Sitosahau Siku niliyobeba gunia la maiti, nikizani ni samaki

Sitosahau Siku niliyobeba gunia la maiti, nikizani ni samaki

Mshumaa_Tz

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2020
Posts
681
Reaction score
2,501
Sitokuja kusahau Mwaka, 2017 baada yakuwa nimehitimu chuo.

Nililiamua kutafta kibarua chochote ....hill kujiingizia kipato...lakini ....mipango yote ikabuma kama sio kufifia.

Baadae nikaona kwakuwa nina Umbo fulani, mwili nyumba....nikajua hapa, nikiomba Kibarua cha kulinda sikosi..

Basi..baada ya siku ..kama Mbili nikaanza kufight kukipata kibarua...lakini sikufanikiwa kupata...kampuni..ambayo inalipa vizuri, Nikabidi nijiunge kwenye kampuni X ambyo mshahara wake ulikuwa , kama elf 90 per month.

Baada yakuanza ajira yangu mpya kwa , msoto mkali nakufanikiwa kupata mshahara wangu wa kwanza.

Nikaona nianze kuwa nanua samaki kwenye ziwa Asubuhi then mchana natembeza kwenye beseni , majumbani mwawatu.

STORI YAKUBEBA MAITI INAANZA HAPA
kutokana na tamaa za pesa, siku moja nimekwenda ziwani kununua samaki..nikakutana na gunia kubwa limefungwa vizuri likinukia harufu ya samaki wabichi.

Hapo ndipo akili ilinituma kuwa huu mzigo umeibiwa ndo maana umefichwa, basi, niliamua kuubeba kichwani hili niondoke nao, nikaanze maisha mapya yenye nafuu.

Mara naona mzigo umekuwa mzito mithili ya chuma....basi ...nikajipa moyo ...kwamba samaki waliomo ndani ya gunia niwengi sana ,

Ndipo nilipoamua kufungua gunia hili nitenganishe nusu kwa nusu......ndipo Mara paap!!!!! Nakutana navipande pande vya maiti Aiseeee.....nilikimbia speed 100 ...nakuamaua kuhama ule mji ....nakujikita kwenye shughuli tena za ulinzi.

To be honest life is not easy.
 
Mkuu pole sana katika kutafuta mengi lazima upitie


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unashangaa Kuna Degree Holder mmoja yeye sababu anafanya kazi mshahara mdogo /Hana kazi kutwa nzima kulia lia nakujilaaani ovyoovyo.


Nyinyi kuna watu wana pitia mambo makubwa sana !!!


Kwakweli JF ingawa kuna matangopori pia, Humu kuna Watu kupitia shuhuda zao, Unapona kabisa !!.

"What is yours will always be yours no matter what "
 
Huyo jamaa uliyemtaja mkuu nikioana jina lake tu huwa nacheka sana na kukumbuka nyuzi yake ya sintomsahau mjomba. Humo kuna mambo ya kutaka ajira ya udaktari na elimu ya darasa la saba. Pia alikuwa anafanya kazi Tanesco na mjomba hakumwambia madhala ya umeme akapigwa shoti wakati anafanya connection
ya wire nyumbani. 😂😂
 
Huyo jamaa uliyemtaja mkuu nikioaga jina lake tu huwa nacheka sana na kukumbuka nyuzi yake ya sintomsahau mjomba. Humo kuna mambo ya kutaka ajira ya udaktari na elimu ya darasa la saba. Pia alikuwa anafanya kazi Tanesco na mjomba hakumwambia madhala ya umeme akapigwa shoti wakati anafanya connection
ya wire nyumbani. [emoji23][emoji23]
Kile kijamaa kichizi sana, nimeona nyuzi zake nimeishia kuwa mtazamaji. [emoji3] [emoji3]

Leo kaja na uzi wa ku-inspire vijana wa Dar sasa huo ushauri wake uchuro utupu.
 
Daah nimecheka sana mana navuta hisia kamanakuona live kwenye tukio vichakani. Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom