Mwaka 2008, April 17, Ijumaa, nilibanwa na mkojo nikiwa kwenye costa, katika Stendi ya Kabwe, Mbeya Mjini, kuelekea Mwakaleli. Kabla gari haijaondoka, nikaenda kukojoa uwanjani karibu na Barclays Bank. Kabla sijamaliza mkojo, nilikamatwa na jamaa fulani hivi, na akataka kunipa kichapo. Hapakuwepo na choo. Ilibidi nipige magoti na kumuomba msamaha, ndipo akaniachia. Nikarudi garini. Wasafiri wenzangu walinipa pole maana waliishudia sinema ile. Sitosahau! Na sijawahi kuisimulia hii kadhia popote zaidi ya hapa JF.
Sitosahau nilivyokamatwa kwa sababu ya kodi ya baiskeli kule Nachingwea
pole sana mkuu, hiyo inatokea sana ktk mazingira ya safari hasa ya mabasi.
kumbe kuna watu JF Wamekula chumvi! mkuu mwaka gan! ulilipa kodi ya kichwa.
Mwaka 2008, April 17, Ijumaa, nilibanwa na mkojo nikiwa kwenye costa, katika Stendi ya Kabwe, Mbeya Mjini, kuelekea Mwakaleli. Kabla gari haijaondoka, nikaenda kukojoa uwanjani karibu na Barclays Bank. Kabla sijamaliza mkojo, nilikamatwa na jamaa fulani hivi, na akataka kunipa kichapo. Hapakuwepo na choo. Ilibidi nipige magoti na kumuomba msamaha, ndipo akaniachia. Nikarudi garini. Wasafiri wenzangu walinipa pole maana waliishudia sinema ile. Sitosahau! Na sijawahi kuisimulia hii kadhia popote zaidi ya hapa JF.
Sitosahau
KODI YA KICHWA ILIVYO WATESA WAZAZI WETU.
Hii ilikuwaje Mkuu, fafanua kidogo.
Hii ilinyanyasa sana watu.
Watu walikuwa hawazalishi mali kutwa nzima ni kujificha
Tu milimani.
Au ni kuwafungia wazazi ndani ili mgambo wakija tunasema hawapo, mbaya zaidi walikuwa wanavunja
Na milango ili kuangalia kama kuna watu.
BIG GUP SANA MR CLEAN JAPO WATU WANAKUPONDA
ILA ULIFANYA VIZURI KUFUTA HII KODI.