Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Kuharakisha maisha tu, nyumbani sikuwa na shida yoyote ile kila kitu uhakika, na niliaga vizuri tu japo walisikitika kwa maamuzi yangu. Baada ya kumaliza fm 4 nikaona kula vya bure nyumbani inatosha, nikasema nitafute changamoto mpya.

Mambo yalivyokuwa magumu nikapiga simu kwa mama anitumie hela japo sikufanikiwa kuitoa kutokana na changamoto ya mawakala kutoka makete hadi ikonda sikuona wakala. Kutoka Makete hadi Ikonda nilitembea masaa matano kwa mguu.
..
 
Pole sana,
Lkn watu wa Pwani huwa hatusemi "samaki zangu" ni samaki wangu, na sio kwa samaki tu ni kwa viumbe hai wote hata wakiwa wadogo zaidi ya utitiri, unatakiwa useme "utitiri wale" ng'ombe wale sio ng'ombe zile na viumbe hai wengine wote ni huvyo.

Lkn pia nikupe sifa yako,
kuwa hakuna tukio uliloliacha maana hata pale ulipokunywa maji uliangalia saa kuwa maji ulikunywa kwa muda gani.
Nishangazwa zaidi na watu wa pwani walisema"MVUA ANAKUJA"
 
------SEHEMU YA KUMI NA TATU - - - - -

Nilipoona pamepambazuka nikashuka kwenye mti nikawa naelekea barabarani kuona kama kweli usafiri upo maana kwa mazingira ya kawaida Ile barabara unaweza Dhani hakunaga bus linalopita pale. Kama dakika sita hivi nikawa nipo maeneo ya barabara huku nikiwa naona wamama na wazee wakiwa wanaenda kwenye kazi zao za kila siku ikiwemo kilimo na ufugaji,ile nikiwa nimetulia nikawaza kama pesa yangu ipo mfukoni kuangalia mfuko wa nyuma siioni kucheki mfuko wa mbele nikaikuta nikasema hapo sawa Sasa nina Amani ya moyo japo kiasi lakini kwa kuwa nauli ninayo ninatumai kila kitu kitaenda Sawa. Baada ya mda mchache Kuna Dada alipita karibu yangu nadhani alikuwa anakatiza kwenda shambani maana mbele kidogo kulikuwa Kuna mashamba ya ufuta alipopita mm nikawahi kumsalimia Kisha nakamuuliza bus huwa linapita saa ngapi, huyu Dada akasema saa tatu ndohuwa linapita japo Kuna mda linaweza kuwahi pia.

Nikamwambia Asante kumbe inabidi nikae chonjo mda ndio huu yule Dada akauliza kwani unasafiri au unapokea mgeni? Nikamwambia nasafiri ndio maana nipo na begi la safari yule binti akaguna akaendelea na safari. Baada ya dakika kadhaa nikaja kugundua kumbe nimechafuka taabani Shati ipo hovyo, suruali chafu mwili wote haupo sawa nikasema hivi hapana itabidi nitafute sehemu yenye maji ninawe tu uso then kwakua kwenye begi Kuna Shati bado sijavaa Ile itanisave. Kuja kuangalia nikamwona yule Dada bado hajafika mbali kwa kuwa mimi ni kamanda ikabidi nikimbie kumuwahi mpaka nikamfikia, nikamwambia samahani Dada sijasahau chochote ila nilikuwa naomba kama una maji ninawe tu uso nitashukuru sana. Bahati nzuri alikuwa na maji kwenye kidumu cha Lita tano akafungua vimizigo vyake kulikuwa kuna kikombe ameweka akamimina maji nikanawa japo sikuwa na mafuta nikasema haina shida maana hakuna anaenijua huku. Yule Dada akaendelea na safari zake mm nikabaki pale nikafungua begi ili nibadilishe Shati japokuwa suruali ilikuwa chafu ila uzuri ilikuwa na rangi ya kaniki kwahiyo nilipangusa vumbi kwa maji nilikuwa nanawia ikakaa poa ila ukisogea uchafu unaonekana tena mwingi tu.

Nilipofungua begi nikakuta Ile Shati ndohaitamaniki kabisa kumbe yule jamaa aliefungua begi langu kule polini aliipakaza midamu pia alikuwa nguo zote anazibwaga chini na pale chini ndosehemu pia walichuna yule mnyama, nikiangalia hii niliovaa nayo kituko bora yenye midamu ila shida ni nyeupe zile damu zinaonekana kila sehemu. Ikabidi niende kwenye mti flani nikakaa kutuliza kichwa changu maana kupanda kwenye bus na Ile hali sio rahisi. Nilikaa kwenye ule mti baada ya hapo sikuelewa kilichoendelea kumbe nikajiinamia nikapiga usingizi mzito sana. Nikiwa kwenye ndoto nikawa nasikia sauti "wahi upande kaka bus linaenda mbali hili". Nikakurupuka kutoka usingizini kuangalia mbele nikasikia muungurumo wa bus na nipo mbali kidogo na barabara maana nilipoenda kumfata huyu binti anisaidie maji sikurudi barabarani kwahiyo nikaanza kukimbia kwenda barabarani mpaka bus nikiwa naliona kwa macho yangu linapitiliza huku nikimbwata kwa nguvu sauti yenye mlipuko "SIMAMAAAAAAA“....." SIMAMAAAAAAAA", lakini holaa juhudi hazikuzaa matunda Sasa pamoja na bus kupitiliza ilinibidi begi nilishike kwenye mkono nikavuta pumzi baada ya hapo niliondoka kwa kasi ya kulipuka kama Mbape anaechezea Monaco kwa mkopo, dakika sifuri nipo barabarani huku nikiwa napukuta mkono kwenye site mirror ya dreva maana bus halikuwa mbali sana nikaona mwendo wa bus umepungua na kusimama kabisa. Nilipofika kwenye gari nikapanda safari ikaanza Ile naingia ndani kutafuta siti kila mtu ananishangaa ninavyovuja mijasho niponipo tu wenge la kutosha nikawa sipo sawa kimsingi.

Tukapita mpaka maeneo ya Ile shule ya chinongwe huku nikiwa na huzuni sana. Nilipoenda kukaa kulikuwa Kuna Dada mmoja tukakaa nae ila ajabu nikuwa kila mda alikuwa ananiangalia nilivyo kwa jicho la kuibia mm nikawaza nikasema ndoishakuwa hivi Sasa nitafanyaje. Safari iliendelea ikafika mda nikarelax tu na gari ilipokaribia main road konda akapita kuchukua nauli nikamwambia mm nina 22000 Sina 25000 akasema toa, nikampa akarudisha 3000 yangu huku safari ikiendelea na uelekeo ni Dar Es Salaam japo baada ya hapo itabidi niende mkoa wa pwani mlandizi huko ndokuna rafiki wa baba angu nilielekezwa nikakae. Tukapita baadhi ya vijiji ila tulipokaribia lindi mjini eneo moja linaitwa DARAJANI ni mbele kidogo kutokea mnazi mmoja ukiwa unaelekea lindi mjini, Bus la machinga likaharibika ikawa ni saa tano kasoro hivi. Nikajua ni hitlafu tu baada ya dakika kumi hivi tutasepa. Kumbe tatizo lilikuwa serious sana walihangaika kulitengeneza zaidi ya masaa matatu lakini hakuna kilichofanyika kufika saa nane hivi abiria wakaanza kuwaka wakidai waagiziwe bus jingine ili tuweze kuondoka. Kumbe tulikuwa tunabwata tu maana wafanyakazi wa lile bus wote waliondoka akabaki dereva peke ake. Abiria wakasema kama hamtaki kutuletea bus jingine mtupe nauli zetu.

Mpaka inafika saa tisa hakuna jipya, ilibidi abiria mmoja apige simu kwa traffic polisi waje eneo husika na baada ya mda wakafika huku wakimkoromea dreva kwanini hataki kupiga simu kwa boss alete bus jingine ili abiria tuondoke na kila abiria alisema hata saa sita usiku wao wataondoka hawataki kulala lindi. Wale polisi wakapiga simu kwa boss akaja meneja wa kampuni ni mwarabu kembamba hivi kilikuja na harrier nyeusi huku kanagonga konyagi. Kalipofika kakauliza KIDAGAA yupo wapi? Yule dreva akasema kidagaa kaenda mjini anakuja mda si mwingi, nadhani kidagaa ni yule konda. Abiria wakawa wanawaka kweli huku njaa zimetuponda nikaona yule meneja mwarabu anajibu kwa dharau akisema "Mnawahi wapi nyinyi acheni kututisha" halafu anaongea mbele ya polisi huku anavuta sigara. Kitendo kile kilinifanya nikakwazika sana nikajisemea moyoni "your richness can't buy our dignity", ikabidi ninyanyuke nikamsogelea nikaona kashtuka huenda kutokana na mwonekano niliokuwa nao nikamwambia usiogope NAOMBA NIRUDISHIE NAULI YANGU kakajibu kwa jaziba kakasema mpumbav wee leta hiyo tiketi, nikatoa tiketi mfukoni kakaangalia halafu kakaingia mfukoni kakanipa 23000 yangu kakasema haya katafute gari Lako nikamwambia poa. Ni kaingia kwenye bus nikachukua begi langu nikakaa pembeni kuangalia ustaraabu mwingine. Baada ya mda kidogo huyo kidagaa akafika na spea ili watengeneze chapu bus liondoke, walikukuruka lakini wakaufyata.

Ngoma ilipoonekana ni ngumu ikabidi yule mwarabu aagize Kosta yake sijui inapiga root gani akasema iende haraka GEREJI ifanyiwe service ya kutosha maana inabidi ipeleke abiria Dar Es Salaam halafu pia wachukue Costa yoyote hapo lindi mjini ije uchukue abiria wake wakakae pale stend maana kuendelea kukaa pale darajani ni kupoteza mda. Kweli baada ya Lisaa Costa ikafika kuwapakia wale abiria wote wakiwa na mizigo yao tena zilikuja mbili ili waweke kambi lindi mjini kusubiri Kosta yake ifanyiwe service waondoke kwenda Dar Es Salaam maana gari kubwa lilikuwa halitengenezeki tena kwa mda huo. Costa zilipofika tu yule mwarabu akasema pakia wote ila huyu jamaa alierudishiwa nauli simtaki tena nadhani kwanza hata muonekano wake akili zake haziko Sawa. Kidagaa ambae ndomfanyakazi wake anaemwamini akasema 'imeisha iyoo'. Abiria wote wakaondoka nikabaki mimi tu maeneo yale na baadhi ya mafundi waliokuwa wanalinda lile bus.

Sina hili wala lile nikaona bus limewaka ila boss wao akasema walipeleke sehemu moja inaitwa mnazi mmoja wakalilaze, huenda bado lilikuwa na shida somewhere. Kwahiyo wakaondoka wote mimi nikabaki pale huku nikishuhudia jua linazama kwa macho yangu bila kugusa chochote mdomoni lakini safari yangu haina matumaini tena kama mwanzo. Nilikaa sana pembeni kidogo mwa Ile barabara mpaka mida ya saa moja hivi Kuna Majamaa yakapita nikayauliza kama nitapata msaada wa usafiri wakasema wao sio wa husika wa mambo hayo ila sehemu nilipo si salama Kwangu inabidi niondoke maana pale darajani Kuna matukio makubwa ya kiharifu huwa yanatendeka. Nikaona hapa nimelikoroga ikabidi nitulize akili yangu vizuri nikasema ngoja kwanza niangalie zile namba za simu kwenye karatasi za yule mzee wa mlandizi nikipata simu nimpigie kuwa sitafika Leo ila labda kesho mda wowote maana kama saizi ni saa mbili kasoro mlandizi nitafikaje Leo Leo. Nikachukua begi nikafungua zipu ya mwisho maana ndonahifadhi namba kwenye karatasi na line yangu ya simu. Kuja kucheki sioni line wala karatasi yenye namba za simu. Nikasema hapana hili ni wenge tu ngoja niangalie vizuri, nilipekua begi Zima sikuona line yangu yenye pesa 20000 niliyotumiwa na baba wala karatasi yenye mamba zangu muhimu [emoji22], nilikuja kugundua yule mpumbav wakule polini aliekuwa anakagua beg langu hovyo bila ustaraabu ndoaliangusha hivi vitu kwahiyo nikawa nimekosa vyote. Sasa ngoma iliyobaki nikutafuta usafiri mida hiyo ikawa ni saa tatu kasoro usiku kwa kuhisi na eneo nililopo niliambiwa si salama sana kwahiyo hapanifai inabidi niondoke.

......... Inaendelea usichoke.........
Njooo redio free Africa, RFA usimulie hiii simulizi utakuwa zaidi ya zabron, na rojazi
 
Aisee hv nikitaka ile story ya rojas naipaje kwenye mitandao humu...yan yule jamaa ni teja ila cha ajabu anajua kuhadithia utafkiri unaangalia movie....ile trip yake ya south ilikuw ni hatari mbaya aisee[emoji23]
Kuna watu walikuwa nazo sijui walizifuta, maana jamaa anaongea sio poa na ametuliaaa, mzee wa Jo - beg
 
Back
Top Bottom