Habari wakuu, nimekumbuka wema nikiowahi kufanyiwa hati maye mpaka sasa tumefanyika kuwa ndugu, kuna watu wana mioyo mizuri na wema ndani yake.
Ipo hivi 2020 kipind niko chuo, ilikuwa imefika muda wa kwenda filidi na filid yangu ilikuwa ni jijini Dar es salaam, basi nilikuwa na best angu yeye ndio kwao na anakaa kwa kaka yake GOBA, ila sikuwa nimepanga kufikia kwao ila nilitaka tu nikapange.
Basi bwana pembeni ya nyumba yao kulikuwa na jirani walikuwa wamezoeana sana hasa best angu, alienda kuniombea kukaa pale kwa mwenye mji, na alikuwa na familia yake mke, vijana wanne wakiume ambao wawili ni lika langu, hawa wengne wadogo walikuwa, nikakubaliwa , nikapewa room ya nje ambayo tulikuwa tunalala na wale vijana.
Sasa kwa akili yangu nilijua nitakuwa kama mpangaji, na kulipa bills zote kwa muda nitakao kaa siku 49, kwa maana filidi yangu ikikuwa ni kibaha kwenye kampuni moja ivi, ila nilishangaa sana kwakua hawakutaka nilioe chochote, nilikula bure, nilala bure, maji umeme vyote nilitumia bure, hawakuwahi kunitenga, walinifanya mwanafamilia, mpaka muda wa sebureni wananiita naenda kukaa nao, nikienda filidi jioni nikirudi nakuta chakula.
Nilishangaa sana upendo nilionyeshwa, nami kulipa fadhila nilihakikisha nafanya kazi pale home, kusaidia vyombo na usafi wa hapa na pale, japo kuwa naweza sema ile familia kuna ushua flani ivi pesa ipo na pembeni nakumbuka blaza alikuwa anajenga gorofa la kupangisha, na pia kulikuwa na nyumba kapangisha , ila mimi hakunidai chochote. Siku ya ibada ikifika jumapili wao wanaenda wanapoabudu na mimi wananiacha niende nako abudu, tulipendwa sana blaza pamoja na mke wake. Hata pia rafiki angu kwao ni kwakishua na blaza wake alilalamika sana kwanini hakumwambia ningekuwa nakaa pale ila sijui ni mipango ya MUNGU.
Mpaka siku naondoka walinambia nikitaka kwensa kuwaona niende tu kwasababu nimeshakuwa mwanafamilia. NAWAPENDA SANA NA IPO SIKU NITAWALIPA FADHILA ZAO KWANGU MUNGU AWATUNZE ILE FAMILY.🙏