwangu yule mama muuza samaki nikawaza wale wa mama wa mwanzo waliopandia IKWIRIRI kwani ni tofauti na hawa? Mbona siwaoni? Pembeni Kuna mzee mmoja alipandia somanga kwahiyo tukawa siti moja nikamuuliza akasema wale kwao ni somanga IKWIRIRI huwa wanaenda kuuza samaki wakiisha wanarudi somanga, nikasema hapo Sawa
Mama muuza samaki akawa amefika Kwangu nikamwambia sogeza beseni nichague mwenyewe mama akasogeza beseni la samaki nijichagulie.
Kucheki kwenye beseni niliona samaki wakubwa tupu Aina ya kibua na Changu. Nikajisemea moyoni hapa nimetoka patupu hawa samaki bei yake siiwezi lakini acha tu nimuulize ni bei gani akitaja nimlushe aendelee kuwauzia wengine. Yule Dada akasema samaki ni buku buku. Nikasema ebu rudia tena? Akasema kaka bei haipungui samaki mmoja ni elfu moja. Jamani sikuweza kuamini samaki mkubwa ambae Dar Es Salaam ni 7000 somanga anauzwa buku. Nikasema hapa ndopenyewe nikamwambia anifungie samaki wa buku mbili. Nikachagua samaki wangu huku nikiwa na tabasamu la kusahau shida kwa dakika chache nitakazotumia kumnyanvua samaki na minofu yake. Mama akachukua samaki akawafunga kwenye gazeti na kumimina chumvi kiasi. Kwa kua biashara ni cash to cash basi ikabidi nitoe wallet nimpe pesa yake. Ningaingiza mkono mfuko wa nyuma sikuona wallet nikasema ivi kumbe nimeweka mfuko wa mbele kuangalia mfuko wa mbele wallet hakuna, nikasema nini tena nikaangalia mifuko yote Hola jasho jembamba likianzaga tu kunitoka ujue kweli. Yule mama akasema napitia nikamwambia Sawa aendelee tu kuwauzia abiria wa nyuma akianza kurudi atapitia...
Ikabidi niangalie chini ya seat huenda imedondoka yani Sasa mpaka mwili ukawa unatetema kichwa hakipo sawa na wale samaki nikawadondosha chini kwenye abiria huwa wanapita tukiwa tumekaa.
Nikasema hapana sio kweli wallet imeenda wapi?? Ilibidi nipaniki nikamnyanyua yule mzee tukiokuwa tumepanda nae mzee alivyoniona tu kuwa sipo Sawa nikaona akasimama nikawa naangalia kila Engle ya seat lakini sikupata wallet yangu yenye pesa zangu. Abiria wa pembeni yangu wakaniuliza kulikoni nikawaambia kilichotokea wakaishia tu kunipa pole. Nikajisemea labda nikiweka kwenye begi? Lakini sio kweli maana mpaka begi linawekwa kwenye boot la bus nilichomoa pesa yangu nikiwa ndani ya bus nikanunua maji tukiwa mbagala rangi tatu. Nikiwa nimechanganyikiwa nikasikia konda anatangaza kijiji flani jina nimesahau Kuna jamaa yupo nyuma akasema kwa sauti "shusha" konda akamwambia asogee mbele maana washafika ikumbukwe kuwa Ile misamaki kipindi nasechi wallet yangu nilidondosha chini ya tule tunjia twakupita abiria, jamaa aliekuwa anashuka akapiga akazikandamiza na American buti zake samaki zote zikawa chapati tena zikagandamana na kapeti la bus. Ile nasema we jamaa umekanyaga samaki zangu akajibu kwa hasira hapo ndobakuli ilipo samaki unazibwaga njiani, ikabidi ninyamaze Sasa nikawa sipo Sawa kabisa maana wallet siioni samaki sijalipia na mama ndohuyo anakuja kutoka nyuma kudai pesa ya samaki shilling 2000 na samaki zimekanyagwa hazitamaniki kiasi ambacho hata paka hawezi kula.
....itaendelea.......