Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,637
- 47,413
Watoto wadogo hawawezi kuelewa msoto ulivyo. Wao daily ni story za kula tunda kimasiharaWatoto laini laini watasema hii chai, ila tuliopitia maisha haya tunamuelewa sana mleta uzi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watoto wadogo hawawezi kuelewa msoto ulivyo. Wao daily ni story za kula tunda kimasiharaWatoto laini laini watasema hii chai, ila tuliopitia maisha haya tunamuelewa sana mleta uzi
Hii Tecno F1 unayotumia ni ile mpwayungu aliiuzaga nini
Hata Mimi yangu nitaleta japo no ya kitambo nasubiri tu MacBook iponeWatoto laini laini watasema hii chai, ila tuliopitia maisha haya tunamuelewa sana mleta uzi
Una roho mbaya watu wa kilwa wakasomeIshia hapa hapa. Andika kitabu au anzisha group telegram watu wajiunge kwa kuchangia....
Soma vizuri acha papala, nimesema nilitembea umbali wa dk 45 nilipokaribia kufika kabisa walipokaa nikaona kusogea zero distance nawalipo ni hatari ilibidi nisimame Mita tano kutoka hapo walipokaa yani kabla ya kufika exactly position. Ndipo wakawahi kusema stoooop. Nilipojitambulisha wakasema haya njoo ukaeUnawezaje kupaza sauti kwa umbali wa kutembea kwa mguu kwa dakika 45 na mkawaelewana.? Anyway, next episode.......
Wachina huko makete mnafuata Nini,au ulikuwa unafundisha karateStori ya jamaa imenifanya niende nikafukue ofisini namba ya simu ya dada fulani pale makete ili nimlipe fadhila, bahati mbaya namba alishapewa mtu mwingine.
Imagine huyu dada nilifika pale makete nilikuwa sina hata mia na ishakuwa jioni. Nikaenda gesti kwa sababu chimbo nililopanga kulala palikuwa na baridi kali sana. Yule dada mhudumu wa gesti nilivyoanza kumpiga sound tu akanikatisha, akasema usiendelee kuongea akasema nifate.
Akanionesha chumba nililala bure kabisa nilipewa na maji ya moto japo sikuoga.
Wanaume tunapitia mengi jamani asikwambie mtu.
Soma vizuri..alipaaza sauti baada ya kukaribia..Unawezaje kupaza sauti kwa umbali wa kutembea kwa mguu kwa dakika 45 na mkawaelewana.? Anyway, next episode.......
Ni ID tu mkuuWachina huko makete mnafuata Nini,au ulikuwa unafundisha karate
Du..mwandishi mzuri sana!Tarehe 4 mwezi wa pili 2020 nikiwa katika msongo wa mzito wa mawazo yaliyotokana na ugumu wa maisha nilijikuta nafanya maamuzi magumu bila kutarajia. Nilikuwa nakaa gheto maeneo ya buguruni sheli japo gheto lilikuwa na mshikaji wangu ambae tulisoma nae primary mawenzi shule ya msingi iliyopo moshi mjini mwaka 2006 ndotulimaliza darasa la saba hapo.
Nikiwa nimelala saa sita usiku naona napigwa mgongoni kwa nguvu kuamka namuona rafiki angu tunaelala chumba kimoja pia ndommiliki wa gheto mm kaniweka tu kishkaji, nikasema kulikoni jamaa akajibu kiunyenyekevu akisema "oya demu wangu kafukuzwa na Dada ake alipokuwa anakaa kwahiyo hana pakwenda nasaizi ni saa saba usiku amekuja yupo hapo kibarazani anataka tulale humu kwahiyo please wewe ni mwanaume ebu tafuta ustaraabu wa kuondoka saizi ukija asubuhi tutaweka mambo Sawa ".
Nikamwambia sasa mda huu mm niende wapi ndugu na Sina hata sehemu yakujiegesha!? Akajibu nitajua mwenyewe, ikabidi nivae niende kimboka night club kupoteza mda nikawa naangalia movie kwenye mabanda ya pale kimboka maana majamaa huwa hawalali. Ilipofika asubuhi nikatia timu bahati nzuri nikakuta wote wameamka ila wapo kitandani nikamsalimia shemeji pamoja na jamaa angu japo hawakuonesha uso wa tabasamu walikuwa serious kiasi ambacho nilishindwa kuwaongelesha.
Nilipotazama juu kwenye enga zakuwekea nguo zangu ghafla sikuona nguo yoyote, nilipouliza jamaa akasema nimekuwekea kwenye begi ili ukija usisumbuke kuzipanga maana shemeji ako kasema yeye hatoki atakaa hapahapa sasa hatuwezi kulala watatu. Ilikuwa ni kipindi kigumu sana Kwangu zaidi ya Alpha konde alipotolewa madarakani. Nikatazama juu chini nikawaza nikasema haina shida.
Nikabeba begi langu nikawaaga wakasema kila raheli. Nilikuwa na simu Aina ya tecno F1 na mfukoni nikawa na 20000 nikasema Poteleapote nitaenda popote pale kutafuta rudhiki.
Kwa pesa niliyokuwa nayo kukaa Dar Es Salaam hapakunifaa tena, hiki ndokipindi ambacho mikoani unapaona nafuu kuliko jiji la Dar Es Salaam. Nikiwa na begi langu Zito la nguo mpaka mida ya saa kumi jioni nilikuwa sijajua niende wapi na nitalala wapi. Nilipoona mda unakwenda ilibidi nimfate jamaa mmoja ivi yeye anauza nguo za jinsi buguruni sokoni kama unaenda shell nilipofika alinichangamkia akijua ni mteja kumbe ni mtu mwenye dhiki aliehitaji msaada. Sikupoteza mda ilibidi nimwambie ukweli yote yaliyotokea ila msaada wangu mkubwa ilikuwa anitafutie mteja wa kununua simu yangu.
Akasema nauzaje nikamwambia simu nauza 90000 tu jamaa akasema ngumu kupata mteja leoleo Sema ngoja nimpigie simu Dada mmoja anauza chakula Ana shida sana na simu kubwa. Yule dada akaja alivyoiona na alivyokuwa na pupa ya kumiliki smart phone nikajua tu huyu ni mteja. Jamaa akasema niongee nae ilibidi nimwambie nauza laki moja maana ngozi nyeusi ukitaja bei harisi ushahalibu. Yule Dada akasema ana 80000 nikajifanya nakataa akaongeza 5000 nikamwambia toa pesa akanipa nikampa simu akaagana na jamaa akaondoka. Sasa kimbembe kikaanza Kati ya mm na huyu Dalali.
Jamaa nikampa 5000 akasema niache utani inabidi nimpe 20000 nikacheka kidogo huku mdomo ukiwa umekauka maana mpaka jua lilizama sijapata chochote cha kuchezesha kinywa changu.
Nikamwambia 20000 hapana kutokana na shida niliyonayo jamaa akasema vinginevyo anamwambia yule dada hii simu ya uwizi arudishe. Nikaona isiwe tabu nikampa 10000 nikasema hutaki naondoka na pesa sirudishi maana ilibidi nikunje sura vinginevyo nitakwama. Jamaa akapokea.
Alipopokea Ile pesa nikapotea mda huohuo. Sasa kimbembe nipakulala maana ikawa ni usiku huku nikiwa nimechoka sana. Nikaingia bar moja ivi inaitwa sewa. Nikaongea na muhudumu akasema Vyumba kwanzia saa saba usiku mdaa huu ni short time. Kwa kuwa nilikuwa na shida nikavumilia Ilipofika saa saba nikawa hoi kweli kweli nikiwa nimekaa kwenye kiti huku bar ikiwa imefungwa yule muhudumu akaja akasema kaka pole nenda kalale chumba hicho apo. Akasema nimpe 4000 tu maana naonekana sipo sawa. Nikampa pesa yake Nikaingia kulala japo madadapoa walikuwa wanagonga sana mlango niwafungulie lakini sikujali.
Asubuhi kukapambazuka nikasema leo inyeshe mvua liwake jua sikai Dar. Mm nimemaliza kidato cha sita ila sikubahatika kuingia chuo kikuu lakini najua sana kufundisha. Nikasema hapa ngoja nikatafute kibarua cha kufundisha mikoani ila tu isiwe dodoma. Nikawaza sana nikasema hapa safari ni kwenda lindi. Nikachukua daladala mpaka mbagala, ilikuwa saa sita mchana, kufika pale wakasema mda huu Gari za lindi mpaka temeke hapa mbagala ipo gari ya kwenda kilwa mda huu inaitwa MASHALAH.
Kwasababu kichwa changu mda huo hakikuwa sawa nikasema nikate tiketi tu hata ya kwenda kilwa nitajua mbele ya safari. Wakasema nauli Dar mpaka kivinje ni 11000 halafu Dar mpaka kilwa ni 13000.
Saa sita na nusu tukawa tumeondoka Dar Es Salaam kuelekea kilwa nikiwa Sina ndugu wala yoyote anaenijua lakini nikiwa na Amani ya moyo kwakuwa kilwa sio sudani wala Uganda ni Tanzania pia.
Inaendelea...
Safari ya kuelekea Kilwa ikaanza. Nililipa nauli ya Dar Es Salaam to Kilwa shilling 13000 mfukoni mpaka na panda bus nikawa nimebakiwa na 70000 tu kutokana na pesa nyingine Jana usiku Nililipa gest 4000 asubuhi kabla ya kwenda kukata ticket nilienda saloon kunyoa kwa 2000 baadhi ya pesa nilikula mihogo na maji ya kunywa njiani. Ubovu nikuwa kwenye siti nilikuwa nimekaa na mtoto mdogo wa kike ambae alipakiwa na mzazi wake ila yeye huyo mzazi hakuwa anasafiri sasa akaniambia kuwa nimsaidie kumwangalia lakini pia konda alikuwa amepewa taarifa kimsingi ni mtoto ambae huenda ni miaka 11 au 12 huyu dogo yeye alikuwa anashukia somanga. Kwahiyo nikakosa hata msaada wa kuanzia nikifika kilwa itakuwaje maana nilikuwa nategemea labda mtu nitakae kaa nae atanipa mawazo namna ya mji ulivyo na jinsi ya kuhendo swala langu. Tukiwa safarini ilibidi nimuulize huyu dogo endapo anaijua kilwa ili tu nipate pakuanzia dogo akasema yeye hajawahi fika anaishiaga tu somanga maana ndo kwao. Nikapiga moyo konde nikajisemea moyoni kuwa liwalo na liwe itajulikana.
Tukiwa safarini niliona kibao kimeandikwa IKWIRIRI gari likasimama kwa dakika chache nikajiuliza kulikoni tena kumbe Kuna wa mama walisimamisha wakapanda lakini cha ajabu walikuwa wananuka shombo ya samaki na mabeseni yao. Kuna mmoja alikuja kusimama karibu yangu nikamuuliza kama Ana samaki akasema Sina mwanangu samaki zimeisha. Nikakausha huku mawazo ya kwenda nisipopajua yanakuja nakunikosesha raha kabisa. Mungu yumwema baada ya dakika chache nilipata usingizi mzito sana hii nikutokana na siku ya jana kutokupata usingizi wa kutosha namm kulala Kwangu nikupumzisha mawazo. Nilikuja kushtuka kutokana na makerere mengi yawafanyabiashara wadogo wadogo hususani wanaouza biskuti, korosho, mahindi ya kuchoma na kadharika, kuangalia pembeni dogo simuoni niliyeambiwa nimwangalie nikasema kulikoni tena nikaamka chapu kwenye siti nikaenda kumuuliza konda dogo niliekaa nae yuko wapi??. Konda akasema nina mambo mengi kaka huyo dogo ni yupi? Nikamwambia nilikuwa nimekaa nae siti moja mm nikalala lakini cha ajabu simuoni konda akasema keshashuka. Nikamuuliza kwani somanga tumepita maana mm ni mgeni konda akasema nipande kwenye bus hapo tulipo ndosomanga yenyewe na dogo kashapokelewa na wazazi wake tayari.
Nikapanda kwenye gari. Bus likaiacha somanga na safari ya kwenda kilwa ikawa imewaka moto, niliona bus limejaza wa mama ambao walikuwa wanauza samaki kwenye bus. Kwa kuwa nilikuwa na njaa sana nikasema hapa samaki ni bei sana nilifanya mistake kutokununua muhindi wa jero somanga anyway nitauliza kama ana samaki hata wa buku mbili hata kambale nitatafuna usabato nauweka pembeni.
Nikiwa nasubiri afike Kwangu yule mama muuza samaki nikawaza wale wa mama wa mwanzo waliopandia IKWIRIRI kwani ni tofauti na hawa? Mbona siwaoni? Pembeni Kuna mzee mmoja alipandia somanga kwahiyo tukawa siti moja nikamuuliza akasema wale kwao ni somanga IKWIRIRI huwa wanaenda kuuza samaki wakiisha wanarudi somanga, nikasema hapo Sawa
Mama muuza samaki akawa amefika Kwangu nikamwambia sogeza beseni nichague mwenyewe mama akasogeza beseni la samaki nijichagulie.
Kucheki kwenye beseni niliona samaki wakubwa tupu Aina ya kibua na Changu. Nikajisemea moyoni hapa nimetoka patupu hawa samaki bei yake siiwezi lakini acha tu nimuulize ni bei gani akitaja nimlushe aendelee kuwauzia wengine. Yule Dada akasema samaki ni buku buku. Nikasema ebu rudia tena? Akasema kaka bei haipungui samaki mmoja ni elfu moja. Jamani sikuweza kuamini samaki mkubwa ambae Dar Es Salaam ni 7000 somanga anauzwa buku. Nikasema hapa ndopenyewe nikamwambia anifungie samaki wa buku mbili. Nikachagua samaki wangu huku nikiwa na tabasamu la kusahau shida kwa dakika chache nitakazotumia kumnyanvua samaki na minofu yake. Mama akachukua samaki akawafunga kwenye gazeti na kumimina chumvi kiasi. Kwa kua biashara ni cash to cash basi ikabidi nitoe wallet nimpe pesa yake. Ningaingiza mkono mfuko wa nyuma sikuona wallet nikasema ivi kumbe nimeweka mfuko wa mbele kuangalia mfuko wa mbele wallet hakuna, nikasema nini tena nikaangalia mifuko yote Hola jasho jembamba likianzaga tu kunitoka ujue kweli. Yule mama akasema napitia nikamwambia Sawa aendelee tu kuwauzia abiria wa nyuma akianza kurudi atapitia...
Ikabidi niangalie chini ya seat huenda imedondoka yani Sasa mpaka mwili ukawa unatetema kichwa hakipo sawa na wale samaki nikawadondosha chini kwenye abiria huwa wanapita tukiwa tumekaa.
Nikasema hapana sio kweli wallet imeenda wapi?? Ilibidi nipaniki nikamnyanyua yule mzee tukiokuwa tumepanda nae mzee alivyoniona tu kuwa sipo Sawa nikaona akasimama nikawa naangalia kila Engle ya seat lakini sikupata wallet yangu yenye pesa zangu. Abiria wa pembeni yangu wakaniuliza kulikoni nikawaambia kilichotokea wakaishia tu kunipa pole. Nikajisemea labda nikiweka kwenye begi? Lakini sio kweli maana mpaka begi linawekwa kwenye boot la bus nilichomoa pesa yangu nikiwa ndani ya bus nikanunua maji tukiwa mbagala rangi tatu. Nikiwa nimechanganyikiwa nikasikia konda anatangaza kijiji flani jina nimesahau Kuna jamaa yupo nyuma akasema kwa sauti "shusha" konda akamwambia asogee mbele maana washafika ikumbukwe kuwa Ile misamaki kipindi nasechi wallet yangu nilidondosha chini ya tule tunjia twakupita abiria, jamaa aliekuwa anashuka akapiga akazikandamiza na American buti zake samaki zote zikawa chapati tena zikagandamana na kapeti la bus. Ile nasema we jamaa umekanyaga samaki zangu akajibu kwa hasira hapo ndobakuli ilipo samaki unazibwaga njiani, ikabidi ninyamaze Sasa nikawa sipo Sawa kabisa maana wallet siioni samaki sijalipia na mama ndohuyo anakuja kutoka nyuma kudai pesa ya samaki shilling 2000 na samaki zimekanyagwa hazitamaniki kiasi ambacho hata paka hawezi kula.
Wambulu wanapatikana Kanda ya ziwa ipi?Nimeielewa kitu,ni kwanini walimu hudharauliwa,kumbe ni maisha magumu
Sasa dada wa kimbulu toka Kanda ya ziwa kwenda kujichimbia mbwinde huko no hatari hii,
Bora udalali kwenye hili jiji
[emoji109][emoji109]-------SEHEMU YA KUMI - - - - - - -
Aiponiambia nirudi halafu wale wageni wakiondoka ataniita mm nikamwambia Sina simu utaniita vp? Akasema basi niwe namuuliza mara kwa mara lakini bado sikuweza kukubali kirahisi maana nikahisi labda wananichezea akili hawa japo sio kweli mpaka ilifika mda ikabidi nimuulize kwanini huyo kijana alikubali ilihali anajua atapokea wageni, mkuu alijibu kuwa hakupata mawasiliano na yeye maana huyo kijana anakaa kwenye Vyumba viwili na wiki chache alisema tukipata mwalimu chumba kipo ila baada ya hapo Jana usiku kumpa taarifa akasema anaugeni na hajui watatoka lini pale. Nilimwambia ukweli kwamba nimechukia na mdaa sielewi naenda wapi maana huku mimi ni mgeni.
Baada ya kuonyesha uso wa simanzi nikaona kachukua simu yake akampigia mwalimu mmoja hivi shule inaitwa Mwitero sekondari kama sijakosea kwa mjibu wa maelezo yake ila huyo mwalimu akasema shida ni accommodation. Akampigia tena mkuu wa shule flani inaitwa CHINONGWE SEKONDARI nikasikia anasema mwambie aje maana hapa nina mwalimu mmoja tu waphysics, nilisikia maana alikuwa ameweka loud speaker, baada ya hapo nikamwambia siendi mpaka anihakikishie asilimia mia kuwa nikifika siondoki halafu amwambie na level yangu ya elimu kuwa ni form six. Mkuu wa shule akachukua simu akampigia tena akamwambia kila kitu akasema niende.
Baada ya hapo nikiwa nimechoka sana ilibidi nimuage mkuu wa shule ya sekondari kineng'ene kuwa naondoka namtakia kila raheli. Akasema nimsamehe kwa usumbufu hivyo nikachukua namba ya yule mwalimu wa shule ya sekondari CHINONGWE nikaondoka zangu. Huyu mkuu wa kineng'ene alisema CHINONGWE sio mbali sana ipo wilaya ya RUANGWA kwakina Kassim majaliwa Kassim sikuleta ubishii kwa kuwa sipajui. Ikanibidi niende mpaka pale barabarani nikasema hapana hapa lazima Niite bodaboda kwakweli inipeleke mpaka main road yaani mtange. Kuna dogo mmoja akapita na pikipiki nikamuuliza kijanja unaenda wapi akasema mtange nikamwambia nipe lift basi dogo akasema nimpe buku tu, nikamwambia poa tuondoke. Huu mda nilikuwa na hasira za ghafla sana kutokana na mambo tu ya hovyo yanavyoniandama, mda si mwingi tukafika mtange nikashuka.
Nikataka kupanda hiace za kwenda town ili nikadake gari za kwenda luangwa lakini nikasema ngoja niulize huenda njia nihiihii. Nikamwomba yule dogo tuliekuja nae kwenye pikipiki aniazime simu yake nimpigie huyo mkuu wa shule ya sekondari CHINONGWE anipe maelekezo ya kutosha nafikaje huko. Nikapiga simu akasema shule ipo wilaya ya RUANGWA lakini nisipande Costa zakwenda huko maana shule ipo mbali sana na wilaya badala yake nipande Gari za MASASI nishukie NDANDA halafu baada ya hapo nimpigie simu atanipa maelekezo. Baada ya hapo dogo akasema nisubiri hapa hapa gari za masasi zitapita, kweli baada ya dk chache ikaja Costa ya kwenda masasi nikauliza nauli konda akasema 4000 nikaguna kidogo nikamwambia nashukia NDANDA akasema ni 4000 nikaona isiwe tabu nikapanda safari ikaanza. Masaa mawili hivi baadae tukafika ndanda nikashuka. Nikawa nimebakiwa na buku teni tu mfukoni (10000).kufika ndanda nikamfata jamaa mmoja alikuwa anauza mahindi ya kuchoma kandokando ya barabara Nikamwomba simu yake nimpigie huyo mkuu wa shule ya CHINONGWE anipe maelekezo jamaa akasema simu yake haina salio ila bahati nzuri kulikuwa Kuna mteja anasubiri hindi pale akadakia akasema taja namba tumpigie. Nilipompigia akasema Kuna dreva bodaboda anamtuma mda si mwingi yupo hapa ndanda aje kunichukua kwa hiyo nisubiri kwa huyu muuza mahindi nanimwambie nimevaaje ili amuelekeze huyo bodaboda ila nisiondoke kwa huyu muuza mahindi atanikuta.
Kweli baada ya nusu saa jamaa akatokea alivyofika tu akasema Kuna jamaa nimekuja kumchukua anaenda kijiji kinaitwa CHINONGWE nikamwambia ni mimi hapa. Tukapanda kuelekea CHINONGWE, huko ni mbali sana halafu barabara niyavumbi usafiri ni shida maana ipo Costa moja tu inayopita njia hiyo kwenda nachingwea na ikipita hakuna tena usafiri zaidi ya bodaboda, kwa mujibu wa huyo bodaboda alivyosema. Ilikuwa ni safari ndefu mno yenye mabonde mengi Sana lakini mida ya saa kumi na moja jioni tulifanikiwa kufika chinongwe sekondari. Baada ya kufika mkuu wa shule akapigiwa simu na bodaboda ili apewe malipo yake yule mkuu akasema mwambie huyo kijana akupe mm hapa niko mbali na pesa Sina pia. Yani hapa ndonilichoka bodaboda akasema huwa ni 10000 ila kwa huyu mwalimu huwa anamfanyia 7000 nikasema mm Sina pesa jamani huku nikionyesha uso wa huzuni na majanga. Jamaa akapiga simu tena, mkuu wa shule akasema nitoe 5000 elfu mbili watamalizana wao. Ikabidi nilipe 5000 nikabaki na buku tano tu mfukoni.
Nilipofika kumbe mkuu wa shule alikuwa amemwambia makamu wa shule aje anipokee. Makamu wa shule ya sekondari chinongwe aliyefahamika kwa jina la JAFE akaja kunipokea akasema tuingie ofisini. Huyu makamu alikuwa mbinafsi sana afu ana katisha tamaa lakini mbeleni nitaeleza alivyokuja kunisaidia. Makamu akaenda nje kumwita mwalimu flani alikuwa anasimamia ujenzi wa shule na mwalimu flani hivi ni mdada wakiiraki au wamburu wa babati, walipokuja makamu akasema jamani tuna mgeni lakini huyu mgeni atakuwa analipwa na nani hapa?. Mimi nikadakia nikamwambia mm staki malipo ila nipate pakula na kulala tu, wakacheka ila mm nilikuwa very serious maana sikutaka kabisa masihala tena. Yule makamu akawa anamlaumu mkuu wa shule akisema huyu kijana atatufedhehesha tu maana hana simu, pesa ya sabuni ataipata wapi, pesa ya mafuta na mengineyo na wewe unaogopaga kuchangisha wazazi kulinda nafasi yako. Mizozo ilipoanza nikaona yule madamu wakiiraki akasema jamani huyu mkaka anaonekana uso ni mzito kachoka sana na mda huu ni saa moja kasoro ebu tumtafutie sehemu ya kulala.
Yule madamu akaenda kufanya usafi nikatandikiwa nguo kwenye sakafu maana walisema hawakupewa taarifa mapema hivyo godoro hamna mm nikasema haina shida. Nikiwa nimelala njaa inaniponda usiku wa saa nne hivi naona makamu anasukuma mlango maana hauna komeo kutokana na kile chumba kina mda hakina mtu hivyo hakikufanyiwa matengenezo. Alipokuja akasema mimi nakushauri hapa uondoke kijana hii shule mm ndomkongwe hata huyu mkuu kanikuta, hii shule haina rasilimali yoyote utaishije humu bila pesa??. Sikutaka kumjibu zaidi ya kuwa kimya ghafla nikaona sauti ya pikipiki mjengoni makamu akaenda nje kupokea mzigo flani mwenye pikipiki akasepa. Kumbe zilikuwa CHIPSI YAI aliniagizia nikala nilipokula akasema nipumzike ila asubuhi nifanye mchakato kwingine pale hapanifai maana huyu mkuu wa shule anakurupukaga bila kuwashirikisha na hata hivyo nitafedheheka mbele ya wanafunzi maana ukiwa huna pesa unaonekana tu. Mimi nikalala kusubiri kesho yake tuzungumze yote mbele ya mkuu wa shule alienihakikishia kwa asilimia mia kuwa sitaondoka.
....... Inaendelea usichoke......
Kuna mijitu haijui hata papuchi inakaa sehemu gani, Yani ipo ipo tu.Wambulu wanapatikana Kanda ya ziwa ipi?