Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Sitosahau safari yangu ya Lindi iliyojaa maumivu na tabu nzito

Hii hadith umeanza jichanganya sehemu nyingi ukiwa na lengo la kuionogesha. Unataka matukio mengi sana mpaka unakosea. Hilo la huyo binti kumtaka inaonesha kabisa hukujipanga vizuri kulielezea. Na hilo la Majangiri kuwasha moto mkubwa kiasi cha wewe kutembea dk 45 kuufikia ni uongo mwingine ambao hukujipanga.

Mwendo wa kuuona moto umbali wa dk 45 ni moto mkubwa sana ambao majangiri hawawezi hatarisha maisha yao hivyo. Na hapo ukataja bunduki SMG eti uliifahamu sababu ulipitia JKT acha kufanya watu wote humu watoto. Wewe andika hadithi kama hadithi si lazim udanganye kuwa yalikukuta.
Wivuu
 
Watu wazima uzima upi? Jamaa anachokosea ni kutaka kuwaaminisha watu wenye akili kuwa story ni ya kweli wakati ni ya kutunga. Hilo hatuwezi likubali. Aende zake huko. Wamemtoa kwenye group alilokuwa aki copy na kuja ku paste huku. Wakimrudisha ataleta tena story. Aache kutudanganya sisi wenye akili.
Unaweza kutuwekea vyeti tuone akili nyingi ulizonazo?
 
Kuna mdau safuher alichambua vizuri tukio like na kuweka maoni yake ila kwa ufupi kipande kile kina mambo mengi ambayo ni ngumu kuamini kwa watu ambao wameishi uswahilini na kujua nature ya vibaka japo wote hawalingani .

Ukiaacha jinsi alivyochoropoka aliniacha hoi jinsi alivyopambana nao na matukio mengine kwenye kisa hiko hapo mood yote ya kufuatilia iliisha nikabaki kuwa msomaji comments kutokana mtu hukujipanga kisaikolojia kama utapigwa na kitu kizito kichwani..
😂😂😂😂😂😂😂
 
Mtoa simulizi nilikwambia,ukifika sehemu ya demu iruke hujanielewa,unaona sasa yaan kwa kutaja demu tu ushaanza kupoteza ladha na watu pia wataanza tena kuitilia shaka hadthi yako kwasbb haingii akilini ngumu sana kuwaza mwanamke kwenye situation ile,hiyo moja , pili ni kwamba ulitumiwa hela 20000,simu ya makamu ulikuwa nayo wewe na uliulizwa una shngap ukasema huna hela so ile twenty uliotumiwa ulipokea kwa mtindo gani?
Alieka line yake ata mi nlikuwepo......kuhusu kadem lazima aweke story ili kunogesha, sa story gan kavu isokuwa na mapenzi
 
Inanikumbusha mwaka 2011 niliacha nyumbani kila kitu kizuri kuanzia chakula cha uhakika mpaka sehemu nzuri ya kulala. Nikaenda wilaya ya tatu eti kutafuta maisha. Kuna usiku mmoja ulikuwa mgumu sana kwangu, sitasahau.
Tupe story kwa urefu kiasi Mkuu.
 
Back
Top Bottom