Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Hao waliokusaidia hapo Kijenge walikuwa ni ndugu zako?

Inaonekana ndugu yako wa Dar hakuwa muaninifu eeeh?

Kimsingi hawakua ndugu ila walikua wanafahamiana na huyo ndugu yangu aliyetakiwa kunipatia pesa. Ilikua tukutane nae Arusha tuende nae Moshi.

Hapo Kijenge nilikutana na jamaa wakanielekeza Kwa hao walionisaidia, wanaishi Njiro. Kumbuka nimetembea bila kujua naelekea wapi nikatokea Kijenge, nikaona kibao Cha kanisa la Lutheran, kwenda pale nikaulizia Kwa hao walionisaidia nikaambiwa wapo Dar ( walikua na shughuli pamoja na huyo ndugu yangu Sasa). Lakini mie sikupewa taarifa, vinginevyo ningeenda Dar Kisha Moshi.

Hata wao walishangaa nimepajuaje huko Njiro ila walifurahi.

Ndugu yangu sio kwamba hakua mwaminifu, alijisahsu kunipa taarifa za mabadiliko ya mipango yetu. Kumbuka hata simu sikuwa nayo. Nilikua natembea na vocha za TTCL, ukiona kibox unaiingiza namba unapiga.

Walivyomaliza, akawakabidhi wale jamaa pesa, wakaniletea nikanunue vitu huyoo Moshi.

Hapo katikati sijaelezea nilienda Arusha Technical College Kuna jamaa tumetoka nae Kijiji kimoja, nikaambiwa hajafika Bado. Niliona Giza. Nashukuru Mungu nilishindwa kukaa Kule Njiro, ukiamka asubuhi unaletewa chai, unakula, haufanyi kazi yeyote ni kwenye TV tu. Nikarudi College Bahati nzuri jamaa akawa ameripot nilikaa huko hadi siku naenda kuchukua pesa Njiro, kununua vitu na kuelekea shule.

Huyo jamaa wa College Mungu aendelee kumbariki, alikuja pitia mitihani namshukuru Mungu alinipa nafasi ya kufanya chochote ( nikiwa nimeshaanza kazi). Bahati nzuri na yeye Yuko Dar siku hizi tumekua kama familia Moja.

Maisha Yana mambo mengi sana
 
Kimsingi hawakua ndugu ila walikua wanafahamiana na huyo ndugu yangu aliyetakiwa kunipatia pesa. Ilikua tukutane nae Arusha tuende nae Moshi.

Hapo Kijenge nilikutana na jamaa wakanielekeza Kwa hao walionisaidia, wanaisgi Njiro. Kumbuka ninetembea bila kujua naelekea wapi nikatokea Kijenge, nikaona kibao Cha kanisa la Lutheran, kwenda pale nikaulizia Kwa hao walionisaidia nikaambiwa wapo Dar ( walikua na shughuli pamoja na huyo ndugu yangu Sasa). Lakini mie sikuoewa taarifa, vinginevyo ningeenda Dar Kisha Moshi.

Hata wao walishangaa nimepajuaje huko Njiro ila walifurahi.

Ndugu yangu sio kwamba hakua mwaminifu, alijisahsu kunipa taarifa za mabadiliko ya mipango yetu. Kumbuka hata simu sikuwa nayo. Nilikua natembea na vocha za ttcl, ukiona kibox unaiingiza namba unapiga.

Walivyomaliza, akawakabidhi wale jamaa pesa, wakaniletea nikanunue vitu huyoo Moshi.

Hapo katikati sijaelezea nilienda Arusha Technical College Kuna jamaa tumetoka nae Kijiji kimoja, nikaambiwa hajafika Bado. Niliona Giza. Nashukuru Mungu nilishindwa kukaa Kule Njiro, ukiamka asubuhi unaletwa chai, unakula, haufanyi kazi yeyote ni kwenye TV TU. Nikarudi College Bahati nzuri jamaa akawa ameripot nolikaa huko hasi siku naenda kuchukua pesa, kununua vitu na kuelekea shule.

Huyo jamaa wa College Mungu aendelee kumbariki, alikuja pitia mitihani namshukuru Mungu alinipa nafasi ya kufanya chochote ( nikiwa nimeshaanza kazi). Bahati nzuri na yeye Yuko Dar siku hizi tumekua kama familia Moja.

Maisha Yana mambo mengi sana
Kabisa, umeshajipatia rafiki.
 
Dah! Ukiona mtu anaomba lift Kwa Bodaboda ujue kweli Yuko serious, nimejikuta nacheka na kuhuzunika Kwa pamoja.

Kwamba ukiwa hauna pesa unajulikana tu.

Hii stori inanikumbusha siku naenda kuanza kidato Cha sita Moshi nikitokea Kanda ya kati kupitia Arusha, sitasahau maishani mwangu. Nimefika Arusha nikalala kesho yake nikutane na ndugu yangu anaetokea Dar kuniletea pesa za ada na matumizi, kumpigia Kwa zile box za ttcl, ananiambia nishushe Dar, hatoweza kuja Arusha...hapo nna pesa ambayo nililala guest tu, nakosa nauli ya kwenda Dar

Niliadhimia kulala nje ili nibanie pesa ya kulala guest inisaidie nauli kesho yake. Nikadhania stand ya Arusha watu wanakesha ili nijumuike nao Hadi asubuhi, kumbe pale watu hawakeshi. Nikajitutumua nikapiga kahawa kutoa usingizi na kupunguza machungu ya baridi.

Watu walianza kupungua nikabaki peke yangu, nikawa nakatiza mitaa kama ntabahatisha sehem kijiwe nikeshe, wapi. Ikafika mahala nakutana na polisi wa doria na mbwa, nikaona hapa ntaishia lockup.

Ilipofikia saa nane kasoro usiku, nimepigwa na baridi, nilivaa t-shirt tu, nikafanya maamuzi ya kutafuta guest house nilale, sikuwaza Tena mambo ya nauli. Nilihangaika sana guest zilikua zimejaa. Nikaja kupata njia ya kuelekea Ilboru. Ilibaki chumba kina vitanda vitatu, Kwa hasira nililala Cha kwanza, nikaenda Cha pili, nikamalizie Cha tatu, wakati naingia yule Mama mhudumu ananiambia Kuna maji ya kuoga ya moto, sikumbuki nilimjibu kitu Gani lakini sikuoga Wala kutoka Tena Hadi asubuhi.

Kesho yake Nimeenda stand, nauli Sina, nawaza niongee na makondakta nikifika Dar niwasiliane na ndugu niletewe nauli niwaachie bag. Kila nikiwaza Hilo Wazo ujasiri unaniishia, sikuweza kuondoka. Nikaamua kuwa mtalii natembea bila kujua naelekea wapi, nilijikuta Kijenge huko ndio muujiza wangu ulipokua. kilichotokea Mungu alikua na makusudi yake.

Ni kitu kimenifanya Hadi Leo mtu akiniambia ana shida/ tatizo nimsikilize Kwa kutulia.

Sikwenda Dar nilipotakiwa kufuata pesa za ada na matumizi, nilijikuta nimefika sehem sahihi hapo hapo Arusha, nikaambiwa nisubirie ntaletwa Kila kitu kabla ya kuelekea shule Moshi. Nilikua naambiwa ingia ndani, naogopa nataka nikae chini. Yaani matatizo yaliyonipata na zile shida naona kama Kila mtu anajua yaliyonipata na hadhi yangu sistahili hata kuingia kwenye nyumba ya watu.

Jioni najifanya kuaga utafikiri nna pakwenda, ndio nikaambiwa tumeambiwa usiondoke Hadi utakapoletewa vitu vyako.

Mwisho, ukipata nafasi ya kumsaidia mtu Kwa namna yeyote Ile, na ukaona kabisa unapata msukumo moyoni mwako, Fanya hivyo. Usijiulize maswali mengi sana ( sikiliza moyo unasemaje) akikutapeli mwachie Mungu tu, itakua umefanya Kwa nafasi Yako.
mkuu maisha yana chapter mpya kila sekunde.

mimi mara kwa mara nakutana na watu wananiomba nauli,huwa natoa kabla hata hajamaliza story yake,maana kufubazwa na shida nakujua.
 
Kabisa, umeshajipatia rafiki.

Yeye hajui Ile kunihifadhi Arusha chuo alinisaidia kiasi Gani. Sikumwambia Mikasa niliyopitia hua anashangaa kwanini nathamini sana hicho kitendo wakati pale chuo ni kawaida tu mtu kwenda.

Nikajifunza jambo lingine, unaweza kumpatia mtu 5,000/- au 10,000/- ukaona SI kitu kumbe Kwa wakati huo, huyo uliyemsaidia anaona umemvusha pakubwa sana.
 
Inawezekana maana kuna wayahudi walikuwa wamewekwa kwenye kambi wakisubiri kuuawa, walikuwa wamechanganywa na wanawake ila wakawa wanapigana mambo

Halafu pia jamaa alikuwa katumiwa 20k na mzee wake, alikuwa amehakikishiwa kupata chakula na sehemu ya kulala kwa siku kadhaa, so stress zilikuwa zimeshuka kiasi cha kutosha kuwa na nyege [emoji23][emoji23]
[emoji16][emoji16]
 
-------SEHEMU YA KUMI NA MBILI - - - - - -

Mkuu wa shule pamoja na makamu wakaniambia niondoke mda huo kwahiyo ilinibidi niingie chumbani nikachukua begi langu haraka nikaliweka begani nduki. Nadhani walifanya haya pia kumridhisha madam asije kuona wapo pamoja na mimi, yani nimeonekana ni mharifu halafu bado wanaendelea kunipa hifadhi? Wakaona kudumisha umoja walio nao kama walimu nikulivaa hili tatizo kama Lao kwahiyo wakaamua kunitimua. Nikaenda mwambaoni mwa barabara Ile ya vumbi nione wapi pakuanzia Sema shida baridi ilikuwa inaniponda sana ila njaa sikuhisi tena kutokana na situation niliyonayo kwa mda huo hata ningepewa kuku wa KFC nisingemla. Nikaona hapa nikielekea kwenda kule kijijini center sipati msaada wowote ule tena baadhi wakiniona usiku huu wanaweza hata kumpigia simu mkuu wa shule kuwa yule kijana ulokuja nae mchana kula Wali njugu mbona yupo huku usiku huu na begi kama kafurushwa, kwa hiyo mambo yangeweza kubumburuka nikaona ngoja niambae hiihii barabara ya vumbi kwenda huko mashambani maana Kadri unavyozidi kwenda magharibi ndounazidi kujichimbia ila tu nisiende mbali sana na barabara maana asubuhi hiyo gari ya MACHINGA ndohuwa inapita ili nipande niondoke huu mkoa ulionitesa vya kutosha. Ile naendelea kutembea nikaona Kuna mzee ana kirungu anasurvey maeneo ya shule nilivyomuona nikapozi kidogo nikamsalimia akaja karibu nikakumbuka kumfahamu kumbe ni mlinzi wa hii shule.

Ikabidi huyu mlinzi ni muulize hii barabara ya vumbi iliyonyooka kama Kuna gari lolote huwa linapita asubuhi akasema ndio ni gari ya MACHINGA inatoka nachingwea kwenda Dar Es Salaam akasema lakini mbona usiku huu na mizigo kwanini nisingesubiri mpaka asubuhi? Ile anauliza tu kumbe wale walimu walikuwa wanatuzoom nikasikia sauti inasema ahse we kijana tulikwambiaje? Ondoka maeneo haya we mpumbavu ivi kwanini huelewi, nikaona yule mlinzi anasema kumbe wewe ni mharifu itakuwa basi ondoka hapa nenda sehemu yoyote ila mbali na eneo langu la kulinda yani maeneo ya shule. Nikipindi ambacho nilikuwa nakataliwa na kila Aina ya watu kwakweli niliteseka sana. Ikabidi niondoke kabisa kwenye yale mazingira nikaanza kupiga mguu kuambaa hiyo barabara ya vumbi mpaka nitakapoona ni salama Kwangu nitapumzika, nilitembea sana kwa kweli umbali mrefu mno japo nilibahatika kupishana na pikipiki nilisimamisha hakusimama baada ya masaa mawili hivi nikiwa bado natembea nilijihisi mgongo unauma sana nikasogea pembeni kupumzika ila shida ya kule udongo ni mwekundu sana kwahiyo nikaona nitafute sehemu yenye majani au gongo kubwa nikae na kupumzika kabisa.

Nilipoingia kwenye kichaka nikatulia zangu huku nikimwomba Mungu asamehe yote niliyotenda maana binadamu anasamehe tu makosa lakini Mungu anasamehe dhambi. Nimekaa zangu kwa mbali niliona Kuna moto unawaka nikasema nini kile tena?, nikawaza sana nikaona uoga niuweke kapuni acha nifate moto uliko huenda nimakambi ya watu either mashamba au wafugaji. Na kweli nilipofika umbali wa mita tano hivi nikasalimia kwa nguvu wakaitika nikawaomba nisogee wakasema stooooop wewe nani na unataka nini? Kwa sauti imeambatana na uoga nikasema mimi Mpwayungu village nimetoka mbali sana nahitaji kesho asubuhi nichukue usafiri wa kwenda Dar es Salaam huku mimi ni mgeni naombeni nije niongee kilichonikuta, walisita kidogo wakaongea kilugha kwa dakika moja hivi Kisha wakasema karibu. Naomba muelewe kuwa nilipoona huu moto nilidhani upo karibu lakini kumbe ni mbali sana na barabara halafu nilipita kwenye mamisitu flani hivi sema tu Ile misitu sio mikubwa sana huenda pia kwa sababu ya kutokuwa na uoga mkubwa kama mwanzo ndokilifanya nizidi kwenda mpaka kwenye ule moto lakini ni umbali almost wa dk 45 kuufikia nadhani macho yangu yalikuwa makali sana kuuona. Niliposogea tu pale kitu cha kwanza kuona ilikuwa ni panga mbili na nyama ilikuwa inachomwa nadhani alikuwa digidigi. Wale Majamaa kwa ukaribu kabisa ndipo nikagundua sio wenzangu, kwanza sura zimepondeka kinyama wanaweza kula hata ugali kwa picha ya samaki, japo yale mapanga yalikuwa yamelowa damu lakini sikuogopa sana maana nilijua ni damu ya yule mnyama waliokuwa wanamchoma.

Nikaa kwenye gongo moja hivi wakaanza kunihoji nikaona jamaa mmoja hivi mwembamba akachukua begi langu nakuanza kupekua kimoja baada ya kingine mbaya zaidi zile nguo akawa anaziweka chini kung'uta kila kitu, mm nilikuwa mkimya sana zaidi ya maji ya kwenye mtungi alipomaliza akazibeba nguo na mabahasha kwa mkupuo nakuyashindilia kwenye begi. Nikajisemea moyoni hapa wakija tu kunipiga sachi kwenye mifuko hizi njema haziachi hii 25000 maana haya majambazi nimeingia cha kike. Bahati nzuri hawakunikagua kwenye mfuko wangu wa suruali Kisha wakasema kijana kuwa na Amani nikawapa Asante za kutosha nikapiga goti wakasema haina shida wewe kaa tu, Nikaa tukaanza kupiga soga mbili tatu huku wakiendelea kunywa kinywaji nadhani ilikuwa ni pombe zao za kienyeji. Yule jamaa aliekuwa anasacha begi langu sikuona vizuri pembeni Kuna nini Kuja kuona kumbe ilikuwa ni bunduki Aina ya SMG niliijua maana nimepitia JKT kwa mujibu wa sheria. Nikasema haya majangili haya maana hata nyama ilivyokuwa inachomwa niyapolini. Tulikaa sana baada ya masaa mawili hivi yaani kwenye saa tisa usiku Ile nyama yakawa yanaikata kwa panga ikiwa humo kwenye moto huku yanakula, yakasema kijana chukua panga ukate nikaona nikikataa nitajenga taswira mbovu ngoja niliunge.

Nikachukua panga namimi nikate nyama ila haitoki kwenye moto, halo nyama ilikuwa ya moto hatari Ile kuishika tu nilikutana na huo moto unaunguza na nyama inaunguza ila nilijitahidi kuikata japo kwa mbinde sana nikakata bonge la pambe ili nisijisumbue kukata tena, kimsingi ilikuwa ni tamu sana japo sikujua ni aina gani ya nyama. Wale Majamaa nikaona ghafla wamekaa kimya kukata Ile nyama hawakati na pombe hawanywi yani wakawa kimya ghafla tu kwa pamoja mwishowe yule jamaa mwenye bunduki nikaona kaishika kijasiri sana tena kwa haraka japo kwa ukimya, nikasema wanataka kunishuti nini. Nikaona yule jamaa anawaambia wenzake tuondokeni kwa hiyo zile panga mbili mmoja akachukua panga moja na mwingine panga moja wakabeba na vifaa vingine na vimizigo vyao wakasepa wakasema kijana sisi tunaondoka kwaheri. Ni usiku wa saa tisa na nusu nikawa peke angu kwenye ule moto ila niliogopa sana dakika sifuri mwili wote ulilowa jasho nikajiuliza Kuna nini kinakuja nyuma mpaka hawa watu wameondoka ghafla hivi. Nikasema potelea mbali acha waniue kama ndolengo Lao au kama Kuna kitu kinakuja nipo tayari, nikabeba begi langu chapu kwa haraka Ile kugeuka tu niliondoka nduki kuelekea barabarani nilikimbia sana mwishowe miguu ikakosa stamina nikadondoka chini kama gunia puuuh!. Nikaamka tena nikakimbia ghafla nilishtuka nipo barabarani. Kilichonifanya niondoke pale ni jinsi ya hawa watu walivyoondoka pia mwonekano wao ulionekana criminal nikajua tu hawa ni Wanted maana sura zote Zina majeraha Kuna mmoja nilishuhudia alipokuwa anakata nyama alikuwa hana vidole viwili kwenye mkono, mwingine ana bonge la ngewe kwenye paji la uso. Hivyo nikajiongeza tu kuwa hapa sio salama naukizingatia mm ni mtu wa majanga kama nimelaniwa na wazazi vile.

Nilifika pembezoni mwa Ile barabara ya vumbi ambayo niliambiwa gari ya MACHINGA asubuhi itapita nipande kwenda Dar Es Salaam. Nilikuwa nahema halafu sijiamini, nikafanya maamuzi ya haraka ya kupanda juu ya mtu. Nilipanda kwenye mti flani upo ndani kidogo ya Ile barabara ila haukuwa mkorosho. Nilipopanda nikashikilia moja ya tawi ambalo ni nene sana nikatulia tuli japo mapigo ya moyo yalizidi kuongezeka. Sikulala kabisa nikaona Kuna kisehemu naweza kupachika begi langu nikaweka lile begi nikaona limekaa vizuri hivyo nikawa mvumilivu zaidi ya askari waliojenga ukuta wa mererani wakiahidiwa ajira, usiku ulikuwa ni mzito sijawahi ona halafu nilikuwa nashtukashtuka tu bila sababu za msingi ilifika kipindi mpaka mti niliokwea nikawa siuamini. Mungu ni mkubwa nikaona panapambazuka ilinibidi sasa nishuke haraka kujongea taratibu mpaka hapo barabarani na hapakuwa mbali sana na pale nilipoenda kukwea juu ya mti.

........ Inaendelea usichoke.......
 
Hii stori inanikumbusha mbaali sana, nishalala sana kwenye miti na chini ya mabua ya mahindi' haya maisha ni tatizo sana!
 
Kiakili ya kawaida tu haiwezekani vibaya wakuweke chini ya ulinzi alafu wote wakuache ukiwa uko peke yako waende kwa mademu,lazima angekuepo mtu wa kukusimamia.

Alafu pili waende kwa hao wadada kuwasalimia kivipi wakati walikuwa wanakuja hapo hapo.

Alafu tatu ulitokaje nduki kali wakati ulikuwa na begi zito ambalo usingeweza kukimbia sana bila wao kukukamata.

Alafu nne vile vyeti walivyovitoa kwenye begi walivirudisha kabla ya wewe kukimbia na begi au vipi.

Ila mimi naifatilia stori kwa sababu inasisimua,ya ukweli ama sio ya ukweli hiyo hainihusu.
Enjoy story
 
Yeye hajui Ile kunihifadhi Arusha chuo alinisaidia kiasi Gani. Sikumwambia Mikasa niliyopitia hua anashangaa kwanini nathamini sana hicho kitendo wakati pale chuo ni kawaida tu mtu kwenda.

Nikajifunza jambo lingine, unaweza kumpatia mtu 5,000/- au 10,000/- ukaona SI kitu kumbe Kwa wakati huo, huyo uliyemsaidia anaona umemvusha pakubwa sana.
Kabisa! Ukifanikiwa usimsahau huyo jamaa.
 
Back
Top Bottom