Sitosahau wema niliofanyiwa

Sitosahau wema niliofanyiwa

Under-cover

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2023
Posts
1,834
Reaction score
3,042
Habari wakuu, nimekumbuka wema nikiowahi kufanyiwa hatimaye mpaka sasa tumefanyika kuwa ndugu, kuna watu wana mioyo mizuri na wema ndani yake.

Ipo hivi 2020 kipindi niko chuo, ilikuwa imefika muda wa kwenda field na ilikuwa ni jijini Dar es salaam, basi nilikuwa na best angu yeye ndio kwao na anakaa kwa kaka yake GOBA, ila sikuwa nimepanga kufikia kwao ila nilitaka tu nikapange.

Basi bwana pembeni ya nyumba yao kulikuwa na jirani walikuwa wamezoeana sana hasa best angu, alienda kuniombea kukaa pale kwa mwenye mji, na alikuwa na familia yake mke, vijana wanne wa kiume ambao wawili ni rika langu, hawa wengine wadogo walikuwa, nikakubaliwa , nikapewa room ya nje ambayo tulikuwa tunalala na wale vijana.

Sasa kwa akili yangu nilijua nitakuwa kama mpangaji, na kulipa bills zote kwa muda nitakao kaa siku 49, kwa maana field yangu ilikuwa ni Kibaha kwenye kampuni moja hivi, ila nilishangaa sana kwakuwa hawakutaka nilipe chochote, nilikula bure, nilala bure, maji umeme vyote nilitumia bure, hawakuwahi kunitenga, walinifanya mwanafamilia, mpaka muda wa sebuleni wananiita naenda kukaa nao, nikienda field jioni nikirudi nakuta chakula.

Nilishangaa sana upendo niliooneshwa, nami kulipa fadhila nilihakikisha nafanya kazi pale home, kusaidia vyombo na usafi wa hapa na pale, japokuwa naweza sema ile familia kuna ushua fulani hivi pesa ipo na pembeni nakumbuka blaza alikuwa anajenga gorofa la kupangisha, na pia kulikuwa na nyumba kapangisha , ila mimi hakunidai chochote. Siku ya ibada ikifika Jumapili wao wanaenda wanapoabudu na mimi wananiacha niende nakoabudu, tulipendwa sana blaza pamoja na mke wake. Hata pia rafiki angu kwao ni kwakishua na blaza wake alilalamika sana kwanini hakumwambia ningekuwa nakaa pale ila sijui ni mipango ya MUNGU.

Mpaka siku naondoka walinambia nikitaka kwenda kuwaona niende tu kwasababu nimeshakuwa mwanafamilia.

NAWAPENDA SANA NA IPO SIKU NITAWALIPA FADHILA ZAO KWANGU MUNGU AWATUNZE ILE FAMILY.🙏
 
Mimi pia nimesoma msingi mpaka university hadi napata kazi nikiwa kwenye mikono ya watu mbalimbali na si ndg wa damu.

Wapo nilioweza lipa fadhila kidogo maana hata nitoe nini siwezi lipa wema wao hata robo.

Wengine hata sijui walipo kwa sasa ila nawaombea kwa Mungu azidi kuwabariki kila iitwapo leo.
Ama kweli, Dunia hii ina watu na nusu!
 
umesema alikuwa anajenga nyumba ya ghorofa ya kupangisha si ndy
 
Watu wema Bado tunaishii...karibu Tena ,awamu hii ukimaliza chuo karb Tena tukakupa ajiraa
 
Back
Top Bottom