gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 790
- 1,373
Jina langu ninaitwa Soka (sio jina halisi) na kwetu ni huko Moshi uchagani. Nilisoma kwa shida na kufanikiwa kupata elimu ya Sekondari na kisha kujiunga na mafunzo ya ualimu katika chuo cha Marangu na kuhitimu kwa kutunukiwa Daraja A. Baada ya kuhitimu nilipangiwa kituo cha kazi ni huko Kwamsisi mkoani Tanga katika shule ya msingi Kwamsisi.
Nilivyofika nilishangazwa sana na mazingira ya shule na kijiji kwa ujumla. Kwanza nilipokelewa na wazee wa kijiji walio nionya sana kuhusu kile kijiji, wakaniambia niwe makini. Mzee mmoja aliyejitambulisha kama mzee Kingalu akanipatia kipande cha mfupa na kuniambia kuwa ni lazima nilale nacho ili niweze kuwa salama.
Niliogopa sana, nilipelekwa kwenye nyumba ya walimu ilikuwa ni nyumba ya bati iliyojengwa kwa kuta za miti na kusilibwa vizuri kwa udongo pia iliezekwa kwa bati. ilikuwa ni nyumba yenye hadhi kwa eneo hilo kwani asilimia kubwa ya nyumba za pale kijijini zilikuwa ni nyumba za udongo na kuezekwa na nyasi.
Siku ya kwanza nilipoingia shuleni ili niweze kutambulishwa nilishangazwa sana na mazingira yalivyokuwepo. Wanafunzi walikuwa ni wengi mno na walimu tulikuwa watano tu, ilikuwa ni mimi na mwenzangu wa kike tulioripoti ndani ya wiki hiyo pamoja na walimu wengine watatu akiwemo mzee mmoja mstaafu aliyeombwa kuhudumu hapo shuleni.
Siku niliyoripoti walimu wenzangu walinishangaa na kunionya kuwa kama sikuwa na kinga yoyote basi hapo kijijini sito paweza. Mimi niliwajibu kuwa siamini kabisa kwenye nguvu za giza na ninaimani kwa Mwenyezi Mungu kuwa ndiye atakaye nisaidia kwani mimi ni mkristo Mkatoliki. Nikatambulishwa mbele ya wanafunzi na mimi nikajitambulisha.
Siku hiyo nilifanya maandalizi kadhaa kwa ajili ya kipindi na kisha kuanza kazi yangu ya kufundisha. Siku za mwanzo nilishangazwa na umakini wa wanafunzi darasani, wengi walikuwa wakinitazama kwa makini na wengine walikuwa hawaongei wala kujibu chochote hata ukiwauliza maswali wakati wa kipindi, nilikuja kugundua kumbe walikuwa ni kama wamelala huku wakiniangalia kwa sababu ilikuwa hata nikiwashtua kwa kuwatingisha walibaki wakinitazama tu!
Nyumba yangu niliyopewa na uongozi wa Kijiji ilikuwa pembezoni kidogo na eneo la shule, na kama mnavyojua mazingira ya kijijini, nyumba ilikuwa pembezoni mwa kijiji. Siku moja nilivyokuwa nikirudi kutoka kazini, mtaani wakazi wengi walikuwa wakinitolea macho ya mshangao kama vile walikuwa wakinitamani sikuelewa hawakuniongelesha kwa lolote na nilivyo wasalimia wengi wao hawakunijibu walibaki tu wakinitazama! Niliwaona baadhi yao wakininyooshea vidole kama vile wanaelekezana kitu, mimi nilitembea haraka haraka kuelekea yalipo makazi yangu.
Nilifika nyumbani kwangu, vile naufungua tu mlango nilishangazwa kuona mnyama kama panya akitoka ndani ya nyumba yangu kwa kasi kubwa sana kupitia mlango mkuu wa kuingilia sebuleni, alikuwa amebeba mfupa! Nilishtuka sana baada ya kuingia chumbani kwangu na kuukosa ule mfupa niliopewa na mzee Kingalu, nikatambua kwamba uliondoka na yule panya niliyepishana naye pale mlangoni.
Nilivyofika ndani kwangu nikafanya utaratibu wa kuandaa chakula na baada ya kula nikajipumzisha kitandani na kupitiwa na usingizi totoro. Nilishtuka niliposikia jina langu likiitwa, "Soka! Soka!" hapo kijasho chembamba kikanitoka na nilipotazama mlangoni ulikuwa ni mwanga mkali sana na sikuweza kuona kitu chochote nikafikiria ni nani huyo aliyekuwa akiniita kisha nikaisikia tena ile sauti, na mara hii kwa mtetemo.
"Wewe ni mgeni hapa kijijini Kwamsisi, ila umewakasirisha wavyele(wazee wa kimila) kwani ulijiwekea zindiko la mfupa bila ruhusa ya wavyele. kwa hiyo mambo yatakayo kupata ni makubwa mno!"
Mimi nikawajibu kuwa ule mfupa nilipewa tu na mzee Kingalu na wala yeye hakuniambia kama ni zindiko hata hivyo jana nilivyo rudi kutoka kazini sikuukuta ule mfupa kwa hiyo kama ni zindiko mimi sina. Yule mtu akacheka sana na kuniambia kuwa yule panya niliyemuona sio panya wa kawaida bali ni mtaalamu wa kutegua mabomu ya kichawi, kisha ile sauti ikapotea na hapo mimi nikashtuka kutoka usingizini. Nilihisi kuwa huwenda ikawa ni ndoto tu iliyokuwa ikinisumbua japokuwa nilikuwa naogopa sana nilichukua biblia yangu nikalala nayo huku nikisali rozali.
Pia, soma: Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi-2